Putin sends in his most ruthless special forces killers to finish off jihadist

Putin sends in his most ruthless special forces killers to finish off jihadist

Kwa jinsi wanavyosifiwa hao spetsnaz huko chechniya kusingekuwa na waasi wa miaka na mikaka

Hehehee nafikiri ni vile waasi wanakawaida ya kujichanganya na raia wa kawaida. Huwa ni ngumu saana kuwatofautisha.
 
afadhali bhana, isis wanasumbua sana aisee
 
Donald Trump the republican presidental candidate support this move done by Russia.

Mkuu kati ya raia wa Merikani wanao wania kiti cha Urais, binafsi naona Donald Trump fits the bill, jamaa huyu ana akili sana mtulivu hana papala, uwezo wake wa kifedha unamfanya awe huru katika mahamuzi yake, hilo tu linamfanya hasingiliwe na mabepali wa viwanda vya kuhunda silaha kumshinikiza kuanzisha vita kila kona ya Dunia ili wahuze silaha zao.

Trump amesema mara kadhaa kwamba yeye hana tatizo na Putin, actually aliongeza kwamba yupo tayari kushirikiana nae kwa madhumuni ya kuleta amani Duniani, Donald Trump ananikumbusha sana utawala wa Bush Jr ambae 4 some reason alikuwa karibu sana na Putin na mambo yalikuwa yanakwenda vizuri tu baina yao, uhusiano wa Merikani na Urusi umekuja tibuka baada ya Obama kuingia madarakani, yamekuwa mabaya zaidi katika term yake hii ya mwisho!! Wakati mwingine nashindwa kuelewa who is Power ndani ya Whitehouse - je, ni Obama mwenyewe au Ma-neocon wanaongozwa na kichaa mwenye asili ya Poland (Zbigniew Brzezinski) huyu mzee chuki zake kuhusu URUSI zinapitiliza mipaka - muda wote anashinikiza Serikali ya Merikani kuishambulia na ikiwezekana kuikalia URUSI - linajisifu eti "Nuclear war is winnable", si rahisi kuelewa kama yuko mentally sound au la! Kajisahau kabisa kwamba nchi yake alikozaliwa alikombolewa kwa Damu ya Warusi wakati wa mapigano ya WWII.

Wamerikani wamejaliwa kwa propaganda za vijiweni, ukweli ni kwamba Warusi hawana mpango wa kupeleka wanajeshi wake huko Syria, habari zilizo letwa humu ukisoma kwa umakini utaona ni propaganda tu za kutaka kuwachafua Warusi ambao wanefanikisha kuwasambaratisha ISIS kwa kiwango kikubwa - mark you operation hii hajazidi wiki moja lakini imeweza kufanya kazi nzuri kuliko ya wa Merikani/NATO ambao karibu mwaka unakatika bila ya kupata mafanikio yoyote dhidi ya ISIS - actually hawakuwa na nia thabiti wa kuwaodoa ISIS huko Syria zaidi ya kuwapatia silaha ili wangushe Serikali halali ya Bashir El Asaad, mafanikio ya URUSI imewahuma sana Wamerikani hawependi kabisa Mataifa mengine yafanikiwe pale wao walipo shindwa, Merikani inakereka sana kuona URUSI inafakiwa kuwadhibiti ISIS - Dunia for the first time baada ya WWII ndio imeshuhudia umahili wa Taifa hili katika fani ya sayansi ya silaha, mafunzo mahili ya Airforce yao, Navy nk nafikiri watatumia kikosi kidogo cha ma commando ku-mop up remnant ISIS huko Syria.

Wamerikani wana Wivu wa kike,majigambo na kizitisha tisha Nchi za NATO kuhusu an imaginary threat kutoka Urusi - nchi za NATO wanacho sahau ni kwamba hizo ni mbinu chafu za Merikani za kutafuta uhalali wa kuendelea kubaki Continental Europe wakijifanya wanawalinda, lengo lao kuu ni kutaka kutumia Nchi hizo kusambaza silaha kuizingira Urusi wakiwa na imani kwamba vita ikifumuka Baina yake na URUSI basi vita hiyo itapiganwa huko Ulaya na si Merikani - wana mawazo ya kitoto kabisa!!

Wamerikani wakae wakijua kwamba wakijisahau na kujaribu kuishambulia URUSI basi huo ndio utakuwa mwisho wa TAIFA lao, kwa nini nasema hivyo: Taifa la URUSI lina taarifa ya siku nyingi kuhusu mpango kabambe wa Merikani na Uingereza wa kutaka kuishambulia URUSI na kukalia mali asili yao, mipango hii ilihanza kusukwa mwishoni mwa WWII - Waziri mkuu wa Uingereza Churchill alitaka Urusi ishambuliwe mapema baada ya WWII kwa kutumia silaha za nuklia lakini Truman alimwambia kwamba Urusi ni Taifa kubwa kieneo, Merikani kwa wakati huo haikuwa na mabomu ya kutosha ya nuklia kuweza kusambaratisha/shinda URUSI, hivyo walipaswa kuhairisha mpango huo kwa takribani miaka mitano ili waweze kuhunda mabomu ya nuklia ya kutosha kutekeleza malengo yao, mpago huo ulikuwa shelved kwa muda sio kwamba ulihachwa kabisa waliogopa baada ya Warusi kuhunda mabom ya nuklia.

Intelijinsia ya URUSI ilipo pata taarifa kuhusu mpago wa Merikani na Uingereza kuishambulia kwa kutumia mabomu ya nuklia, basi na wao wakafanya juu chini kuhunda nuklia bom wakawa wamefanikiwa ndani miaka mitatu, baadae wakahunda hydrogen bomu - Warusi ndio walikuwa wa kwanza kuhunda thermonuclear bomb lakini ma Yankee yatakueleza adithi nyingine tofauti kabisa, lakini ukweli wa mambo unabaki pale pale kwamba wenzao ndio wanzilishi, baadae Warusi wakapeleka mwana anga wa kwanza kwenye outer space, experience walio gain Warusi katika uhundaji roketi zenye thrust kubwa ya kurusha vyombo vyenye uzito mkubwa angani ndio uliwafanya Warusi wawe wa kwanza vile vile kuhunda silaha za ICBM - Merikani ilikuja kufuata baadae kabisa, kwenye mwanzoni mwa miaka ya sitini Warusi walilipuwa thermonuclear Bomb lenye Nguvu kubwa kuliko yote Duniani mpaka leo karibu miaka hamsini imepita hakuna Taifa lolote limewahi kufikia record hiyo tukiwekea maanani kwamba actually wanasayansi wa URUSI headed by Dr.Andrei Sakharov wali-scale down uwezo wa mlipuko to 50 MegaTonnes za TNT, design ya mwanzo ilikuwa ni a 100MT, wanasansi wakasema hapana tukilipua bomu la 100MT litaleta madhala makubwa sana - swali ni je hivi sasa Warusi wana mabomu/silaha zenye uwezo wa kiasi gani - remember that was fifity years ago si hilo tu cha kushangaza zaidi ni kwamba bomu hili lilihundwa ndani ya wiki 17!! Why? Warusi walipata habari kwamba Merikani na Uingereza wanataka tena kufufua mapingo wao wa kuishambulia Urusi kwa kutumia silaha za Nuklia, ninacho taka kusema hapa ni kwamba inapokuja suala ya Warusi na Taifa lao watafanya lolote ndani ya uwezo wao kijilinda kwa nguvu zao zote - they know that once bitten twice shy - hawawezi kukubali tena kupoteza raia wao kwenye vita kama walivyo poteza raia wao zaidi ya million ishirini wakati wa mapigano ya WWII, Merikani ilipoteza laki saba wakati wa mapigano ya WWII, vita ya kweli hajiwahi kupiganwa ndani ya Taifa la Merikani zaidi ya Civil War na kuwaua wahindi wekundu bila sababu!

Nikiona baadhi ya members wanabeza beza uwezo wa wanasayansi wa Urusi katika nyanja za silaha nawashangaa sana, Ma Yankee yatabaki kupiga piga makelele na kufanya Mataifa yasielewane, yatavamia vinchi vidogo vidogo kama Afghanistani,Libya, former Yugoslavia, Iraq lakini ukweli wa mambo wanajua kwamba hawana ubavu wa kupigana vita na a real McCoy.
 
tommorrow;14261001]Nina wasiwasi isije ikawa kama afghanstan miaka ya 1980 ambapo nyuma ya taliban kulikuwa na us, german na uk. Na mrusi akashindwa vita iliyodumu miaka 10. mimi huwa siwaamini US[/QUOTE]

Mkuu huo ndio ukweli wenyewe.Isis ni zao la U.S.Wako pale kudestabilize serikali zote "vichwa ngumu" za middle east na central asia ambazo nyingi ni washirika wa Urusi.

Hii vita ya Isis ni another C.I.A proxy war designed to prolong american military presence in the middle east kwa sababu za kiuchumi zaidi kuliko kutetea raia wanaoteseka wa Syria,Iraq n.k.

Wamarekani wanao uwezo wa kuifuta Isis in hours but that is not at their best interest.

Wamarekani walikuwa na uwezo wa kuifuta al qaeda duniani kote in just few months but again,kuifuta Al qaeda ni kuharibu covert operations za wamarekani zenye malengo ya kiuchumi sehemu mbali mbali duniani.

Mrusi anaelewa vema sana anachokifanya.Anapiga at the heart of American foreign interests.Ndio maana wanaoelewa mambo haya kwa undani wana hamu ya kujua mwamerika atafanya nini baada ya hapa maana "kaingiliwa" uani kabisa na kudhalilishwa.

Hata hivyo ni muhimu tukaelewa pia Mrusi nae yuko pale kulinda maslahi yake na si vinginevyo.Kama lisingekuwa eneo muhimu kiuchumi na kiusalama kwa Russia wala tusingewaona mashujaa wa Spetsnaz wakitoka kambini kwenda Syria.

Russia inafanya maandalizi makubwa kijeshi huko Syria na kuonyesha dhahiri kuwa targets zake ni kubwa zaidi ya vikundi vinavyompinga Assad.

Ukitaka kupata hints kidogo kuhusu mvutano huu inabidi uguse kidogo migogoro ya Iraq,Libya,South Ossetia,Caspian sea,Afghanistan na Ukraine.It's all about "oil politics".

Mrusi anaelewa kuwa American influence inapozidi katika eneo la middle east na Central Asia ndivyo uchumi na usalama wake unavyozidi kuwa mashakani kwani hayo ni maeneo yenye umuhimu mkubwa kwake kiuchumi,maeneo tajiri hasa kwa mafuta na pia kuna nchi muhimu kwake kijiopolitiki,zikiwamo zilizojimega toka U.S.S.R ya zamani.

Mataifa ya magharibi yamekuwa yakihangaika kupunguza utegemezi wao wa mafuta yatokayo nchi ambazo haziko friendly nao.Wameshaona jambo fulani linakuja huko mbele ilhali uchumi wao bado utategemea mafuta kwa miaka mingi ijayo.Wanatafuta other sources of oil ambazo zitakwenda sawa na maslahi yao mapana.Suala la oil exploration ni muhimu kwao,na pia Syria,Iraq,Kuwait etc ni muhimu kwao kuwa na influence.

Bahari ya Caspian kuna utajiri mkubwa wa mafuta.Kwa muda mrefu Urusi na Iran zinafanya harakati kubwa kuhakikisha eneo hilo linakuwa chini yao.Kusambaratika kwa Urusi kulitoa mwanya kwa Marekani na Ulaya kujiingiza eneo hilo zikijenga mahusiano na mataifa mabaki ya Urusi kama Georgia,Arzebaijan ili kudhibiti utajiri huo.

Kwa mfano,kuna bomba kubwa la mafuta kutoka Caspian sea chini ya Arzebaijan linalopita Georgia na Uturuki kusupply mafuta Ulaya ya magharibi lililojengwa na makampuni 11 makubwa ya mafuta ya West yakiongozwa na B.P.

Ni mojawapo ya jitihada za Marekani na washirika wake kupunguza utegemezi wa mafuta toka nchi washirika wa Urusi na pia kuikomoa Urusi kiuchumi.

Kurudi kwa Russia kama taifa lenye nguvu duniani kunaanza kufufua upya mgogoro katika eneo hilo ambapo bado makubaliano katika nchi zinazoshare Caspian sea bado hayajatengemaa huku Urusi ikijitahidi kurudisha ushawishi wake kwa nchi hizo.At the moment nchi hizo zimegawanyika huku Kazakhstan na Armenia zikiwa upande wa Urusi zaidi na Arzebaijan yenye utajiri mwingi zaidi kuliko wengine ikielemea West.

Caspian sea iko katika eneo muhimu kijiografia kati ya Urusi na middle east.

Mwaka 2009 Assad alikataa kusign mkataba wa kujenga bomba la gas toka Qatar(mshirika wa U.S) kwenda Uturuki through Saudi Arabia,Jordan,Syria halafu 2010 akaanzisha jitihada na Iran(mshirika mwenzie wa Urusi) kujenga bomba toka Iran kupitia Iraq kwenda Syria ili kuuza gesi Ulaya na muda haukupita machafuko yakapamba moto ndani ya Syria huku baadae Isis wakiiyumbisha serikali ya Iraq na Syria.

Mmarekani anafanya kila awezalo kuhakikisha middle east inanyonyeka kiurahisi,huku Mrusi nae kwa kutumia washirika wake kama Iran na Syria akihakikisha influence yake eneo hilo haiondoki.Na U.S,Saudia vs Iran,Russia ndio chimbuko kuu la tensions za sasa hivi kati ya usuni na ushia katika middle east.

Si ajabu sasa Russia anafanya maandalizi makubwa kijeshi kuliko uwezo wa wapinzani wa Assad ulivyo.Anajua nguvu iliyoko nyuma ya vikundi hivyo ndio size yake kijeshi,na si vikundi vyenyewe.

Urusi imeanza kuijenga upya kambi yake ya kijeshi ya Tartus nchini Syria,kambi pekee ya mbali ya Urusi ya zamani iliyokuwa imebakia baada ya Cold war.

Bandari ya Tartus ni base iliyotumika na Russian navy fleets zilizokuwa bahari ya Mediterania kwa ajili ya maintenance na supply ya ammunitions kwa washirika wake kama Iran.Sasa inajengwa ili kuweza kupokea meli za kivita na nyambizi za nyuklia za Russia.

Rais Assad pia amekaribisha kwa mikono miwili wazo la Russia kujenga airforce base kubwa katika bandari ya Latakia.

Juzi hapa Uturuki imelalamika ndege za kijeshi za Urusi kutoka Syria zenye teknolojia ya hali ya juu mno zimeingia mara tatu katika anga yake kwa siku tofauti na kwa makusudi.Rais Edorgan ameiomba NATO kuingilia kati!

Siku mbili hizi tunashuhudia surface to air missiles za kisasa na mpya toka meli za kivita za Russia zikitumika ndani ya Syria.



Leo hii tunazungumzia deployment ya askari wa ngazi ya juu wa Urusi.Yaani matayarisho haya ni ya hali ya juu mno kijeshi,kutoka ardhini,angani na baharini,mbinu za kijeshi ambazo hutumika tu kujihami kwa kuzuia au kutengeneza shambulizi kubwa sana la kijeshi.je,hii ni vita dhidi ya Isis only?!

Nimemsikia waziri wa ulinzi wa Marekani Ashton Carter akiionya Urusi kuwa itajutia uamuzi wake wa kuingia Syria.

Katika maneno yake amesema si lazima NATO kuingia Uturuki kuilinda dhidi ya uchokozi wa Russia bali wanaweza kufanya jambo kuonyesha kuwa wanao uwezo wa kuidhibiti Urusi.

Akaendelea kusema Urusi isifikirie kupata upinzani wa kijeshi moja kwa moja kuwa tatizo kwake,bali vita ya Jihadi inayoandaliwa na Saudia dhidi ya Iran na Urusi inaweza kuwa tatizo kubwa kwake.Je,Saudia na U.S wanamuandalia mrusi "chaka" kama lile la Afghanistan enzi zile?Akasema kama 1% ya 1 billion muslims ikiitikia call ya Saudia kupigana Jihad,Russia inao uwezo wa kudhibiti watu hao?

Kwa maneno haya na kwa kuzingatia uhusiano wa U.S, Saudia na hawa jihadist,mrusi awe makini sana.Vita ya kigaidi tumeishuhudia isivyokuwa na mwisho na kama Mrusi atatengenezewa jihadists na kupigana nao vita isiyokuwa na macho(anywhere,anytime) na isiyokwisha kama ya Iraq na Afghanistan,atakuwa amesave american interest bila kupenda.Can Russia contain this threat?

Kweli mkuu yasijekujirudia ya 80's.
 
Naona Spetsnaz hawajasaidia vita hii kuisha mapema.
Isil wamelipua ndege ya kirusi kule Egypt,wameua watu Ufaransa.
Wachina wametekwa hotelini Mali.
Ndege ya Urusi imedunguliwa na Uturuki.Ugaidi unapamba moto.
Waasi wameuzingira Damascus na Assad ana wakati mgumu zaidi pamoja na support ya Urusi.

Je,Russia ilikurupuka kulianzisha dubwana hili bila kuona hii escalation?
Ataweza kucontain hii hali?For how long?

Watu walishamwambia hawatapigana nae directly ila atashangaa tu vita haiishi!

Wamarekani,Saudia na jihadists wao ni kirusi kibaya.Ujue mikia yake yote kabla ya kupambana na pweza huyu or else one day utaichoka vita na kurudi kwenu mwenyewe bila kufukuzwa.
 
Back
Top Bottom