6. ALFONSO CANO
jina lake kamili ni Guillermo Leon Saenz Vergas, alikua kiongozi wa waasi wa FARC(Fuerzas Armadas Revolucionarias de Colombia au kwa kizungu revolutionary armed forces of colombia)
lengo lao kubwa ni kutaka colombia iongozwe kwa mfumo wa kikomunisti. waliwapigania maskini dhidi ya mabeberu wa colombia pia walipinga ushawishi wa marekani nchini mwao.
ili kupata pesa za kukiendesha kikundi, waliuza dawa za kulevya, kutoza kodi kwenye maeneo waliyoyatawala, na kuwauza mateka waliokuwa wanawashikilia. pia inadaiwa kuwa comrade Hugo chavez rais wa zamani wa venezuela alikua anawapa msaada wa fedha
alfonso cano aliuawa kwa kupigwa risasi na majeshi ya serikali mwaka 2011