PreGE2025 Prosper Tesha: Wachimbaji madini tumekubaliana kura zetu zote ni kwa Rais Samia

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Wont be the same

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
1,564
Reaction score
2,483
Wachimbaji wa madini nchini wamejitokeza kwa nguvu kuunga mkono juhudi za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuboresha sekta ya madini, huku wakiahidi kumpigia kura kwa kishindo katika uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu.

Mwenyekiti wa Madini ya Vito Prosper Tesha ameyasema hayo hivi karibuni katika taarifa yake wakati wa ziara ya Naibu Waziri Mkuu Dkt. Doto Biteko alipotembelea eneo la Mundarara yanapochimbwa madini ya Rubby wilayani Longido mkoani Arusha.

Tesha ambaye pia ni Mkurugenzi wa kampuni ya uchimbaji wa madini ya RGI Company Ltd amesema mafanikio yaliyopatikana chini ya uongozi wa Rais Samia, hususan katika sekta ya nishati na madini, ni ushahidi tosha wa uongozi unaojali maendeleo ya Watanzania.
Your browser is not able to display this video.
 
Acha uongo Mimi nimchimbaji , mbona sijahusika kwenye kikao kilichofikia muafaka wa Makubaliano hayo, Jifunze kuwa mkweli angalau kidogo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…