Promotas na maneja - duh hii inasikitisha sana

Promotas na maneja - duh hii inasikitisha sana

mbongopopo

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2008
Posts
1,611
Reaction score
764
Habari hii inasikitisha




TEMBA PHOTO NA VIJIMAMB
O INAMASIKITIKO MAKUBWA KUWAAMBIA ILE SHOW YA YAMOTO MEMORIAL WEEKEND HAITAKUWEPO



Temba Photo na Vijimambo Media & Entertainment inamasikitiko makubwa kuwataarifu wadau wake kwamba lile Tamasha la bendi ya Mkubwa na Wanae (Yamoto) lililokua lifanyike New York na Washington, DC May 22 na 23, 2015 sasa halitafanyika kutokana na poromota mwingine wa Marekani kuingilia kati baada ya kuona Tangazo kwenye Vijimambo kwamba Temba Photo wakishirikiana na Vijimambo Media & Entertainment inawaleta Yamoto Band.

Maongezi ya Yamoto Band yaliyofanywa kati ya NY Ebra na Meneja wa kikundi hicho bwn. Said Fela na kukubaliana gharama zao za kufanya maonesho New York na Washington, DC na kilichokua kimebaki ni taratibu za kuwaombea VISA ya Kazi na hatimaye waweze kuja na kutoa burudani kwa wadau na wapenzi wa kikundi hicho nchini Marekani..

Chakushangaza ni tangia juzi kati Ny Ebra alipompigia simu Bwn. Said Fela, hakutoa tena ushirikiano wa kutosha na kumweleza kuwa ameongea na poromota mwingine wa huku Marekani na kumtaka waje mwezi wa April badala ya onesho letu lililokua lifanyike mwezi May na cha kusikitisha poromota huyo akamwambia aatueleze tumpigie simu pamoja na kwamba hicho hakikua makubaliano hapo mwanzo hata hivyo Ny Ebra alimpigia simu huyo poromota mara kadhaa lakini hakupokea simu yake.

Jana Jumanne March 17, 2015 NY Ebra alijaribu kumpigia Bwn. Said Fela kutaka kumjulisha kwamba poromota wake hapokei simu. Bwn. Said Fela hakuipokea simu yake. Leo March 18, 2015 NY Ebra alimvutia waya tena Siad Fela lakini Meneja wa kikundi cha Mkubwa na Wanae ilishaonesha ameishajazwa pumba nyingi ndipo NY Ebra kwa niaba ya Vijimambo na Temba photo aliamua kubwaga manyanga na kusikitika na tabia maji taka aliyofanya poromota huyo ambayo anapokua na onesho au shughuli moja wapo Vijimambo na Temba photo uheshimu shughuli yake. Hii sasa ni kuvuka mipaka na Vijimambo na Temba photo tunalaani vikali tabia kama hii.

Mwisho tunawaomba radhi wadau wetu na tunaagalia kwa sasa ni msanii gani mwingine tumlete kwa ajili ya kutoa burudani na kukata kiu yenu ya muda mrefu.

Vijimambo na Temba photo inawatakia kila la kheri Yamoto Band kwa onesho lenu Marekani

Asante

Uongozi Timu Vijimambo kwa ushirikiano na Temba photo

source: vijimambo blog

%%%%%%%%%%%%%%%%%%%%%%%%%%%%

ya kwangu:

=> nimekumbana na hii habari wakati nasoma blog hii kama kawaida yangu

=> Kwa kweli ningependa na kufurahi kama wangetaja jina la huyo promota sababu wana namba yake ya simu ili next time asirudie kuiba kazi za watu kwa connection labda na aheshimu kazi za watu. wote mko mbali ya home(TZ) why wengine nao wasifanye kazi zao kujiendeleza? watanzania kwanini kurudishana nyuma?

=> Why kumwingilia mtu mwingine kazi ni kwasababu ya tamaa ya pesa? je mlishindwa nini kuwatafuta nyie kwanza? je kwa nini muwe nyie tu na wengine aleta wasaniii?

=> Na wewe meneja kwa nini kiherehere hata kama unakimbia si uwaeleze kuwa hautaki kazi na tena? unamaneji vipi hayo na ona sasa umeharibia watu kazi na matayarisho bookings etc. wewe maneja ni hatari na sio vizuri waeleze sio kukimbia wateja ni wananchi kumbukeni msije jikuta wenyewe.


=> na nyie mliokuwa mnasubiria wapewe visa, ni kazi gani mnafanya bila kuandikiana mkataba hata ule wa wao kukubali kazi kwanza mkiwa mnajiandaa kutayarisha?
natumaini mmejifunza

kutype kutumiana na mtu awepo na TZ wapige saini na kwa niaba yenu. ningependa muelewa wa haya labda atueleze mie nashangaa.


 
Back
Top Bottom