Q-NET naomba pesa yangu milioni 5, nimenunua saa mpaka sasa najuta kuwafahamu

Qnet naomba muwe waungwana mlimshawishi mke wangu na shemeji watoe milioni 8 ambayo walinunua saa mkasema baada ya miezi 13 watapata bilioni 3.3, mbaya zaidi mkamwambia don't share the information. Yaani mnafanya siri mazungumzo, hela mke katoa lakini mnamzungusha sijui mnasema apeleke mtu mwingine tena ndo alipwe, nyie ni matapeli wakubwa na kesi iko police.

Nawapa onyo mkinishinda mahakamani naenda Gamboshi kuwaroga, nyie watu wa ajabu mlianza kwangu baada ya kunipiga porojo zenu nikawashitukia mkamdanganya mke na shemeji na hii njia yenu kutusalimia good morning hata jioni nahisi ndo njia ya kuwapumbaza watu, nawaambia io hela mtaitoa, mama yangu msukuma.
Looh! Umoja katika ndoa yenu unatia shaka! Wewe walitaka kukutapeli ukawastukia. Haya, mkeo hukumwambia. Mkeo kauvaa mkenge, m.8 hiyoooo imechomoka halafu inakuja hapa jamvini na mikwala bubu! Aaah haya buana, hiyo pesa ikirudi niite nikufundishe biashara ya ku make fasterfaster.
 
Mkuu naona umefikisha malalamiko yako kwa dada yetu
371b19d2fc1221fe5166a956f0466f7b.jpg
dah jamaa kwa Id fake hadi insta... Ila pole yake aisee ml 8 parefu
 
kuna jirani yangu alikuja akaniambia hiii kitu nikamwambia naenda kufuga kuku na hizo hela akabisha sasa kila nikisoma huku huwa namtumia link hadi sasa hazifungi wala kusoma whatsup zangu.

Ila ukweli sisi ni wasahaulifu sana ilianza DECI watu hawakusikia ikaja D9 haya mara foverev living sasa mara bitcoin na bado watu wanajiunga. No short cut in life
"Vichwa panzi" na "tamaa mbele"
 
Nenda tu Gamboshi, hiyo hela hupati na mahakamani huwezi shinda maana hawa jamaa wanavibali, wanachokuambia ni wekeza ktk mfumo wa kununua, ukishanunua ujue umeshampa aliyekushawishi kamisheni, sasa ili upate na wewe tafuta fala mwingine umshawishi anunue ili upate kamisheni, product ya million 8 uliyokwishaichukua in a form of purchasing itawezaje kutengeneza hela for you, haiwezekeni..Qnet ideology is to fool someone then train him to fool others to earn money!
Hehehehe

Ova
 
Back
Top Bottom