Putin anaionya ECOWAS kama nani? "AU" kemeeni huu upuuzi. Afrika sio Crimea

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,115
49,840
Hii ni dharau na matusi Kwa Waafrica, African Union Kemeeni huu upuuzi wa Putin,Afrika Sio koloni Wala Jimbo la Russia.
---

Urusi imeionya Jumuiya ya kiuchumi ya Afrika Magharibi Ecowas kuhusu kuchukua hatua za kijeshi ambazoinasema itachukua dhidi ya wanajeshi waliofanya mapinduzi nchini Niger.

Inasema kuwa uamuzi huo unaweza kusababisha mgogoro ambao hautaonekanakwa muda mrefu.

Katika taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Russiasiku ya Ijumaa, ilizionya nchi za Afrika Magharibi kutopeleka wanajeshi Niger.

Taarifa hiyo ilisema, "Tunaamini kwamba hatua hiyo ya kijeshihaitatatua tatizo la Niger, badala yake hali hiyo itasababisha mzozo mkubwa,ambao tarehe yake haijulikani, na hali katika eneo la Sahel itakuwa ngumutena".

Wakuu wa usalama wa Ecowas wanapanga mkutano siku ya Jumamosi kupangajinsi ya kuandaa jeshi.

Siku ya Ijumaa, kundi la Ecowas lilikubali kuanzisha 'kikosi cha kudumu'katika maandalizi ya kuchukua hatua za kijeshi dhidi ya jeshi la Niger.

Tayari, rais wa Ivory Coast, Alassane Ouattara, alisema kuwa nchi yakeitatuma takriban wanajeshi 1,000 ambao watajiunga na safu ya vikosi vingine vyakijeshi ambavyo vitakuwa kwenye mpango wa kutumwa Niger.

Marekani, Ufaransa na Umoja wa Ulaya tayari zimeunga mkono uamuziuliochukuliwa na kundi la Ecowas kumrejesha madarakani rais mteule MohamedBazoum.

BBC
 
Back
Top Bottom