Proved: Halima Mdee alinena

Hajampa Mbowe na pia hawezi kwani anachagua wanyonge. Kwanini uzungumzie mambo ambayo hayajatokea?
Hana uwezo wowote NCCR tu imemshinda ndio uwe uwaziri jamaa yako kachemka kinoma.

Tumeshawazoea huwa mnataka jambo lolote lifanyike mtakavyo nyinyi mlitaka ateue mtu kutoka kwenu imekula kwenu kawaida yenu kupiga makelele kama vyura mabondeni usiku, lolote lile ata liwe zuri halina ubaya wowote nyie mnapinga tu ili mradi mtekeleze wajibu wenu wa kuitwa wapinzani,Ndiyo kawaida yenu nyie Wagambo!
 
hapa anapanua wigo wa siasa na kuondoa siasa za mazoea na za chuki dhidi ya vyama vya siasa ili hata wa cdm akipata na akafanya hivyo watu wasione km ajabu...na ieleweke kumpa mbatia hiyo nafas sio kwamba ccm haina watu au wanachama makini

Kwa nini afanye hivyo sasa akiwa amebakiza miaka miwili na nusu kuondoka na sio miaka saba iliyopita tangu aingie madarakani!!! Kuna kitu fulani kimejificha katika hili... Muda ukifika litafichuka tu!!
 
Jamani muwe wakweli wengine ikiwa kwenu hamsemi,mbona alipoteuliwa prf.WESIGA BAREGU Kwenye tume ya katiba hamkusema pandikizi?na zaidi ya yote Baregu akamsifia jk nkwa uteuzi mzuri

Baregu alipendekezwa na chama chake wewe kuwa mjumbe, na kila mmoja wetu alikuwa anajua kuwa lazima atateuliwa mjumbe mmoja kutoka chadema, sio kama ilivyokuwa kwa mbatia kuteuliwa from nop where!..
 
Nakubaliana na Mhe Mabere Marando aliyewahi kusema kuwa James Mbatia anaiua NCCR-Mageuzi.....Sidhani kama Wabunge wa NCCR watakuwa na nguvu ya upinzani bungeni wakati ambapo M/Kiti wa chama chao amekubali kuteuliwa kuwa Mbunge wa Viti Maalum na M/Kiti wa CCM....huu mkakati ulifanywa kwa CUF na sasa wamepoteza dira, sera, mwelekeo na fikra....
 
Kwa hiyo huyu Mbatia pale bungeni atakuwa mbunge wa CCM?, au NCCRCCM?, au viti maalum?. Ni dhahiri huyu ni pandikizi hivyo wapinzani pale bungeni wamuogope kama ukoma.

Hapo nami najiuliza sana,atakuwa anasimama kwa chama gani
 
lakini je huu ni utaratibu mzuri wa kujifanya mpinzani mara unateuliwa na watawala walioshindwa na kuwaungusha wananchi. Kikwete kashindwa kazi na sasa anatafuta wa kufa nae. Mbatia anaweza kuifkiri ameula. Lakini mnafiki huumbuliwa na mungu iko siku ataumbuka .kikwete si wa kuambatana nae kwanza yeye siyo role modal aah role modal wa mambo mabaya ya kufilisi nchi na mareafiki . Kusafiri sana. Baba anayesafiri sana atalima saa ngapi? Alikabidhiwa nchi ikiwa na akiba ya bot ya miaka 3. Sasa tumuulize amepeleka wapi hiyo hazina hadi anashindwa kuendesha serkali? Sasa hivi nchi inaendeshwa na mafisadi ndio wanaofadhili serkali ya kikwete kwa kilakitu. Iko siku huyu jamaa atakimbia nchi msipoangalia
 
Msisahau, Mh. Dr. Slaa alifanya kazi kubwa kuzima soo kati ya Mbatia na Mdee. Uzi huu unaweza kumtibua Mbatia avunje muafaka :becky:
 
Kwa heshima aliyonayo Mbowe pamoja na Busara zake hangeweza kukubali Ubunge au Uwaziri wa kupewa na JK. Huyu JK anaona nchi inamdodea sasa anataka lawama ziende kwa vyama vyote! Alianza na CUF sasa NCCR Kesho atajaribu kuwabipu CDM ila washamshtukia!!!
 

Hillary Clinton alikuwa mpinzani wake ndani ya chama chake cha Democrats
 
...blah, blah, blah...watu tunashindwa kuelewa nini maana ya demokrasia ya kweli au kukuwa kwa demokrasia....hivi leo hii watu wengi huitolea marekan km nchi iliyopiga hatua ktk demokrasia....
Sawa, lakini tuanze kwa kuangalia etiquette ya internet... font na rangi unayotumia, ni dalili ya ulimbukeni. Why are you trying to ram down our throats whatever it is that you believe! Hii ni dalili ya kukosa uvumilivu kitu kinachopingana kabisa na dhana ya msingi ya demokrasia, what are you trying to hide, mapungufu yako ya uelewa?
kwa mfano Obama pindi anagombea urais Hillary Clinton alikua mpinzani wake lakini sasa hivi huyu mama ndie waziri wa mambo ya nje kwan huyu mama kaathiri kitu gani kwa utendaji wa Obama na serikal yake???
Kwanza Obama na Mama Clinton wote ni democrats na walikuwa wanagombea uteuzi ndani ya Chama chao, mfumo ambao huujui na hata ukiujua hutauelewa. Siasa ya Marekani ni zaidi ya uijuavyo kwani mara baada ya uteuzi wa mgombea Uraisi kukamilika ndani ya chama, wagombea huzika tofauti zao na kuwa kitu kimoja katika kampeni. Ndio maana hivi sasa ndani ya chama cha Republican, wapinzani wa Romney wote wanaanza kumuunga mkono moja baada ya mwingine katika kuipeperusha bendera yao.
Hapana, ni ajabu na ngeni...Kwanza, marekani wabunge hawateuliwi na Raisi, wanachaguliwa na wananchi kama ilivyo kwa Raisi mwenyewe. Mbunge wa Marekani hafungwi mkono kukitetea chama chake, anaweza kabisa kupingana na msimamo wa chama chake na kuwaunga mkono upinzani. Huko ndiko kupanua wigo wa demokrasia na siyo huu usanii unaofanyika Tanzania, eti mtu aliyekataliwa na wananchi anakuja kuteuliwa na Raisi, this is not democracy, it is disingenuousness!
na ieleweke kumpa mbatia hiyo nafas sio kwamba ccm haina watu au wanachama makini sio hivyo hiyo ndio maana halisi ya siasa za kuvumiliana na kuheshimiana na kwa uwazi zaidi...
Acha upuuzi, Mbatia ni mwenyekiti wa chama cha NCCR aliyegombea ubunge na kukataliwa na wananchi...sasa huko kuvumiliana na kuheshimiana kwa uwazi zaidi kunatoka wapi? Huyu huyu Mbatia amewahi kutuhumiwa na wenziwe ndani ya chama chake kwa undumilakuwili na unafiki na najua hizo ni sifa kubwa ndani ya CCM, je hizo ndizo sifa zilizomkuna aliyemteua? KONGOTO, please think out of the box!
naomba tubadilike SIASA HAINA ADUI WA RAFIKI WA KUDUMU''' naomba kuunga mkono hoja
Toka lini Mbatia amekuwa adui wa Kikwete kisiasa, last I heard ni kuwa amekuwa na tabia ya kumtetea Raisi hasa pale anapotupiwa lawama kiutendaji. KONGOTO, nakuomba sana usiwe mvivu wa kufikiri na ujaribu kutafakari kwa mfano huko visiwani tunayo serikali ya mseto, je unaweza kudai kuwa kwa kufanya hivyo wigo wa demokrasia umepanuliwa? Haiingii akilini mtu mwenye akili timamu kuunga mkono hoja ya kijinga kama ya kuopoa viongozi kutoka katika dampo walikotupwa na wananchi.
 
Last edited by a moderator:
Jamani muwe wakweli wengine ikiwa kwenu hamsemi,mbona alipoteuliwa prf.WESIGA BAREGU Kwenye tume ya katiba hamkusema pandikizi?na zaidi ya yote Baregu akamsifia jk nkwa uteuzi mzuri
Mkuu umefika sehemu nyingine kabisa kwani kuna member wengine wa tume waliopigiwa kura na wananchi? ili tuseme baregu kapewa umember maalumu? Pia tunaangalia uwezo wa mtu Mbatia kilaza sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…