Pugu: Rais Magufuli azindua ujenzi wa Reli, asema dereva mzuri hasikilizi maneno ya watu

Casuist

JF-Expert Member
Jul 23, 2014
1,189
2,970
Habari waungwana,

Leo Rais Magufuli anazindua reli ya kiwango inayofuata kiwango cha kimataifa(Inakadiriwa 55% ya reli yote duniani imetumia kipimo hiki na reli zote zenye mwendokasi mkali zinatumia kiwango hiki ukiacha Urusi, Uzbekistan na Finland).

Fuatana nami kujua kitachojiri kutoka Pugu.
========

Kwa sasa wanatambulishwa wageni mbalimbali na kabla alizungumza mkuu wa mkoa wa Dar, Paul Makonda.

Anayeongea kwa sasa ni mwenyekiti wa kamati ya wataalamu na anasema reli inatarajiwa kubeba tani milioni 17 kwa mwaka, sehemu ambayo ina milima mikali zitajengwa handaki(tunnels). Huko nyuma kulikuwa na mawazo ya kujenga SGR lakini watu walikuwa wakija na maono tofauti.

Anayezungumza sasa ni Mkurugenzi mtendaji shirika hodhi la reli(RAHCO), Masanja Kadogosa NA anasema niaka 112 iliyopita, utawala wa kijerumani ulijenga reli ya kati na ukawa ujenzi wa pili kwa ukubwa katika miradi ya kikoloni ya Kijerumani. Kiwango walichotumia ilikuwa ndio kiwango kilichotumiwa na nchi za ulaya baada ya kuanza kutumia reli. Reli ilifungua biashara kati ya ziwa Tanganyika na Pwani.

Wakandarasi 40 waliomba kandarasi na kampuni za Uturuki na Ureno zilikidhi na timu ya wataalamu walisafiri kuona sehemu ambayo wameshajenga. Watajenga jumla ya kilomita 300, stesheni 6 za abiria na 6 za kupishana treni.

Soma pia: Uzi mkuu unaoonesha yaliyojiri kwenye mradi wa SGR tangu kuanza kwake mpaka mradi ulipofikia hivi sasa

Uzio wa watu kupita juu kwa sababu treni itakuwa inaenda kasi sana na inatajiwa kugharimu dola milioni 185 baada ya kodi. Sehemu kubwa ya mradi huu

  • Kufanya usanifu wa kina Dar- Moro
  • Kubaini kina na kiwango cha maji katika mito ambayo reli inapita
  • Utafiti wa udongo
  • Sehemu ambazo zitaathirika reli itapopita
  • Kujenga yadi ya kkundiowa treni na kufanya matengenezo
  • Ujenzi wa mfumo wa umeme wa kuendeshea reli hii na utajengwa kwa ushirikiano na TANESCO
Masanja Kadogosa: Treni moja ni sawa na semi trela 500 hivyo itapunguza matumizi ya mafuta, itakuwa na uwezo wa kwenda Dodoma chini ya masaa matatu na nusu na Mwanza chini ya masaa 10. Itahitajika kuondoa watu wote waliovamia maeneo ya reli.

Miaka iliyopita uliahidi watanzania watasafiri kwa bajaji Mwanza hadi Mtwara, Dar-Dodoma chini ya masaa matatu na kiuchumi watu wataweka muda mwingi zaidi katika uzalishaji badala ya kusafiri, Tunaahidi kusimamia mradi kuisha katika muda uliopangwa na chini ya bajeti.

Anaeongea kwa sasa ni kutoka kampuni ya ukandarasi ya Uturuki na anaongelea urafiki wa Tanzania na Uturuki, anasema usafiri ni jambo la muhimu katika kuongezeka biashara. Anasema historia imeandikwa na wanashukuru kuwa sehemu yake, Treni hii ni muhimu kwa Tanzania na majirani zake, reli inafata viwango vya Marekani na ina ubora na mwendo.

Anamshukuru waziri wa uchukuzi, Mwenyekiti RAHCO na mchakato wote ambao anadai ulikuwa wazi(Transparent). Anasema sasa ni muda wa kuvaa Helment na kuanza ujenzi na anaelezea malighafi zitazotumika katika ujenzi wa reli hiyo, changamoto pekee ni ushirikiano wa kutosha na itachukua miezi 20 kutoa treni kutoka Dar kwenda Morogoro.

Anamkabidhi zawadi ya picha inayooshesha njia ya reli kwa Rais Magufuli.

Anaeongea kwa sasa ni waziri wa uchukuzi, Makame Mbarawa na anasema serikali imeamua kujenga reli yenye uwezo wa kujenga tani milioni 17 ikilinganishwa na ya sasa yenye uwezo wa kubeba tani milioni tano pekee.

Faida kubwa itapatikana kwenye bandari ya Dar es Salaam na pia watanzania 600,000 watapata kazi za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja na kinaaza kujengwa kipande cha kwanza hadi Morogoro. Tutamsimamia mkandarasi katika ujenzi na tunakupongeza mheshimiwa Rais kwa kufatilia kwa kidetete mchakato huu.

Sasa waziri anamkaribisha Rais Magufuli.
=========

Anaeongea kwa sasa ni Rais Magufuli.

Rais John Magufuli: Namshukuru sana mwenyezi Mungu alietujaalia tufike hapa, mheshimiwa waziri na wizara kwa kunikaribisha na wananchi wa Pugu kwa kunipa kura nyingi sana zilizoniwezesha kuwa Rais leo ikiwa mara yangu ya kwanza kuja hapa.

Tulipopita tukiomba kura, mambo mengi tuliahidi ikiwemo kuhakikisha tunaimarisha miundombinu ikiwa ni pamoja na reli ya kisasa, tuna reli ya kati ambayo sehemu kubwa ilijengwa na wakoloni(Wajerumani na waingereza na kutumia miaka 30).

Reli nyingine ni ya TAZARA ambayo ilijengwa kwa ufadhili wa China, reli hii ya leo tumehusika wenyewe kuanzia mchakato wake mpaka utoaji fedha. Itakuwa inabeba uzito mkubwa kuliko zote tulizozizoea na pia itakuwa na mwendo mkubwa, itawezekana watu kulala Morogoro na kufanya kazi Dar es Salaam. Reli hii baadae itaelekea Burundi na Rwanda. Itakuza biasha na nchi za jirani kwani biashara za Afrika zina changamoto ya miundombinu na usafiri na inakadiriwa kuongeza gharama ya biashara kwa asilimia 40.

Barabara zetu nyingi zinaharibika kutokana na kubeba mizigo mizito, tafiti zinaonyesha reli ina uwezo mkubwa wa kubeba mizigo mizito. Itatoa ajiri kupitia sekta mbalimbali, nawasihi watanzania wenzangu kujipanga ili kunufaika na mradi huu.

Mradi umegawanywa katika vipande vitano na cha kwanza tunaweka jiwe la msingi leo kipande ambacho kitakuwa na kilomita 300, itatumia umeme pamija na diesel. Tumeambiwa watamaliza ujenzi huu ndani ya miezi 30. Bahati nzuri fedha hizi zipo, mradi huu fedha zimetengwa katika bajeti ya mwaka huu.

Malipo ya awali yamelipwa wiki iliyopita ya bilioni 300 na inaweza kuwa jibu zuri kwanini fedha za maendeleo huwa hailipwi mapema kwani lazima mkandarasi awe sehemu ya ujenzi(Site). Rais wa Uturuki kasema atatuma mabenki yao ili iwezekane kapata mkopo nafuu kumaliza kipande cha Moro-Dom.

Benki ya dunia wametoa bilioni 300 kukarabati reli ya zamani ili iendelee vizuri.

Wale waliozoea kusoma kwenye mitandanao, wakasome kwenye mitandao nchi nyingine iliyojenga reli kama hii kwa fedha zake yenyewe.

Dereva mzuri hutakiwi kusikiliza nyimbo wala watu walipoelekea, angalia lori linapoelekea ili ulifikishe salama, mimi ni dereva mzuri. Nawahakikishia lori liri litafika kule tunapoenda, nawahakikishia tutafika.

Ukiona wanaopiga kelele, ni wale waliozoea kupiga dili, ni lori la watanzania na hasa watanzania masikini. Nchi nyingi za Afrika uchumi wake unakuwa kwa asilimia moja lakini Tanzania uchumi wake unakuwa vizuri katika nchi tano bora kwa asilimia 7.

Ninafahamu niliahidi kwa niaba ya watanzania, tunajua tunapoenda, asitokee mtu atupe mambo mengine ambayo hayapo kwenye ilani yetu ya uchaguzi. Najua tunajenga kwa miezi 30, contractor ajitahidi amalize kabla ya miezi 30.

Vita ya kupambana na ufisadi ni ngumu hasa unapowabadilisha watu walizoea kwa miaka 50 katika ufisadi, ukimkunja lazima atavunjika tu. Samaki akishakomaa mvunje tu. Kutoka moyoni nafanya kazi kwa niaba yenu. Mlinituma nifanye, ni mabaya? Niendelee? Ninawashukuru sana, tumechezewa sana, Tanzania tunaweza.

Kunachezeka michezo ya watu ambayo hata hamuwajui kutaka kutuchonganisha, South Sudan wamepata uhuru juzi lakini wanapigana. Ninayafahamu madhara ya DRC, nchi nyingi zilijaribu kupiga hatua zilichanganishwa. Tutangulize Tanzania kwanza, siasa baadae, hakuna mtanzania anaekula siasa, watu wanataka maendeleo.

Tuangalia Tanzania kwanza, muiache serikali ya chama cha mapinduzi iliyochaguliwa miaka mitano ifanye kazi. Ni matumaini yangu reli itajengwa kwa ubora inayotakiwa, hapa imeandikwa 160, hata mkifanya 180 sio mbaya, watanzania wanapenda spidi pia.

Mungu ibariki Tanzania, ibariki reli hii, sasa niko Tayari kuweka jiwe la msingi. Mama Hawa Ghasia njoo usalimie kidogo kuwawakilisha wabunge.

Hawa Ghasia: Kwa niaba ya wabunge wenzangu, tumefurahi kushiriki katika shughuli hii ya kihistoria, reli ni kama mishipa ya fahamu katika mwili wa binadamu. Nakuhakikishia kama tulivyopitisha bajeti na mwaka 2017/18 bajeti ya miundombinu itapita bila matatizo na kwenye kamati imeshapita.
 
Mkuu wa mkoa dar poul makonda amedai kwa sasa Dar ni salama kuliko hapo nyuma kwani huko nyuma kulikua na matukio mengi ya mauaji ya majambambazi hofu iliope inatengenezwa na watu wachache ameyasema hayo leo wakati wa sherrhe za uwekaji wajiwe la msingi wa reli mmpya
 
Nimeona kwenye uzinduzi wa reli ya STD gauge, wakati RC Bashite amepewa nafasi kumkaribisha Rais camera za Azamtv hazikumpiga picha za video kuonyesha sura yake, alisikika sauti yake tu, anasema kesho atashangaa kuona hakuna kwenye headlines uzinduzi wa reli katika Frontpage za magazeti ya kesho, kweli Bashite ni mpenda kiki.
 
Nampongeza ila hivi ilikuwa ni lazima azindue leo tarehe 12/04? siku ya kumbukumbu ya kifo cha Waziri Mkuu Edward Moring Sokoine? Au ndio anaiadhimisha kwa staili hii? (Kuzindua kwa heshma ya Hayati, Sokoine?)
 
Mkuu wa mkoa dar poul makonda amedai kwa sasa Dar ni salama kuliko hapo nyuma kwani huko nyuma kulikua na matukio mengi ya mauaji ya majambambazi hofu iliope inatengenezwa na watu wachache ameyasema hayo leo wakati wa sherrhe za uwekaji wajiwe la msingi wa reli mmpya

Hayo mambo aliyosema yanauhusiano gani na uzinduzi wa reli?
 
Habari waungwana,

Leo Rais Magufuli anazindua reli ya kiwango inayofuata kiwango cha kimataifa(Inakadiriwa 55% ya reli yote duniani imetumia kipimo hiki na reli zote zenye mwendokasi mkali zinatumia kiwango hiki ukiacha Urusi, Uzbekistan na Finland).

Fuatana nami kujua kitachojiri kutoka Pugu.
========

Kwa sasa wanatambulishwa wageni mbalimbali na kabla alizungumza mkuu wa mkoa wa Dar, Paul Makonda.
Kudos Rais wangu Makini .... Historia itakuja kukubeba kwa utendaji wako uliotukuka ...
 
z
Mkuu wa mkoa dar poul makonda amedai kwa sasa Dar ni salama kuliko hapo nyuma kwani huko nyuma kulikua na matukio mengi ya mauaji ya majambambazi hofu iliope inatengenezwa na watu wachache ameyasema hayo leo wakati wa sherrhe za uwekaji wajiwe la msingi wa reli mmpya
iro brains reli na train zinahusiana nini na vifo vya majambazi kupungua ndo usalama kwli alitaga huyu hapo kakariri usiku kucha kuongea upuuzi huo :D:D:D:D:D:D:D:D
 
Back
Top Bottom