Yericko Nyerere
JF-Expert Member
- Dec 22, 2010
- 17,026
- 20,513
Rais Vladimir Putin wa Russia leo ameidhinisha ombi la eneo la Crimea kujitenga na Ukraine na kuwa sehemu ya Russia huku akizituhumu nchi za Magharibi kuwa zina unafiki mkubwa katika sera za kimataifa.
Katika hotuba yake iliyojaa hisia za utaifa alioitoa katika kikao cha pamoja cha mabunge mawili ya Russia mjini Moscow katika eneo la Kremlin, Putin amezikosia vikali nchi za Magharibi na kusema zina unafiki mkubwa kwani ziliidhinisha Kosovo kujitenga na Serbia lakini sasa zinataka kuwanyima watu wa Crimea haki sawa na hiyo. Huku akishangiliwa na hadhirina, Putin amesema, 'leo hauwezi ukakitaja kitu ni cheusi na kesho ukasisitiza kuwa ni cheupe.' Rais wa Russia amesema nchi za Magharibi zimevuka 'mstari mwekundu' kuhusu Ukraine. Amesema viongozi wapya waliokuja madarakani Ukraine, baada ya kupinduliwa muitifaki wa Russia, ni wanazi mambo leo wenye chuki kubwa dhidi ya Russia. Putin ameelezea wasiwasi wake kuhusu muungano wa kijeshi wa NATO unaoongozwa na Marekani kuenea hadi mipaka ya Russia. Punde baada ya hotuba yake, Rais Putin amepuuza vitisho vya vikwazo vya nchi za Magharibi na kutia saini mkataba wa kuifanya Crimea kuwa sehemu ya Shirikisho la Russia. Weledi wa mambo wanasema kadhia ya Crimea imeandaa uwanja wa kuzuka vita visivyo vya moja kwa moja kati ya kambi ya Wamagharibi inayoongozwa na Marekani kwa upande mmoja , na Russia kwa upande wa pili.