Putin achimba biti kwamba Leopard 2 na Abraham haziwezi kubadili kitu Ukraine

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Oct 26, 2018
21,713
35,525
3 Februari 2023, 06:08 EAT
Vladimir Putin amelinganisha uvamizi wa Urusi nchini Ukraine na mapambano dhidi ya Ujerumani ya Wanazi, katika hotuba yake ya kuadhimisha miaka 80 ya kumalizika kwa Vita vya Stalingrad.

Akitoa mfano wa uamuzi wa Ujerumani kupeleka vifaru Ukraine, rais wa Urusi alisema historia inajirudia.
"Haiaminiki lakini ni kweli," alisema. "Tunatishiwa tena na mizinga ya Leopard 2 ya Ujerumani."

Ujerumani ni mojawapo ya nchi nyingi zinazoisaidia Ukraine kutetea eneo lake.

Urusi ilianzisha uvamizi wake wa umwagaji damu,karibu mwaka mmoja uliopita, na kusababisha nchi za Magharibi kutuma silaha na misaada kwa serikali huko Kyiv.

Akizungumza mjini Volgograd - jina la kisasa la Stalingrad - Bw Putin alidokeza kwamba anaweza kuamua kutumia zaidi kuliko silaha za kawaida.

"Wale wanaotarajia kuishinda Urusi kwenye uwanja wa vita hawaelewi, inaonekana, kwamba vita vya kisasa na Urusi vitakuwa tofauti sana kwao," kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 70 alisema. "Hatutumi vifaru vyetu kwenye mipaka yao, lakini tuna njia ya kujibu. Haitaishia tu kutumia vifaa vya kivita. Kila mtu lazima aelewe hili."

Msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov alikataa kufafanua maoni ya Bw Putin lakini aliwaambia waandishi wa habari kwamba "silaha mpya zinapotolewa na mataifa ya Magharibi, Urusi itatumia zaidi uwezo wake kujibu".

Bw Putin alikuwa Volgograd kuadhimisha kumbukumbu ya mwisho wa Vita vya Pili vya Dunia vya Stalingrad, ambavyo vilishuhudia jeshi la Sovieti likiwakamata karibu wanajeshi 91,000 wa Ujerumani katika mabadiliko makubwa ya vita.
Zaidi ya watu milioni moja waliangamia katika vita hivyo - vita vya umwagaji damu zaidi.
Volgograd ilibadilishwa jina kwa muda kuwa Stalingrad kwa siku ya kuadhimisha kumbukumbu hiyo, na mapema wiki hii mnara mpya wa kiongozi wa zamani wa Soviet Joseph Stalin lilizinduliwa.
Stalin - ambaye aliongoza Umoja wa Kisovyeti kati ya 1924 na kifo chake mwaka 1953 - alishtakiwa kwa kupanga njaa nchini Ukraine kati ya 1932-33.

Tukio hilo - lililoitwa Holodomor na Waukraine - liliua takriban watu milioni tano na lilitambuliwa kama mauaji ya halaiki mapema wiki hii nchini Bulgaria.
Katika muda wote wa vita nchini Ukraine, Bw Putin amejaribu kwa uwongo kuwasilisha uvamizi wa Urusi kama vita dhidi ya wazalendo na Wanazi - ambao anasema wanaongoza serikali ya Kyiv.
Na akarejelea mada hiyo katika hotuba yake yote.
"Sasa, kwa bahati mbaya, tunaona kwamba itikadi ya Unazi, tayari katika sura yake ya kisasa, katika udhihirisho wake wa kisasa, tena inaleta vitisho vya moja kwa moja kwa usalama wa nchi yetu," alisema.
"Tena na tena inabidi tuondoe uchokozi wa nchi za Magharibi.

Lakini aliapa kwamba ingawa ilikuwa "isiyoaminika lakini ni kweli" kwamba Urusi ilikuwa ikitishiwa tena na vifaru vya Ujerumani, Moscow ilikuwa na jibu kwa nchi yoyote ambayo iliitishia.

Berlin imekubali kutuma mizinga 14 ya Leopard 2 kwa Ukraine, na kusababisha kampuni ya Urusi ya Fores - kampuni ya sekta ya nishati ya Urals - kutoa rubles milioni tano (£ 58,250) kwa askari wa kwanza wa Kirusi kuharibu au kukamata moja.

Bw Putin pia aliweka maua kwenye kaburi la mwanajeshi wa Usovieti ambaye alisimamia ulinzi wa jiji hilo, na alitembelea jumba kuu la kumbukumbu ambapo aliongoza muda wa kimya kwa wale waliokufa katika vita.
Wakati huo huo, maelfu ya wakazi wa Volgograd walijipanga kwenye barabara za jiji hilo kutazama gwaride la kijeshi.

th

CHANZO CHA PICHA,REUTERS
Wakati ndege zikiunguruma,
vifaru vya kisasa na vya zama za Vita vya Pili vya Dunia vilibingiria katikati mwa jiji. Baadhi ya magari ya kisasa yaliwekwa alama ya Z, ambayo imekuwa ishara ya uvamizi wa Urusi.

Vyombo vya habari vya ndani viliripoti kwamba Gavana wa mkoa Andrey Bocharov - ambaye aliandamana na Bw Putin kwenye jumba la kumbukumbu - hakuwepo kwenye gwaride. Hakuwa ameonekana tangu Januari 24, na kusababisha uvumi kwamba alikuwa akijitenga kabla ya kukutana na rais.

Kwingineko, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alisema Urusi inajiandaa kulipiza kisasi dhidi ya nchi za Magharibi kwa kuisaidia Ukraine.

"Sasa Urusi inaelekeza nguvu zake. Sote tunajua hilo. Inajiandaa kujaribu kulipiza kisasi, sio tu dhidi ya Ukraine, lakini dhidi ya Ulaya huru na ulimwengu huru," Bw Zelensky alisema huko Kyiv.

Akizungumza pamoja na Rais wa Tume ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen, Bw Zelensky alisema Urusi "inaongeza kasi ya kukabiliana na vikwazo" na kumtaka kiongozi huyo wa Umoja wa Ulaya kuweka vikwazo zaidi kwa uchumi wa Urusi.
 
Back
Top Bottom