Nakumbushia swali languProfessor ni mtu wa Morogoro
Kuna sehemu niliona ulikuwa unamuunga sana mkono Lissu ndio maana nikahisi wewe ni CHADEMAHapana...
Mambo yangu yote yamekua yanasimamiwa na kusababishwa na serikali iliyopo madarakani...
Cc: mahondaw
Polisi wapi?Kwa uwezo wa Jeshi letu la Polisi, nina uhakika atapatikana akiwa hai
Punguza chuki kwa PolisiPolisi wapi?
Polisi hawa hawa wa Tanzania wanaokulinda wewe pamoja na familia yako.Polisi wapi?
Halijajibiwa mkuuAkikujibu uni tag
Nimemuona amemjibu Upepo wa Pesa hapo juu, ila swali lako amelikwepa kijanja janja tuHalijajibiwa mkuu
Ni kwa sababu habari hii nimeiona sasa na sio wakati ule. Nilikuwa sijui kama Waziri Kabudi alikwishatoa kanusho juu ya ile kauli yake.Kwanini sasa sio wakati ule?
Mbinu za kitotoNi kwa sababu habari hii nimeiona sasa na sio wakati ule. Nilikuwa sijui kama Waziri Kabudi alikwishatoa kanusho juu ya ile kauli yake.
Kwani kumshauri mtu ndio kumlaumu?...Unamlaumu John M. Kabudi
Kwanini unasema hivyo mkuu?Mbinu za kitoto
Ninadhani waliompa nafasi wanajua vema kuzidi mimi na weweUnamlaumu John M. Kabudi wakati unafahamu Sio Mwadiplomasi mzuri maana hawajawahi kufanya kwa Vitendo zaidi ya nadharia ta Darasani
Soja wanadiplomasia mzuriHabari za wakati huu kaka na dada zangu wote wa hapa JamiiJorums.
Ninajua fika baada ya kuandika thread hii kuna watu watanitukana sana, wengine watasema ninajipendekeza kwa wakubwa, wengine watasema ninatafuta uteuzi, wengine watasema mbona ninajishushia hadhi.
Ila ninachosema mimi ni kuwa sipo hapa jukwaani kwa minadi ya kufurahisha watu. Bali nipo hapa kuongelea ukweli kama ambavyo unapaswa kusemwa.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Profesa Palamagamba Kabudi aliwahi kukanusha kuwa amethibitisha 'kifo' cha mwanahabari Azory Gwanda.
Msemaji mkuu wa serikali ya Tanzania, Dkt Hassan Abbas alimnukuu Profesa Kabudi kwa kupitia mtandao wake wa kijamii wa Twitter akisema: "Nimepokea kwa masikitiko taarifa potofu zinazoendelea kuchapishwa kwenye mitandao ya kijamii ikinukuu kimakosa mahojiano yangu kwenye kipindi cha BBC FOCUS ON AFRICA zikidai kuwa nimethibitisha kwamba mwanahabari Azory Gwanda amefariki dunia."
Lakini Prof Kabudi pia alisema bado haijulikani kama Bw Gwanda yungali hai: "Mpaka sasa hakuna uthibitisho kuwa Azory yuko hai au amefariki. Vyombo vya ulinzi na usalama vinaendelea kuchunguza tukio hilo na matukio mengine yaliyotokea katika machafuko ya Kibiti, Pwani yaliyosababisha ama watu kadhaa kupoteza maisha au kupotea."
Kabudi alisema kuwa, kilichotokea ni tafsiri potofu ya kile alishokisema: "Hii sio tafsiri sahihi kuhusu kile nilichokisema. Katika mahojiano hayo nilieleza kuwa tukio lililotokea Kibiti lilikuwa ni la kuhuzunisha na wapo watanzania waliouawa na wengine kupotea. SIKUTHIBITISHA kuwa Azory Gwanda amefariki."
USHAURI WANGU WAZIRI KABUDI ANGESEMA MANENO HAYA
=====
Nilichokisema ni kweli kuwa Azory Gwanda alikufa. Azory alikufa ndani ya mawazo, akili na mioyo ya wanaharakati ambao kila uchwao walikuwa wakiisumbua serikali kwa kuihoji juu ya taarifa sahihi za mahali alipo na hatua za upelelezi zilizofikiwa na jeshi letu la Polisi.
Sisi kama serikali tunatambua vema mchango wa makundi haya ya watetezi wa haki za binadamu pamoja na asasi za kiraia katika kutukosoa na kutukumbusha juu ya wajibu wetu kwa jamii ya watanzania iliyotupa dhamana ya kuwaongoza.
Kwa niaba ya waziri wa mambo ya ndani, ninapenda kutoa tena salamu za pole kwa familia ya Azory kwa kupotelewa na mpendwa wao na taarifa kamili juu ya tukio hili zitatolewa pindi upelelezi utakapokuwa umekamilika.
Tunaahidi kuwa tutahakikisha kunaendelea kuwa na mazingira bora, salama na rafiki kwa wanataaluma wote wa tasnia hii ya habari kuweza kufanya kazi zao kwa ufanisi na weledi wa hali ya juu.
=====
Ni bora baba yangu mzee Kabudi angesema maneno haya.
USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Kama hauna ushahidi wa kutosha kaa kimyaMoja ya sifa mbovu ya huu utawala wa kiimla ni kuteka, kutesa na kuua