Punguza unywaji wa pombe, ukiweza acha kabisa

kuna jamaa yetu alikuwa na kauli kama hizi yeye mwenyewe akidai "anakunywa kistaarabu". sasa bwana uku na uku ikafika mahali mwili ukaumuka kama yule

Wengine wana matatzo yao pia na aina ya pombe.

Halafu kunywa kiasi na kunywa kistaarabu ninmambo mawili twafauti. Inawezekana alikua akinywa anakunywa nyingi mno lakini bado anakua mstaarabu ila kazidisha kiasi.

All in all sisi tunaokunywa tunatambua pombe ina madhara na kama hunywi usijaribu baki na juice ya embe.
 
Kama Mimi vile kwenye jokofu Kuna bia za kuzidi naziangalia tu!
Ila siku nikichafukwa nalewa
Dah,

Jana usiku nilikuwa najibu huu uzi. Nikalala nikaota nimesafiri nipo katika bonge la hoteli, nimekaa peke yangu, mara akaja dada mmoja very smart akanichangamkia akanipa chupa ya wine, nikawa namwambia mimi sinywi.

Yani majaribu mpaka kwenye ndoto.
 
Dah,

Jana usiku nilikuwa najibu huu uzi. Nikalala nikaota nimesafiri nipo katika bonge la hoteli, nimekaa peke yangu, mara akaja dada mmoja very smart akanichangamkia akanipa chupa ya wine, nikawa namwambia mimi sinywi.

Yani majaribu mpaka kwenye ndoto.
Tumeshaathirika kisaikolojia ya pombe
 
Ahsante kwa ushauri wako ila unaujua utamu wa pombe au unausikia tu kwenye bomba?

Ushawahi kunywa safari ya baridi kwenye jua kali?

Ulishawahi kunywa jack Daniel au John walker mizinga ya kiume ukiwa na washikaji zako wa faida?

Acha grants za kike ambazo huwa sipendelei bablai,
Je,ushawahi kunywa pombe za kifaransa mixer mizinga ya kijerumani,au umeacha kuhubiri kanisani unaamua kuja upande wetu?

Wee huu upande unajitambua sana wewe endelea kuchunga kondoo wako tuache

I love Jack Daniel Spirit original
We jamaa unaishi kwenye madhabahu ya pombe...hahah!
 
TAMBUA UNYWAJI SAHIHI WA POMBE

Kitu cha msingi kwenye pombe siyo kujua aina ya beer au kilevi. Kitu cha msingi ni kujua percentage of pure alcohol (asilimia ya pombe halisi) na ujazo wake ( volume).

Unit moja ya pombe ni sawa na 10mls of pure alcohol or 8g of the same. Mwanaume hutakiwa kunywa unit 3 za pure alcohol na mwanamke 2 kwa siku( standard units)

Mfano , let say una kinywaji cha pombe(mzinga) umeandikwa 40 percent na ujazo labda 500mls. Hiyo asilimia 40 ni pure alcohol ya ujazo . Ukizidisha mara 500mls unapata 200mls za pure alcohol. So kwenye mls 500 only 200mls are pure alcohol
Kama unit moja ya pure alcohol Ina 10mls za pure alcohol , katika 200mls tulizopata zitakuwa na unit 20 za pure alcohol ( chukua 200mls gawanya kwa 10mls).

Je ,kiasi gani unywe kwa mzinga huo ?

Ni rahisi sana ! Ikiwa unit 20 za pure alcohol zina ujazo wa mls 500 , je unit 3 kwa mwanaume ujazo utakuwaje ?
Jibu 500mls zidisha mara 3 gawanya kwa 20. (75mls )
So utakunywa mls 75 tu kwenye mzinga huo sawa na vifuniko 3 vya mls 25 vya kwenye chupa ya dawa za syrup.

Kumbuka! Pombe huzuia uchomaji wa chakula cha wanga na mafuta kwa zaidi ya saa 72 na kupelekea ongezeko la Uzito, vitambi ,ini kujaa mafuta ( alcoholic fatty liver diseases ) na insulin kinzani ( insulin resistance) , hivyo kuwa katika hatari ya kisukari na shinikizo kubwa la damu.

Ukiweza usinywe pombe kutokana na kusisimua ubongo kwenye eneo la madawa ya kulevya ( mu opioid receptor ) hivyo kusababisha utegemezi ( dependency)

Jinsi pombe inavyoathiri mwili wako

1. Ubongo wako: Pombe hata kiwango kidogo, husababisha madhara yasiyorekebishika kwenye seli za ubongo;baadhi hufa na zingine hubadilika.

2: Moyo wako: Pombe huongeza hatari ya shinikizo la damu, kiharusi, na kudhurika kwa misuli ya moyo.

3: Mapafu yako: Pombe huhafifisha shughuli za upumuaji.

4: Mfumo wako wa uzazi: Kwa wanaume pombr inaweza kuharibu seli za testesi,zikisababisha upungufu wa nguvu za kiume,kushindwa kuzaa na huenda kuongezeka kwa matiti.Kwa wanawake pombe inaweza kusababisha mvurugiko wa mzunguko wa hedhi na ovari kushindwa kufanya kazi.Pombe pia imehusianishwa na kasoro za kuzaliwa kwa watoto na matatizo ya ubongo.

5: Ini lako:Kwa sababu ini lako lazima lichuje pombe kutoka kwenye damu,pombe huathiri ini kuliko kiungo chochote katika mwili wako.
~Kalori za ziada katika pombe huhifadhiwa kama mafuta kwenye ini.
~Seli za ini zinazofanya kazi hufa kutokana na sumu kwenye pombe.
~Tishu za makovu huchukua nafasi ya seli zilizokufa,zikisababisha kuharibika kwa ini.

6: Mfumo wako wa kinga: Pombe hudhoofisha kinga ya mwili dhidi ya maradhi.

7: Ongezeko la saratani:Koromeo,Umio,Ini,Matiti kwa wanawake,Tumbo,Kongosho,Utumbo mkubwa,Rektamu,Tezi dume,Yai,Mfuko wa uzazi na mfuko wa mkojo.

Kumbuka kinga ni bora kuliko tiba!!
Mwanao kagoma kabisa kuacha pombe,,,akaamua azitengeneze kabisa
images (2).jpeg
 
Kuna mambo mawili tu yanainusuru dunia kuwa sehemu tulivu....kiasi kwamba visinge kuwepo tungechinjana kama kuku navyo ni DINI na POMBE...
Ondoa dini ya alla,ile sio dini ya amani na kuleta watu karibu kwa umoja na utulivu
 
Natamani kuacha pombe ila napokumbuka bar ndiyo sehemu pekee ambayo hua napatiepo michongo ya pesa, moyo wangu unasita kabisa
 
Back
Top Bottom