Putin aunga Sisi ''kuwania urais Misri''

Putin aunga Sisi ''kuwania urais Misri''

engmtolera

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2010
Posts
5,149
Reaction score
1,441
Putin

""nakutakia kheri na ufanisi katika juhudi zako kwa niaba yangu binafsi na wananchi wa Urusi ''

Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema anaunga mkono amiri mkuu wa majeshi ya Misri Abdul Fattah al-Sisi Kuwania urais wa taifa hilo.

Putin alimweleza Al-Sisi kuwa alifahamu kuhusiana na niya yake ya kuwania urais.

Hata hivyo hakujakuwa na dhibitisho lolote kutoka kwa ujumbe wa serikali ya Misri.

Kiongozi huyo wa jeshi la Misri ndiye aliyeongoza mapinduzi yaliyomng'oa mamlakani aliyekuwa rais wa Misri Mohammed Morsi mwezi julai mwaka uliopita.

Katiba mpya ya taifa hilo inashurutisha kufanyika kwa uchaguzi ifikiapo katikati ya mwezi Aprili mwaka huu.

Kheri Njema
Mwandishi wa BBC anasema iwapo uchaguzi wa urais utafanyika sasa kiongozi huyo wa jeshi anapigiwa upatu kushinda kwa sababu ya umaarufu wake .

Aidha hakujajitokeza mpinzani mwenye ushawishi mkubwa .

Field Marshal Sisi yuko mjini Moscow kujadili mkataba wa silaha wenye thamani ya dola bilioni 2 .

Mkataba huo unawadia baada ya serikali ya Marekani kusitisha makubaliano ya Mauzo ya silaha na Misri baada ya kungolewa madarakani kwa aliyekuwa rais Mohammed Morsi mwezi julai mwaka uliopita.

Chanzo:
Putin aunga Sisi ''kuwania urais Misri'' - BBC Swahili - Habari
 
Naona Egpyt inarudisha uhusiano wake na russia kabla ya Saadat

Russia inaweza kuikinga na kichapo kama alichopata libya,mfano mzuri syria
 
Naona Egpyt inarudisha uhusiano wake na russia kabla ya Saadat

Russia inaweza kuikinga na kichapo kama alichopata libya,mfano mzuri syria

Mmarekani nae anaihitaji misri hapo sasa patakuwa patamu kama Syria vile inavyogombaniwa sasa
 
Mmarekani nae anaihitaji misri hapo sasa patakuwa patamu kama Syria vile inavyogombaniwa sasa

The world is becoming a dangerous place

Muda si mrefu tutaona nuclear confrontation hata kwa a limited scale

Kuna flashpoints tatu potential kwa an all out war involving the US, ya kwanza ni China-japan ,ya pili North korea-South korea na mwisho ni Syrian/Russian vs Nato
 
Mmarekani alikua anawapa wamisri silaha kama ndege za kivita F-15 ambazo wameziprogram zisiweze kupambana na zile F-15 anazowapa waisrael.
Alikua anahakikisha misri hana strategy weapons zinazoweza kuwa tishio kwa israel kama airdefence systems,missile etc.
Marekani walitaka waitumie muslim brotherhood ili kuidhoofisha mashariki ya kati yote,na ndo chanzo cha arab spring.
Wamisri wakashituliwa na saud kuhusu mpango mzima,ndo kisa cha wanajeshi wa misri kumfanyia visa morsi na hatimae kumpindua.,kitendo kilichoiudhi marekani na kutishia kusimamisha misaada.saudia na qatar wakasema watafidia wao ,na wakatoa karibu dola bilion nane kwa mpigo kuziba pengo.
Hata hizo bilion 2 dollar za kununua silaha wamepewa na saud.
 
Hii ya China-Japan naona ndio mbaya zaidi,kwani haiwezi pita siku bila vyombo vya habari vya Uchina kutaja jina la Abe iwe kwa mazuri ama mabaya,hadi kunakipindi unaona kabisa kuwa hawa jamaa wanataka labda kulipiza kisasi juu ya vita ya dunia.
lakini pia hawa wakorea angarau kidogo kunakipindi unawaona wanakuwa na huruma kwa wenyewe kwa wenyewe,labda la syria hili bado ngoma ni nzito
 
Mmarekani alikua anawapa wamisri silaha kama ndege za kivita F-15 ambazo wameziprogram zisiweze kupambana na zile F-15 anazowapa waisrael.
Alikua anahakikisha misri hana strategy weapons zinazoweza kuwa tishio kwa israel kama airdefence systems,missile etc.
Marekani walitaka waitumie muslim brotherhood ili kuidhoofisha mashariki ya kati yote,na ndo chanzo cha arab spring.
Wamisri wakashituliwa na saud kuhusu mpango mzima,ndo kisa cha wanajeshi wa misri kumfanyia visa morsi na hatimae kumpindua.,kitendo kilichoiudhi marekani na kutishia kusimamisha misaada.saudia na qatar wakasema watafidia wao ,na wakatoa karibu dola bilion nane kwa mpigo kuziba pengo.
Hata hizo bilion 2 dollar za kununua silaha wamepewa na saud.

kumbe ndio maana SIS kakimbilia urusi,kwani nadhani ndiko kutamfanya urais wake uendelee kudumu kama atapata nafasi hiyo.
 
Back
Top Bottom