Publicity for preparedness::: Another Govermental impotence

Publicity for preparedness::: Another Govermental impotence

ludoking

Senior Member
Joined
Oct 5, 2008
Posts
124
Reaction score
71
Mh Bernard Membe anatoka katika kijiji cha Rondo Chiponda Wilaya ya Lindi Vijijini. Katika harakati zake za kugombea Ubunge aliahidi kuwepo kwa Mahakama na Hospitali katika kijiji alichozaliwa. Alifanikiwa kujenga Kituo cha afya katika kijiji chake kwa ufadhili wa wahisani. Aliahidi kuwepo kwa mahakimu ili wananchi wake wasisafiri Umbali mrefu kwa kesi za kubambikiziwa.

Kituo cha Afya kilichojengwa wakati kinazinduliwa na Mh JK Hakikuwa na Mfawidhi mbali na yule aliyeazimwa kutoka Ofisi ya DMO Lindi Vijijini ili protokali izingatiwe. JK alivyoondoka kituo kilibaki kinaendeshwa hovyohovyo. Mahakama iliyofunguliwa na Rais wa Nchi walikodiwa wafanyakazi ili ku fake wakati wa uzinduzi mpaka sasa Mahakama haifanyi kazi imefungwa tu .

Juzi juzi kwenye wiki ya maji ambayo Kitaifa ilifanyikia Lindi, Jk HUYO huyo alizindua mradi wa maji uliokuwa umehifadhiwa kwenye 'temporary tanks' na kuwa hadaa wananchi kwamba ni maji ya kudumu. Alivyoondoka na wenye ma tanks waka chukua tanks zao na kusepa. Hivi wananchi imefikia hatua ya kudanganywa hivyo kwa maslahi ya wachache???? JPANGE CHUKUA HATUA

Kwa sasa mikakati mingi, na uadhimishaji mwingi faking strategies za Kitaifa unafanyika Kusini...nguvu nyingi zinaelekezwa KUsini hususani Lindi kwa kuwa Tu!!! Mama Salma ana nia ya Kugombea Ubunge jimbo la Lindi Mjini!!!!....Msio yajua haya, sikilizeni nyimbo za Kundambanda
 
Umeandika mengi bila kuweka ushahidi JF tunapenda ushahidi kama picha,video,audio au documents.Hauna maooni mengi sababu hujaweka vielelezo.
 
Back
Top Bottom