Kingi, hivi huyu jamaa alisomea Arusha Tech College miaka ya 80 mwishoni?
Kuna jamaa aliniacha pale na alikuwa na jina kama hilo na sina habari zake zaidi.
Nakumbuka tu kuwa alikuwa akisomea Electrical Engineering na ni mtu wa Musoma.
Hata akiwa pale TCA, alikuwa ni moja ya viongozi (waziri) wa misosi. Wakati wake kama sikosei kulizuka mgomo na ilikuwa kasheshe maana Mzee Isa Mushi wakati huo ni Mkuu wa Chuo kabla hajahamishiwa wizarani, alihaha na kuanza kutoa vitisho vikali ambavyo vilikuwa havimtishi kabisa Maligo.
Awe asiwe, Mungu ampumuzishe na kuwafariji ndugu na jamaaa...... Amen.