Marekani hawahitaji ushahidi, nafikiri maamuzi ya kuishambulia Syria yamefasha fanywa muda mrefu. Walikuwa wanatafuta sababu tu hata ya uongo watimize lengo hilo. Haiingii akilini ati Syria watumie silaha za kemikali wakati wakaguzi wa umoja wa mataifa wanawasili nchini humo kuchunguza kitu hicho hicho! Bunge la Uingereza limeliona hilo na ukimsikiliza Cameroon nafikiri ni kama anashukuru wamemkatalia. Tusubiri Congress wataamuaje, lakini ninaona ni kama inatafutwa uungwaji mkono kwa sababu wnanchi wa Marekani hawaungi mkono kujiingiza katiika vita vya Syria.View attachment 110050
Naona mambo yanazidi kuwa magumu kwa USA kwani Bunge la UK lilipinga kupitisha hoja ya kuishambulia Syria na leo hii yena Urusi inakuja na Hoja nyingine.
Rais Vladimir Putin wa Urusi anasema tuhuma kuwa serikali ya Syria ilitumia silaha za kemikali ni upuuzi mtupu.
Anasema jeshi la Syria lilikuwa linasonga mbele, hapakuwa na sababu ya serikali kuwapa kisingizio wale wanaotaka kuingia kijeshi.
Bwana Putin alisema ikiwa Marekani ina ushahidi kuthibitisha tuhuma zake, basi ikabidhi ushahidi huo kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Alimkumbusha Rais Obama kuwa aliwahi kutunzwa tuzo ya amani ya Nobel, na alimsihi kuwakumbuka wanyonge katika mashambulio.
Alikaribisha uamuzi wa bunge la Uingereza ambalo halikuunga mkono Uingereza kuingilia kati Syria, na anasema ameshangazwa na uamuzi huo wa bunge.
Putin ataka Marekani ioneshe ushahidi ~ dj sek
Inatakiwa mtu fulani anayewahurumia Watoto na wanawake na wananchi wa Syria kwa ujumla wanaouwawa kila kukicha na majeshi ya Dikteta Assad! Mtu huyo hawezi kuwa Putin!
Ni bora mtu kama Assad akaamua kuacha madaraka na hata kwenda Urusi kula maraha kuliko yeye kuwa sababu ya maelfu ya Wasiria wenzake kufa kinyama. Kitendo cha kuwapulizia madawa ya mauaji kama viroboto fulani ni unyama uliokithiri. Marafiki zake wangetakiwa kumshauri hivyo!Ingekuwa vyema kama US ingeacha kuwapa silaha waasi, kwa hakika hao wakina mama na watoto wasingekufa!
Mkuu wote tunapingana na unyama ule juu ya wale raia hapo kwenye RED napingana na wewe kwani si vema kuiingiza serikali moja kwa moja katika tukio lile kwani kuna pande mbili zinapigana hapo tutasema ni serikali ya Assaad imehusika ni pale kama miongoni mwa waliokufa kwa sumu ile wapo na askari wa waasi laikini kama hakuna kuna uwezekano mkubwa tukio hilo likafanywa na waasi kwa agizo kutoka Marekani ili wapate sababu ya kuingia katika vita hivyo kumtoa Al-assaad kwani kwa kiherehere walichonacho wamarekani sasa kuhusu kuishambulia Serikali ya Assad inaweza kujidhihirisha . Uchunguzi na majibu sahihi ni muhimu ili kuondoa lawama kama walizopata wamarekani kule Iraq kwa kuipiga Iraq kuwa ina siraha za sumu kitu ambacho hakikuwepo.Putin hana tofauti na Bashir Al-Assad, wote ni DICTATORS tu. Madai ya USHAIDI NI UPUUZI MTUPU!Je,anataka kuaiambia Dunia kuwa wale watu 1400 waliokufa na sumu siyo ushahidi tosha?JE,ANATAKA MAREKANI WAMPELEKEE ZILE MAITI ZA WATU WALOUAWA KWA SUMU?Putin ni mnafiki mkubwa na hana hoja. Putin sanasana anachoongalia hapo ni MAFUTA ya SYRIA tu na haoni MAELFU YA WATU WALIOUAWA KWA SUMU! HAINGII AKILINI HATA KIDOGO KUMTETEA DIKTETA ANAYEUA RAIA WA NCHI YAKE KWA SILAHA ZA SUMU! Hili halikubaliki hata kidogo. Al-Bashir lazima apigwe na ang'olewe madarakani kama ilivofanyika kwa Dictators wengine kama akina Saadam Hussein na Muamar Ghadafy.
Mtu yeyote awe Rais au Raia kama anatumia silaha za maangamizi zenye sumu lazima asimamishwe au aondolewe mara moja kwenye jamii ya Wana wa ADAMU. Huyo ni mtu hatari ambaye anaweza kuangamiza hata Dunia nzima!
NAUNGANA NA MAREKANI NA UFARANSA KWA UAMUZI WA KUMTANDIKA AL-ASSAD!NI UMAUZI SAHIHI NA LAZIMA UUNGWE MKONO NA WAPENDA HAKI NA AMANI POPOTE DUNIANI!
Russia hana lolote mbele ya USA, Marekani itaipiga Syria na Assad ataondoka madarakani.Katika vita nyingi zilizo piganwa hapa duniani silaha za Russia hazina record ya kufanya vizuri katika uwanja wa mapambano.Puttin ataaibika.Putin hana tofauti na Bashir Al-Assad, wote ni DICTATORS tu. Madai ya USHAIDI NI UPUUZI MTUPU!Je,anataka kuaiambia Dunia kuwa wale watu 1400 waliokufa na sumu siyo ushahidi tosha?JE,ANATAKA MAREKANI WAMPELEKEE ZILE MAITI ZA WATU WALOUAWA KWA SUMU?Putin ni mnafiki mkubwa na hana hoja. Putin sanasana anachoongalia hapo ni MAFUTA ya SYRIA tu na haoni MAELFU YA WATU WALIOUAWA KWA SUMU! HAINGII AKILINI HATA KIDOGO KUMTETEA DIKTETA ANAYEUA RAIA WA NCHI YAKE KWA SILAHA ZA SUMU! Hili halikubaliki hata kidogo. Al-Bashir lazima apigwe na ang'olewe madarakani kama ilivofanyika kwa Dictators wengine kama akina Saadam Hussein na Muamar Ghadafy.
Mtu yeyote awe Rais au Raia kama anatumia silaha za maangamizi zenye sumu lazima asimamishwe au aondolewe mara moja kwenye jamii ya Wana wa ADAMU. Huyo ni mtu hatari ambaye anaweza kuangamiza hata Dunia nzima!
NAUNGANA NA MAREKANI NA UFARANSA KWA UAMUZI WA KUMTANDIKA AL-ASSAD!NI UMAUZI SAHIHI NA LAZIMA UUNGWE MKONO NA WAPENDA HAKI NA AMANI POPOTE DUNIANI!