Q-NET naomba pesa yangu milioni 5, nimenunua saa mpaka sasa najuta kuwafahamu

Kwani ulivyoingia uliambiwa utapata iyo pesa mara 2 hata kama hujafanya kazi?? Ulipitia presentation zote ukaelewa biashara au uliingiaje.....Hakuna pesa za bure hata siku moja katika Dunia hii..Lazima ustruggle ndo uipate..Kama wewe uliingia ukijua Qnet ni kama Desi au D9 kwamba unaweka pesa then unapata pesa bila kuisotea basi ulipotea njia,utaishia kusema umu kwenye mitandao kwamba Qnet ni matapeli lakini mwisho wa cku utarudi tu na utafanyakazi mana Qnet ni Life time business...Utaondoka kimwili lakini kiuhalisia bado uko...TC yako inakungoja ukaitendee haki...
Qnet sio Pyramid scheme eti waliotangulia ndo wananufaika, mfano mzuri ni kama wewe umetangulia kuingia lakini kwa sababu ya kutokuelewa biashara umeamua kutulia na kuanza kuandika ujinga kwenye mitandao, sasa kuna mwenzio ataingia kesho ataielewa biashara atafanya kazi na kugundua kwamba Qnet ndo biashara aliyotakiwa kuifanya miaka 3 iliyopita ila hakupata iyo fursa......If you look for Negativity, You will get negativity and Viceversa is true....Muwe na mchana mwema......Good morning
Rudisheni pesa zake acheni utapeli
 
Pole kwa kuwa one of their victim! Hawa jamaa ni waongo sana! One of my friend did fall on their trap too! Kabla hajajua kuwa katapeliwa, akataka anipeleke huko! Akaanza nisumbua, Tukutane nkupeleke mahali, Nataka tuwe "Business Partners" Its something huge! Nkimuliza whats that? Hataki kusema! Nkaona isiwe shida, siku moja nkatoka kazini akanipigia simu nkamwambia lets meet! Akanielekeza Office ya kukutana, As unaelekea Mawasiliano kama unatokea Mwenge, unakata kushoto kama unaenda Sinza Makaburini, then Kuna kama ghorofa jipya linajengwa, ofisi yao iko opposite na hilo jengo! Nafika kila anyenisalimia ananambia "good morning".. I was like "what the **** guys, Its almost 7PM.." Wakaningiza kwenye ofisi, Kisha akaja dada na jamaa angu wakaanza nsomesha! Ki ukweli kilichonifanya niwasikilize ni heshima na urafiki nliokuwa nao na mshkaji.. Nlijisikia vibaya kusikia kuwa mshkaji kashalipa 4.4M.. I looked at him with a face of "You've been fucked up dude".... Yule dada bila kujua kuwa nlishawahi kumuona Morroco BRT akigombania gari za Kimara, ati ananidanganya kaacha kazi CRDB, She was a Bank Operations Manager and She was getting 3.5M as Net salary, ila kaacha vinye QNet inalipa... Na ameshafanikiwa nunua Her new ride (Of her dream... Nissan Juke)...

Nliondoka pale na hasira za kucheleweshwa kwangu, plus foleni nlokutana nayo barabarani... Baada ya mwez mshkaji wangu anakuja analia hajarudisha hata 100 kwenye ile 4.4M yakeee alotoa... Mbaya zaid alichagua kifurushi cha travel discounts, na hawana hotel hapa bongo so mpaka akisafiri majuuu! Dah! Nlicheka sanaaaa.... Nkamwambia My friend, there is no such an easy money! You of all the people should have know that!
dah.... Hawa qnet walisha mtapeli mdogo wangu na yeye akawa anajitahidi kunishawishi niende hata kuwa sikiliza tu nkamwambia hata kuwasikia tu sitaki maana na mimi miaka ya nyuma kidogo nlishawahi kuingizwa mkenge na watu wa GNLD wakani toa upepo wa 50k kama kiingilio na hamna faida nliyo wahi kupata.
Nkaaapa sitakaa nijihusishe na biashara ya aina yoyote ile ya Network marketing.
 
Qnet naomba muwe waungwana mlimshawishi mke wangu na shemeji watoe milioni 8 ambayo walinunua saa mkasema baada ya miezi 13 watapata bilioni 3.3, mbaya zaidi mkamwambia don't share the information. Yaani mnafanya siri mazungumzo, hela mke katoa lakini mnamzungusha sijui mnasema apeleke mtu mwingine tena ndo alipwe, nyie ni matapeli wakubwa na kesi iko police.

Nawapa onyo mkinishinda mahakamani naenda Gamboshi kuwaroga, nyie watu wa ajabu mlianza kwangu baada ya kunipiga porojo zenu nikawashitukia mkamdanganya mke na shemeji na hii njia yenu kutusalimia good morning hata jioni nahisi ndo njia ya kuwapumbaza watu, nawaambia io hela mtaitoa, mama yangu msukuma.
Mkuu naona umefikisha malalamiko yako kwa dada yetu
371b19d2fc1221fe5166a956f0466f7b.jpg
 
au wanatumia ndumba,reasonable man hawez akatoa ela yake kijinga hivyo
Hawa watu wanatumia nguvu za Giza sana hasa kwenye second presentation kiuhalisia kama wakikuita na ulikuwa huwajui na hela unayo lazima tu watakupiga ...wanatumia sana psychological weapons mixer na nguvu za mashetani... Wanaochomoka kwa hawa jamaa nibwale wenye uelewa na network marketing, waliowah kuisikia hii qnet, na wale ambao hawana hela...ila kama hela uanyo na huna idea yyte ya network marketing, na hujawah sikia kuhusu Qnet...kupigwa ni kufikia tu...mi nilinusurika na hawa jamaa cse nilimshirikisha Mungu ndo akanitoa salama salimin...jamaa yangu aliacha kazi ya mshahara wa laki saba akajiunha na hawa watu now yupo more frustrated sana....na amechakaa sana...Mungu amsaidie aisee daaah inauma somtym
 
Aisee pole sana mkuu
Kuna binti nilisoma nae Chuo kipindi cha nyuma kidogo;
Sasa mwaka Jana mwishoni akanipigia simu (nilikua sina namba yake)..baada ya kujitambulisha nikamkumbuka akaanza sana kunichangamkia mpaka na kuniita maneno ya kimahaba, Mara my dear, my honey yaan ushenzi mtupu.
Lengo lake kuu lilikua ni kuni capture mind ili iwe rahisi kuweza kuniita ofisini kwao.
Siku ya siku kweli nikaingia line akanidanganya my dear naomba kesho uje uone shughuli ninazofanya ofisini kwangu kila nikimuuliza unafanya shughuli kubwa hivo mpaka unataka ugeni? Hakunijibu huku akinisisitiza wew njoo tu (it was my surprise)
Yaan baada ya kufika hapo kebbys hotel (mwenge)
Ni good morng huku ni saa Tisa alasiri yapata..nikajiuliza hawa ni freemason nin..!? (Kimoyomoyo)
Na cha kushangaza zaidi kila mtu ananiita jina langu.
Nilikaa nikisubiri niingie ndani (huyo binti alidai anaanda chumba kwaajili yangu).
Mara baada ya kuingia ndani nilipewa lecture ya watu kama wawili, kila mmoja akidai alikua anafanya kazi nzuri tu Mara engeener, Mara alikua kwenye NGO's za wazungu.
Baada ya kuwafahamu hao Qnet na kwa namna inavyolipa wakaona haina haja ya kuendelea na kazi isiyolipa wakati QNet inalipa mamilioni ya pesa.
Cha kushangaza kila mmoja alikua ananipa mafanikio ya operational manager wao tu kuwa amenunua gari aina ya prado tx ya milioni 40 kwa mda mfupi.
Nashukuru mungu uhuni huo niliushtukia kwa maana nilishatapeliwa na akina forever living huko.
Huyo binti alianza kuniita kwenye second presentation ili nichague nanunua nin kwenye products zao.
Toka siku aliyonieleza huo upupu Mpaka kesho hata message yake sijibu.
 
Qnet naomba muwe waungwana mlimshawishi mke wangu na shemeji watoe milioni 8 ambayo walinunua saa mkasema baada ya miezi 13 watapata bilioni 3.3, mbaya zaidi mkamwambia don't share the information. Yaani mnafanya siri mazungumzo, hela mke katoa lakini mnamzungusha sijui mnasema apeleke mtu mwingine tena ndo alipwe, nyie ni matapeli wakubwa na kesi iko police.

Nawapa onyo mkinishinda mahakamani naenda Gamboshi kuwaroga, nyie watu wa ajabu mlianza kwangu baada ya kunipiga porojo zenu nikawashitukia mkamdanganya mke na shemeji na hii njia yenu kutusalimia good morning hata jioni nahisi ndo njia ya kuwapumbaza watu, nawaambia io hela mtaitoa, mama yangu msukuma.
Mkeo kwa nn atoe kiasi hicho cha fedha bila kukushirikisha wewe?
 
Bora hata wangesema unanunua gari kwa milion 8 ili ikizinguz unauza hata kwa milion 5.. Unarudisha pesa kidogo sasa saa ya milion 8 kaiuze hata elfu 20 mtu anagoma labda buku 10
Hahaha aisee Mimi waliniambia nianze na SAA ya laki 6.
Nilitamani kuwajibu pumba nikavunga tu nikasepa kimya kimya
 
Back
Top Bottom