Pole sana bro miaka ya nyuma kama 40 iliyopita wanafunzi wakimaliza chuo kikuu walikuwa wanagoma kuondoka hadi wapewe ajira. Kwanini? wasomi walikuwa wachache chuo ni mlimani na sokoine tu.
Miaka hiyo hata kumaliza tu form six ni bonge la msomi.
Sasa hali imebadilika vyuo vikuu viko 40 watanzania wameongezeka ajira hakuna infact ni maendeleo.
Hata nchi zilizoendelea zamani nilikuwa naambiwa mwalimu wa primary anaweza kuwa na shahada.Kwa huku kwetu ilikuwa tofauti diploma ndio mwalimu wa sekondari o level degree sekondari lakini anafundisha high school.
Sasa mambo yamebadilika hata ukiwa na degree unaweza kosa hata hiyo ajira ya kufundisha primary serikalini.
Cha muhimu kwa sasa ukisoma ondoa wazo la kuajiriwa.Maendeleo ndo changamoto zake.