Russia iko dunia ya pili ndugu yangu, wanaperform kwenye viwanda vya silaha pekee lakini huwezi kulinganisha ujerumani na russia. Wajerumani wana reserve ya gas ya miaka 15 ijayo na hata sasa baada ya kuona nyodo za russia wanaplan kununua gas marekani. Kitu wanachoona wanapoteza ni soko la viwanda vya magari na technologia mpya ambazo wanaziuza sana ktk soko la urusi.
Mkuu Kibona, Ujerumani kununua gesi USA bado ni ghari sana, gesi ya USA itakuwa ghari endapo wataamua kununua huko, Na Russia hana haja ya kuwauzia hao wajerumani kwa sababu sasa anafanya biashara na Wachina.
Na Pigo kubwa kabisa ambalo Ulaya hawatalisahu ni la Russia kusagn Mkataba na China wa Gesi ya Biliono 400 USD na juzi kati imeongezeka,
Na kwa sasa hata kampuni za Nishati za Urusi wana ingia mkataba na za Kichina, hivyo Vikwazo vya Kiuchumi kwa namna nyingine ni msiba kwa Ulaya, Na Ulaya wanamtegemea Urusi kuliko Urusi anavyo wategemea wao. Ujerumani unajua ana export % ngapi Russia?
Na kuhusu kwamba Russia anategemea Gesi pekee yake si kweli kabisa, kwa sababu yuko vizuri maeneo mengine na anauza consumer goods kibao na juzi kati ameanza kupata tenda za ndege zake mpya za sukhoi supper jet.
Na Ulaya kwa sasa inapoteza soko lake Urusi na hata wakulima wa Ulaya wameisha ambiwa hata kama mgogoro utaisha ni vigumu kupata soko tena, hili ni pigo kwao na hawawezi uza USA, na USA ni mjanja sana yeye anawaingiza kingi Ulaya halafu anakaa pembeni. Poland kwa sasa matunda yanaoza na hakuna pa kuyauza na alie wapampu kakaa kimya.
Na that is why Ulaya hakuna nchi tena iliyo tiyari kuweka viukwazo kwa sababu wamegundua vina waumiza na wao vile vile, na Russia alikuwa na uwezo wa kuweka vikwazo vya Magari kitu ambachi kingekuwa ni pigo kubwa sana hasa kwa France