Pwani: Hali ya Ulinzi yaimarika Kibiti

Pwani: Hali ya Ulinzi yaimarika Kibiti

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
28,197
Reaction score
64,643
Wananchi wa Kibiti mkoani Pwani wametakiwa kuendelea na shughuli zao za kimaendeleo na kijamii ikiwemo kushiriki katika ibada misikitini na makanisani kutokana na kuimarika kwa hali ya ulinzi na usalama mkoani humo.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro alipokwenda kuwatembelea baadhi ya wananchi mkoani humo kufuatia kuuawa kwa wahalifu 13 katika eneo la Gari Bovu, kijiji cha Chamiwaleni, Kata ya Mchukwi, Wilaya ya Kibiti, Mkoa wa Kipolisi Rufiji.

IGP Sirro pia amewapongeza askari Polisi wote kwa kazi nzuri waliyoifanya na kuongeza kuwa Jeshi la Polisi litaendelea kusimamia sheria na mtu yeyote atakayevunja sheria ni lazima ashughulikiwe kwa mujibu wa sheria.
 
Hivi wale waliouawa msikitini taarifa yao nao imekaaje?
 
Pongezi kwao Polisi
Ila wahakikishe wanawasafisha kweli kweli, wasimwache hata mmoja
 
Back
Top Bottom