Q Chilla: Mimi ni Shabiki wa Diamond, natamani kufanya kazi naye

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,515
28,487
MKALI wa wimbo wa ‘Mkungu wa Ndizi’ aliyerudi kwa kasi katika muziki wa Bongo Fleva, Abubakari Shaaban maarufu Q Chiller, amesema kwa sasa anatamani kufanyakazi na Diamond Platnumz.

Q Chiller alifafanua kwamba anatamani kufanya kazi na Diamond kwa kuwa wote wana uongozi unaojua kazi zao lakini anajipanga kwanza kwa kuandaa wimbo mzuri utakaowawezesha kurudisha fedha zao kupitia mialiko mbalimbali ndani na nje ya nchi.

“Najipanga kurekodi wimbo na Diamond, naamini wimbo huo utaishi na tutatengeneza fedha za kutosha nitamweleza cha kufanya ili wimbo huo usiwe mwepesi maana tunatakiwa tutoe wimbo utakaokuwa mfano wa kuigwa na wasanii wengine,” alieleza Q Chillar.

Aliongeza kwamba licha ya kuwa maarufu pia yeye ni shabiki wa msanii huyo ndiyo maana anatamani kufanya naye wimbo kutokana na uwezo alionao wa kubadilika badilika unaomsaidia kurekodi muziki bora akitolea mfano wimbo wa ‘Sing’ alioimba na AKA wa Afrika Kusini.


Source: Mtanzania
 
Chila alisema Mondi anatembelea nyota yake, mpaka Mondi aka mind....sasa kibao kimegeuka yeye ndio anataka kudandia nyota ya Mondi.......hebu ngoja tuone.
 
Itakuwa collable la nguvu, tena waongezee na vionjo vya saxaphone itabamba Sana.
 
diamond alishawahi kusikika akusema, wajkat akiwa mdg nyimbo za Q-chiller zilikua znampagawisha sana
 
Q - chief simwamini hata kidogo huyu jamaa ni kigeugeu na ni MNAFKI sana tena sana,kuna anachokitafuta si bure. Mimi nashauri asifanye nae nyimbo yoyote na asijiweke karibu nae kabisa na amuogope kama ukoma marafiki zake karibia wote ameshawahi kugombana nao.
 
Q - chief simwamini hata kidogo huyu jamaa ni kigeugeu na ni MNAFKI sana tena sana,kuna anachokitafuta si bure. Mimi nashauri asifanye nae nyimbo yoyote na asijiweke karibu nae kabisa na amuogope kama ukoma marafiki zake karibia wote ameshawahi kugombana nao.
point, diamond hawe makini na hawa wanafiki watamlostisha
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom