Q-NET naomba pesa yangu milioni 5, nimenunua saa mpaka sasa najuta kuwafahamu

Nimepigwa na hawa wezi wa Qnet wamenishawishi nikaingia nikanunua SAA mil 5 nitapata Mara mbili zaidi ya hapo.

Naomba mnipe pesa zangu tutauwana Mwaka huu mil 5 hivi hivi, then mpaka sasa bila bila nitakuja ofisini kwenu na polisi mambo ya utapeli iwe mwisho kabisa.
Fikiri kabla ya kutenda hahahaaaa
 
Rafiki yangu nahisi aliinginzwa mkenge na hawa watu ingawa hakuniambia direct ila niligundua.

Aliniomba nimkopeshe laki 2 akidai anataka kusolve ishu muhimu na kuniahidi atanilipa baada ya wiki 2, nilimpa bila kinyongo nikiwa na imani hela yangu itarudi baada ya muda mfupi alioahidi.

Wiki 2 zikapita, mwezi ukapita hadi mwaka mambo bila bila, baada ya mwezi kupita nikaanza kumdai na akaanza kunipa ahadi, ahadi zikageuka ahadi hewa.

Nikakomaa sana kumdai hadi akafikia hatua akasema nilijichanganya hivyo nadaiwa hela kubwa sana na anaendelea kupambana ili aweze kulipa hizo hela. Hadi hapo nikagundua aliingizwa mjini kwa mtindo huu wa utapeli.

Kuna kipindi nikawa na shida ya hela, nikamcheki anilipe, nikaishia kuzawadiwa block, urafiki ukafa nikapiga moyo konde. Kuna siku tulikutana sehemu aliponiona akala kona fast(akanikimbia).

Baada ya miaka 3 na ushee nilimkomalia akanilipa, tangu alinipe tumeishia kuangaliana status WhatsApp tu.
 
Mimi huwa sikopeshagi jibu langu ni moja sina .
 
Huu ni ujinga wa kiwango cha juu sana,
Na kama umri wako ni zaidi ya 25 ukienda polisi nawashauri wakuweke kwanza mahala ule viboko 20 asubuh mchana na jione angalau akili ikukae sawa
 
Nadhani kuna umuhimu wa financial education katika shule zetu. Haiwezekani ukapata pesa mara mbili without creating any monetary value. Utakuta saa uliyoinunua thamani yake haifiki hata 10% ya gharama uliyolipa, hiyo pia ni insanity. Kwa wenzetu Ufaransa supermarkets haziruhusiwi kuuza hata kwa hasara, that's how seriously they don't want mess-ups with their financial systems. Ila hapa kwetu unaambiwa utapata pesa mara kumi zaidi ya ulichotoa unashangilia, utafikiri pesa inapatikana kwa ramli. If a deal is too good to be true, it might not be true.
Nawashangaa sana watu wanaoingia kwenye pyramid schemes. Ili upate return kwenye investment yako, lazima uwashawishi watu wengine wanunue valueless stuff. Fikiria Watanzania wote wajiunge, wale wa mwisho kujiunga watamshawishi nani ajiunge ili nao warudishe investment yao? The people at the bottom of the pyramid must pay the price and you sound to me that you are paying that price.
Wake up Tanzanians.
Nchi hii tunahitaji ukombozi wa fikra , wabongo wengi tunahitaji easy money ndo maana hata betting kwa sasa zimeshika hatamu, zilianza za mpira siku hizi eti unatoa buku unapata milioni kumi, radio kila dakika zinapromote ndani ya dk 10 matangazo ya betting ni dk 5 nzima mara chota mihera mara patatapata mara tatu mzuka serikali yetu ipo kimya TCRA wako kimya , ulishasikia wapi uchumi wa nch unajengwa na betting? .Hatuajaishia hapo korokoro za wachina kila kituo cha bodaboda vijana wanacheza mia mbili mia mbili .
 
Pamoja na kelele zote hizi, bado vijana wa kule vijijini wanaingizwa kwenye mtego huu masikini, niliona ile ripoti maalum ya ITV, wanatia huruma sana, serikali chukueni hatua ya kuelimisha wanchicjuu ya utapeli huu, na wa kulaumiwa ni yule kuwadi wao Kigwangwallah
 
Kungekuja makampuni ya aina hii ya Q-NET kama matano hivi, labda akili za watz zingechangamka.
Wamezubaa sana!
Kuna dada niliona kwenye ITV ripoti maalum eti kanunua chakula kinaitwaje sijui kwa milioni 8, kuulizwa nini cha zaidi eti wanadai hiko ni chakula kina vitamini na madini gani sijui, sasa si ukale matunda tu ya shs.5,000/= utapata hizo vitamin?!
 
😂😂 Naskia raha na furaha sana nikiskia kuna wapumbavu kama hawa wametapeliwa
 
😂😂 Naskia raha na furaha sana nikiskia kuna wapumbavu kama hawa wametapeliwa
Watanzania bwana kila eneo wanapigwa,DECI walipigwa,Ukimwi wamepigwa,Corona wamepigwa,kwenye elimu wamepigwa,Kilimo wamepigwa,Afya wamepigwa!You can't imagine,vipo vyeti vya kuzaliwa vya mkono!Yaani ni kupigwa tu kila eneo
 
Back
Top Bottom