Jengo si la Manji tena, sehemu kubwa ni la PSPF- Shirika la serikali, na waliomo mle ndani ya jengo ni wafanyabiashara mbalimbali wazalendo wazuri tu watazania. Inasikitisha kushabikia kuungua moto kwa jengo. Ni muhimu kutofautisha umiliki kwa maana ya kuwa na haki na mali fulani na Mali yenyewe.
Mimi niko radhi tuibiwe kama tunavyoibiwa kila kukicha kwenye migodi na makampuni kama ya bia, mabenki nk, ilmradi fedha hio isitoke nje ya mipaka ya tanzania. Wewe iba lakini pesa ibaki Tz kwa maana ya kujenga majengo kama hayo ya Quality Plaza na mengine. Maana hata Manji akifa au akikimbia nchi bado tunakuwa nayo. Ndio maana nafikiri si sahihi hata kidogo kwa mlioshabikia mali kuungua! Ni mali yetu haiondesheki ile ni yetu. Atakapochukuwa nchi jemadari, atasawazisha mapato yote yatokanayo na mali (assets) kama hizi. Lakini kama watakuwa wamekimbiza huko Jersey sio rahisi!
Hivi mnajua ni Bongo tu unaweza ukaingia kwenye Bureau de Change, ukatoa Dola hata 50,000 ukauza na wala usiulizwe tena wewe ni Mtz, na ukienda na vijisenti vyko ni Bongo tu unaweza kununua any amount of dola bila kuulizwa chochote, na bila kupewakaratasi lolote! Ndio hivyo! Ndiyo maana nchi inaliwa. Tujipe pole kwa kuunguliwa mali yetu pale Nyerere Road. Tutumaini jeshi letu la uokozi wa moto limenusuru mali na maisha!
Mkuu maneno mengi ya nini?
Hili jengo ni matunda ya ufisadi uliokubuhu, jengo limenunuliwa na pesa ya wananchi kwa bei ya mara tano ya market price.
Sasa watu wakicheka ni kuwajia juu wale walionunua na kuona kama hiyo pesa itarudi?
Hata kama ililipiwa bima!!!
Ufisadi unaumbuliwa hata kabla hawajastaafu.
We mwenyewe ukiungua nitachekelea:becky:Very Low contribution...Hivi kwakuwa Voda wapo Mafisadi wa CCM, basi ikiuungua au kufilisika Tuchekelee...? au watu wakifa Migodoni tuchekelee eti tu kwakuwa viongozi wetu wamekula Rushwa?...Endelea mjenzi wa Taifa
misleading, pump za fire zina uwezo mkubwa sana wa kutupa maji kwa hiyo usishangae dakika tatu tu maji yameisha, then wanalaumiwa fire. katika miji kunatakiwa kuwe na fire hydrants kwa ajili ya fire fighting lakini sijaona kwa sasa hiyo kitu kwenye miji yetu. long time ago mji wa iringa ulikuwa na hii kitu ila sina hakika kama bado mfumo upo.kama kawa magazeti yataandika kuwa magari ya fire yalifika bila kuwa na maji
Mkuu kama wewe ni fisadi uliyekubuhu, siku ukiungua nitakunywa Tusker bariiiiiidi!Very Low contribution...Hivi kwakuwa Voda wapo Mafisadi wa CCM, basi ikiuungua au kufilisika Tuchekelee...? au watu wakifa Migodoni tuchekelee eti tu kwakuwa viongozi wetu wamekula Rushwa?...Endelea mjenzi wa Taifa
Kuna habari zimetangazwa na Redio one kuwa Jengo la Quality Plaza (nyerere Road) linaungua, kwa wale waloko eneo la tukio tunaomba mtuhabarishe.
Mod Naomba uihamishe hii baada ya 2 hours
hii ilishaletwa kama breaking news humu siku zilizopita