Qualifications Za kujiunga na JWTZ

Qualifications Za kujiunga na JWTZ

chumvichumvi

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2010
Posts
1,207
Reaction score
312
Katika pita pita yangu kwenye website mbali mbali za serekali nilikuta vigezo vinavyoitajika kwa mtu kuweza kujiunga na jeshi la wananchi wa tanzania ambazo ni
Askari
Mtu yeyote ataandikishwa kujiunga na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa sifa zifuatazo: -

Awe raia wa Tanzania
Awe na Elimu ya kidato cha nne na kuendelea na awe amefaulu..
Awe hajaoa/hajaolewa
Awe na umri kuanzia miaka 18 hadi 25
Awe na tabia na mwenendo mzuri
Awe na akili timamu na afya nzuri
Masharti ya Utumishi
Askari atapewa nambari ya utumishi baada ya kufaulu mafunzo ya awali.
Atalitumikia Jeshi kwa kipindi cha mwanzo cha miaka sita, baada ya hapo atafanya kazi kwa mkataba wa miaka miwili miwili kwa kibali cha Mkuu wa Majeshi.
Maafisa
Bodi ya Uteuzi wa Maafisa (Officers Selection Board)
huwafanyia usaili askari wenye elimu ya kidato cha sita na kuendelea toka Vikosini na Shule za askari wapya (Recruitment Schools).
Watakaofaulu masailiano hayo hupewa hadhi ya Afisa Mwanafunzi (Officer Cadet), na hupelekwa Chuoni (Tanzania Military Academy) kwa mafunzo ya uafisa kwa muda wa mwaka mmoja.

kwa ufafanuzi zaidi cheki link hiyo hapo chini
Kujiunga JWTZ | JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA
 
We unafikiri yanazingatiwa hayo. Watoto kutoka maporini ndo wataambiwa hivyo.
 
  • Thanks
Reactions: B40
We unafikiri yanazingatiwa hayo. Watoto kutoka maporini ndo wataambiwa hivyo.


Hallo MAKOLE hapo kweny umri kidogo panatatiza
hususani kama utazingatia mfumo na mzunguko wa elimu hapa
kwetu it is obvious at least 25yrs old you can find graduate
for first degree,so naona wengi hapa tutaikosa hiyo fursa kwa kigezo umri.
 
Hallo MAKOLE hapo kweny umri kidogo panatatiza
hususani kama utazingatia mfumo na mzunguko wa elimu hapa
kwetu it is obvious at least 25yrs old you can find graduate
for first degree,so naona wengi hapa tutaikosa hiyo fursa kwa kigezo umri.

Believe me LUKELO, age is nothing but a number katika nchi hii, sema hutakwenda, sio hatutakwenda kwa sababu unasuffer peke yako kwa kuwa hayupo anayekusimamia.
 
Vigezo vinazingatiwa sana sema kukona exceptional
 
By the way from the source new in takes zitakuwa mwakani either january mwishoni au feb mwanzoni kwa iyo vijana endeleeni kupasha uko mliko
 
Kuna watu hawakuwa na uwezo wa kwenda Secondary lakini wana uwezo mzuri tuu kiakili, kiafya na akipewa mafunzo anaelewa vizuri
Nafasi zao kwenu ni zipi?
 
Mkuu kigezo cha umri wamewapa nafasi hadi umri wa miaka 33. so ni muda mrefu sana wametoa ni nafasi za wataalam hapo huajiri ma engeneer, daktari, wanasheria na taaluma zingine unazozifaham.
 
Kuingia jeshini sikuizi yani ni kuna magumashi balaa especially kwa hao wanaojiita profeshino, tafuten kaz nynge, ni ushauri tu!!
 
Dnt gv up, kwa wale wanaotaka kuptia jkt leo nlkua na mshaur wa jkt wilaya ya kino kaxema nafac znatoka mwez wa 5 mwshon o wa 6 mwanzon xo anzen kupasha
 
Back
Top Bottom