kimsboy
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 8,991
- 17,888
Putin aahidi jibu 'kali' kwa ugaidi wa Ukraine
Oct 11, 2022 02:27 UTC
[https://media]
Iwapo Ukraine itapanga mashambulizi zaidi ya kigaidi dhidi ya Russia, kutakuwa na jibu kubwa la kijeshi sawa na lile lililotekelezwa Jumatatu.
Onyo hilo limetolewa na Rais wa Vladimir Putin wa Russia ambaye amethibitisha kwamba jeshi la nchi yake limefanya mashambulizi makubwa Jumatatu dhidi ya Ukraine kwa kutumia silaha za masafa marefu ambazo zimelenga vituo vya nishati na mawasiliano ya kijeshi vya Ukraine.
Shambulio hilo lilitokea siku mbili baada ya bomu kuharibu daraja la kimkakati la Crimea, ambalo Moscow imeliita shambulizi la kigaidi la Ukraine.
Rais Putin ameendelea kusema kuwa: "Iwapo kutakuwa na majaribio zaidi ya kufanya mashambulizi ya kigaidi katika ardhi yetu, Russia itajibu vikali na kwa kiwango kinacholingana na vitisho vilivyoibuliwa dhidi ya yake."
Kulingana na Waziri Mkuu wa Ukraine Denis Shmygal, Mapema Jumatatu, mikoa kadhaa ya Ukraine ilikumbwa na mashambulizi ya makombora, na miundombinu muhimu isiyopungua 11 iliharibiwa.
Rais Putin alisema kuwa Russia mashambulizi hayo ya kulipiza kisasi yamekuja baada ya majaribio kadhaa ya kuharibu miundombinu ya Russia ambayo yamehusishwa na Ukriane.
Rais Putin amessema miongoni mwa mambo mengine, Ukraine iliharibu sehemu ya mfumo wa kusambaza umeme wa kinu cha nyuklia cha Kursk na ilijaribu kuharibu bomba la gesi asilia la TurkStream linalosafirisha gesi asilia kutoka Russia hadi Uturuki. Aidha na Rais wa Russia amebaini kuwa Ukarine imehusishwa na mlipuko wa Jumamosi ulioharibu Daraja la Crimea.
[https://media]Hujuma ya kigaidi dhidi ya Daraja la Crimea
"Utawala wa Kiev umekuwa ukitumia mbinu za kigaidi kwa muda mrefu sana," rais wa Russia ameendelea kusema na kutaja mauaji ya watu mashuhuri, mashambulizi ya kiholela ya miji ya Donbass na Kiwanda cha Nyuklia cha Zaporozhye kuwa mifano ya vitendo kama hivyo.
"Kwa kweli, serikali ya Kiev imejiweka sawa na vikundi vya kigaidi vya kimataifa. Kuacha uhalifu kama huo bila jibu imekuwa haiwezekani," alisisitiza, kabla ya kuthibitisha kwamba Russia ilishambulia miundombinu ya Ukraine.
Mbali na kuilaumu Ukraine kwa mfululizo wa mashambulizi dhidi ya miundombinu ya Russia, Putin ameashiria kuvurugwa mabomba ya kusafirisha gesi ya Nord Stream. Alisema kuwa Russia inazuiwa na mataifa ya Ulaya kuchunguza hujuma hiyo na akasisitiza kuwa "sote tunamfahamu vyema mnufaika mkuu wa uhalifu huo."
Putin aliyasema hayo alipokuwa akiongoza kikao cha Baraza la Usalama la Taifa la Russia.
Mlipuko wa Jumamosi kwenye daraja la Crimea, kiungo muhimu kati ya peninsula hiyo Russia bara, uliua raia kadhaa na kuangusha sehemu ya daraja linalotumiwa na magari. Aleksandr Bastrykin, mkuu wa Kamati ya Uchunguzi ya Russia, aliripoti kwa Putin siku ya Jumapili kwamba Ukraine ndiyo iliyohusika na uhalifu huo, huku kiongozi huyo wa Russia akibaini kwamba "hakuna shaka" kuhusu hilo.