Punguza unywaji wa pombe, ukiweza acha kabisa

Africa hatunywi pombe kama starehe watu wengi hawajui huu ukweli.

Hakuna starehe ya kunywa bia kreti moja mtu mmoja, mkae mkijuwa kuna Vitu watu vinawasumbuwa.

Hata Yule Gardner G Habash inasemekana pombe Kali ndio source ya ugonjwa wake.

Sasa jiulize mtu asiye na stress atamaliza Vipi chupa zima la scotch?

Labda ninachotaka kusema hapa kama ilivyo tatizo la vidonda vya tumbo sababu yake kuu ni kuishi dunia ya tatu, basi na issue ya pombe iko hivyohivyo.

Bongo sasa hivi ni 03:38 midnight lakini nasikia mziki kwenye pub ya Jirani watu wanakula maji tena asubuhi tunaamkia working day? Unadhani ni kweli hawa watu Wana furaha?

Wengine wakirudi nyumbani mapema ni kama Jehenamu wake zao Wana midomo kama chuchunge nyumbani hapakaliki.
Ni kweli, alcoholism kawaida inakuwa na underlying psychological problems.
 
1000051840.jpg
 
mnaotaka kutoka mtoke kimyakimya mtuchanganya tunaoingia aisee
Karibu chamani, ila wengine ni lazima watoke.

Kuna vichwa vyao panzi hawawezi pombe, kuna ambao wakinywa pombe wanageuka vichaa, kuna ambao wakinywa pombe familia iko tabuni, kuna wadada akinywa pombe ikamkolea basi anaweza kukojooewa na yeyote yule ambaye atakuwa interested naye, hawa wote wanatakiwa kuacha pombe haiwafahi.

Pombe siyo Kwa ajili ya kila mtu, wengine tumeanza kunywa Kwa kununuliwa na Washia zetu kwahiyo hazituzuru chochote zaidi ya kutukausha mifuko tu, lakini kuna ambao wametoka kwenye familia pombe hautakiwi hawa ndio tatizo wanalazimisha kunywa lakini hawatakiwi kunywa.
 
Pombe ni Hatari kwa afya yako usinywe

Mithali 23

29 Ni nani apigaye, Yowe? Ni nani aliaye, Ole? Ni nani mwenye ugomvi? Ni nani mwenye mguno? Ni nani aliye na jeraha zisizo na sababu? Ni nani aliye na macho mekundu?

30 Ni wale wakaao sana kwenye mvinyo; Waendao kutafuta divai iliyochanganyika.

31 Usiitazame mvinyo iwapo ni nyekundu; Iitiapo bilauri rangi yake, ishukapo taratibu;

32 Mwisho wake huuma kama nyoka; Huchoma kama fira.

33 Macho yako yataona mambo mageni; Na moyo wako utatoa yaliyopotoka.
Toranti 14:24-26

Katika Biblia, kuna mistari kadhaa ambayo inaonekana kuruhusu unywaji wa kileo kwa kiasi na katika muktadha fulani, huku ikisisitiza utumiaji wa busara na kuwa na kiasi. Hapa chini ni baadhi ya mistari hiyo:

1. Mithali 3:9-10 – "Mheshimu BWANA kwa mali yako, na kwa malimbuko ya mazao yako yote; ndipo ghala zako zitakapojaa tele, na mashinikizo yako yatafurika divai mpya."

2. Mhubiri 9:7 – "Enenda, ukale chakula chako kwa furaha, na ukanywe divai yako kwa moyo mwema; kwa sababu Mungu amekwisha kuyakubali matendo yako."

3. Zaburi 104:14-15 – "Huotesha majani kwa wanyama, na mimea kwa mahitaji ya wanadamu, ili kuleta chakula kutoka ardhini, na divai iwapendezao mioyo ya wanadamu, na mafuta kuyang'ariza nyuso zao, na mkate umpao mtu nguvu."

4. 1 Timotheo 5:23 – "Usiwe unakunywa maji tu, bali tumia kidogo divai kwa ajili ya tumbo lako na maradhi yako ya mara kwa mara."
 
TAMBUA UNYWAJI SAHIHI WA POMBE

Kitu cha msingi kwenye pombe siyo kujua aina ya beer au kilevi. Kitu cha msingi ni kujua percentage of pure alcohol (asilimia ya pombe halisi) na ujazo wake ( volume).

Unit moja ya pombe ni sawa na 10mls of pure alcohol or 8g of the same. Mwanaume hutakiwa kunywa unit 3 za pure alcohol na mwanamke 2 kwa siku( standard units)

Mfano , let say una kinywaji cha pombe(mzinga) umeandikwa 40 percent na ujazo labda 500mls. Hiyo asilimia 40 ni pure alcohol ya ujazo . Ukizidisha mara 500mls unapata 200mls za pure alcohol. So kwenye mls 500 only 200mls are pure alcohol
Kama unit moja ya pure alcohol Ina 10mls za pure alcohol , katika 200mls tulizopata zitakuwa na unit 20 za pure alcohol ( chukua 200mls gawanya kwa 10mls).

Je ,kiasi gani unywe kwa mzinga huo ?

Ni rahisi sana ! Ikiwa unit 20 za pure alcohol zina ujazo wa mls 500 , je unit 3 kwa mwanaume ujazo utakuwaje ?
Jibu 500mls zidisha mara 3 gawanya kwa 20. (75mls )
So utakunywa mls 75 tu kwenye mzinga huo sawa na vifuniko 3 vya mls 25 vya kwenye chupa ya dawa za syrup.

Kumbuka! Pombe huzuia uchomaji wa chakula cha wanga na mafuta kwa zaidi ya saa 72 na kupelekea ongezeko la Uzito, vitambi ,ini kujaa mafuta ( alcoholic fatty liver diseases ) na insulin kinzani ( insulin resistance) , hivyo kuwa katika hatari ya kisukari na shinikizo kubwa la damu.

Ukiweza usinywe pombe kutokana na kusisimua ubongo kwenye eneo la madawa ya kulevya ( mu opioid receptor ) hivyo kusababisha utegemezi ( dependency)

Jinsi pombe inavyoathiri mwili wako

1. Ubongo wako: Pombe hata kiwango kidogo, husababisha madhara yasiyorekebishika kwenye seli za ubongo;baadhi hufa na zingine hubadilika.

2: Moyo wako: Pombe huongeza hatari ya shinikizo la damu, kiharusi, na kudhurika kwa misuli ya moyo.

3: Mapafu yako: Pombe huhafifisha shughuli za upumuaji.

4: Mfumo wako wa uzazi: Kwa wanaume pombr inaweza kuharibu seli za testesi,zikisababisha upungufu wa nguvu za kiume,kushindwa kuzaa na huenda kuongezeka kwa matiti.Kwa wanawake pombe inaweza kusababisha mvurugiko wa mzunguko wa hedhi na ovari kushindwa kufanya kazi.Pombe pia imehusianishwa na kasoro za kuzaliwa kwa watoto na matatizo ya ubongo.

5: Ini lako:Kwa sababu ini lako lazima lichuje pombe kutoka kwenye damu,pombe huathiri ini kuliko kiungo chochote katika mwili wako.
~Kalori za ziada katika pombe huhifadhiwa kama mafuta kwenye ini.
~Seli za ini zinazofanya kazi hufa kutokana na sumu kwenye pombe.
~Tishu za makovu huchukua nafasi ya seli zilizokufa,zikisababisha kuharibika kwa ini.

6: Mfumo wako wa kinga: Pombe hudhoofisha kinga ya mwili dhidi ya maradhi.

7: Ongezeko la saratani:Koromeo,Umio,Ini,Matiti kwa wanawake,Tumbo,Kongosho,Utumbo mkubwa,Rektamu,Tezi dume,Yai,Mfuko wa uzazi na mfuko wa mkojo.

Kumbuka kinga ni bora kuliko tiba!!
Elimu imekaa
 
Mhubiri 9:7 – "Enenda, ukale chakula chako kwa furaha, na ukanywe divai yako kwa moyo mwema; kwa sababu Mungu amekwisha kuyakubali matendo yako."

Ujiulize je matendo yako yanakubaliwa na Mungu ama yanaleta machukizo.
 
Acha vichekesho vya chekechea
 
Mi nilikua mlevi wa Pepsi sahivi nimeacha kunywa soda nina mwezi mmoja nimeweza kujizuia lengo ni kutokurudia kabisa
 
Back
Top Bottom