Ukilamba mkopo Benki then Unaacha hapo vp?
Ukiona kiza kimezidi ujue kunakaribia kupambazuka lakini pouwa.
Niliachishwa kazi toka mwaka jana mwanzoni nimefatilia kila hatua nimefikia hatua wamenichukua alama za vidole nikarudi nikaambiwa kuwa ukweli hamna pesa ya kulipwa wanasubiri muongozo sijarudi tena nikienda mara yamwisho mwezi wa Saba nimekata tamaa nimemwachia mungu wacha wale tu haki yangu lakini haitakwenda bure mungu awalani woote walio sababisha
Sidhani. Naona kiza kinashika hatamu
Analeta falsafa za mwenda pole,hadithi za vifaranga vya kuku kila siku vinaamini vitanyonya Kesho matokeo Hadi kisu cha Christmas kinawafikia
Tuendelee kuwa na imani labda yanaweza kubadilika mambo
Hawatakutafuta bank kwani? Au mafao yako ndio yanakua kama dhamana? Niliona mikopo ya bank mpaka mwanachama awe amechangia kwa miaka mitano au kumi ndipo anaweza kutumia michango yake kama collateral bank
49 loo parefu mno. Hivi serikali haioni kuwa hapa imechemsha. Fikiria kijana wa miaka 18sasa anafanya kazi unskilled labour. Huyu baada ya kufika miaka 35 au 40 hataweza kufanya kazi za manguvu za kule migodini au kazi ya kukata miwa kwenye sugar industry. Hutu anahitaji sana fao la kujitoa ili akazifanyie shughuli kwa manufaa ya families yake. Serikali ione huruma kwa tabaka hili pia na wale wanaoachishwa kazi ndani ya umri huo 30 - 50.Mabadiliko PPF na NSSF imekuwa mwiba mchungu na wenye sumu kali kwa wafanyazi wanyonge yaani malofa.
Blabla zinazoendelea sasa kuhusu fao la kukosa ajira kama mbadala wa withdrawal, ni geresha tu. Ukweli ni kwamba mifuko ya hifadhi ya jamii ni source nzuri sana ya mapato kwa Serikali.
Ukweli ni kwamba Gvt imeamua makusudi kuwaibia wanachama wa mifuko hii na umma unapumbazwa kupitia vibaraka kama SSRA na baadhi ya wahariri wa media.
Si kweli kwamba Serikali inajali welfare ya mtanzania atakapokuwa mzee wa miaka 60. Ni unafiki mtupu. Wanajua wakikunyima pesa yako sasa utakufa anyway na hivyo kutodai mafao yako.
Hivyo PSSSF na NSSF kupendelea kuneemeka kwa pesa za wafu. Cursed SSRA. Why nilazimishwe kusubiri miaka 55 kuchukua pesa yangu ya mafao baada ya kuachishwa kazi? Kwa nini nilazimishwe kuchukua roborobo kupitia ujinga unaoitwa unemployment benefit!!? A stinking usanii!
Wanasema unapoacha kazi sehemu A uombe kazi sehemu C! Hivi akina lousy Mhagama wanajifanya hawajui ugumu wa kupata ajira Bongo? Kwa uchumi gani?
Wanapata wapi courage ya kumwambia mtu aliyeacha kazi akiwa na miaka 49 asubiri hadi miaka 60 ndio achukue pesa zake ambazo kiukweli ni ndogo masikini. Nani atamwajiri mtu mwenye miaka 50?
Nasikia hawajazingatia hata mfumuko wa bei. Ukiwa na laki moja baada ya miaka 10 utakuja kulipwa kiasi hicho hicho. No interest. No nothing. Huu ni mpango wa ovyo kabisa na ni kaburi kwa wanachama wenye mishahara midogo.
Mtu ana milioni 2 mnataka kumpa kidogo kidogo eti kusubiri apate ajira nyingine. Si mumpe hela yake akajiajiri?
This is a great injustice and the whole law is bad very bad to low income earners.
Ajira hakuna waacheni wanachama watafute plan B. Kwani lazima kuajiriwa? Watu wapewe pesa zao bwana pindi tu wanapoacha kazi.
Mtajitakia laana za bureee wanachama wakifa kabla ya kulipwa fedha zao.
Kila nikikutana na mada yoyote kuhusu mafao huwa napatwa na jaziba mithili ya Mbogo aliejeruhiwa na kuomba hii nchi ikumbwe na dhoruba la Tsunami,Catrina au Kimbunga Juddy, kiondoke na wanasiasa wote waliopitisha sheria hii kandamizi.
Nina hela zangu nssf na lapf mpaka sasa sijapata hata 100.
Kila nikikumbuka hela zangu lazima nipige dua kwa mungu na shetani wamalize tofauti zao ili washirikiane kuwatifua hawa watesi Wetu.
Nasema ipo siku dua zetu zitapolelewa.
Waserikali wanalipwa 30% ya mafao Yao mengine mdogo mdogo
Nashukuru mungu nilishapata pesa yangu bila kutarajia AlhamdulillahNiliachishwa kazi toka mwaka jana mwanzoni nimefatilia kila hatua nimefikia hatua wamenichukua alama za vidole nikarudi nikaambiwa kuwa ukweli hamna pesa ya kulipwa wanasubiri muongozo sijarudi tena nikienda mara yamwisho mwezi wa Saba nimekata tamaa nimemwachia mungu wacha wale tu haki yangu lakini haitakwenda bure mungu awalani woote walio sababisha