Project yangu mpya ya "Fruit Garden"

Zero IQ

JF-Expert Member
Dec 21, 2016
13,917
24,673
Sijui kama kibongo bongo kuna mtu ameshawahi kuwaza hii.

Leo nimekaa nimefikiri sana nikapata wazo na kuja na hii project niliyoipa jina la Fruit Garden (bustani ya matunda),sema tu pesa sina ningejaribu kuifanya.

Project ni ngumu inaitaji pesa na muda, ili kuitekeleza na kuwa vile mawazo na fikra zangu zinataka iwe.

Project yenyewe ni kutengeneza Bustani ambayo ndani yake itakuwa imesheheni miti mbali mbali ya Matunda,ambayo watu watatembelea na kujipatia matunda fresh yakichumwa na kuliwa papo kwa papo.

Ni hivi lipatikane eneo karibu na mji, kama hekari moja na zaidi. Eneo lipigwe fensi fupi, na juu ya fens ziwekwe chuma flani za kuchomelea ambayo itaruhusu wapita njia kuiona bustani ndani kwa urahisi,

Eneo litengenezwe vizuri na ndani ya bustani yatengenezwe mazingira flani kwa kupanda miti ya kutosha ya matunda pekee , kama vile maembe, mananasi, machungwa, maparachichi, maapple,matikiti, zabibu, na miti mingine mingi ya matunda, kwa ustadi na kwa mpangilio wa kuvutia.

Then kupitia miti ya matunda ile mirefu, au ndani ya bustani zitengezwe gardeni nzuri zenye viti stadi vitakayowezesha watu wanaoingia kupumzika na kupata sehemu za kulia matunda wanayoitaji.

Kwa kifupi: Project iwe ni ya kuzalisha matunda na kuyauza yakiwa fresh kwa wateja wanaokuja kutembelea bustani hiyo na kupumzika.

Matokeo ya project hii ni kubwa haraka haraka tu kwanza kupitia fensi inayozunguka bustani kuwekwe gate ambalo watu watapita hapo kwa gate pass (kiasi flani cha pesa) ya kuwezesha kutembelea bustani hiyo, na kwa wanaotaka kupumzika.

Ndani ya bustani yenyewe kuwe na wahudumu ambao ni Nadhifu wa kuwahudumia wateja pindi wanapoitaji kuandaliwa matunda ya kula. Kila tunda likiwa na bei yake, matunda yawe ni fresh tu ni lile litakalo chumwa kuandaliwa na mwisho kuliwa, N.k

Mwisho kabisa kutakuwa na sehemu ya uoteshaji wa miti ya matunda kwa ajiri ya kuuza kwa wateja wanaotembelea bustani hiyo. N.k

Project hii ni gharama kwenye kuitekeleza na inachukua muda lakini faida zake ni kubwa sana kama itafanyika mikoa ya Arusha au Dar es Salam kwa sababu ya wingi wa watu waliopo pamoja na watalii wengi wanaofika kutembeaa katika mikoa hiyo.

NB: Nimendika shortly tu kwa sababu ya muda lakini nafikiri kiasi nitakuwa nimeeleweka.
 
Wazo zuri mmpe mwana CCM wataifanya agenda na:sera za Kila mkoa na wilaya itenge maeneo kwa ajili ya kulima bustani za matunda kwa watanzania wote hili akipat meko atalifanyiaa kazi.
 
Kweli hiyo no zero IQ. Heka moja upande miti yote hiyo au ndio kila sample mti mmoja mmoja! Maana sioni hata hao wateja watakaa wapi maana eneo litakuwa dogo.
 
Ishu ni hali ya hewa,mfano avocados sidhani kama zinastawi vyema Dar. Kingine kwa heka moja kweli itatosha uweke miembe, migomba, mistafeli, michungwa n.k. halafu kingine itafika stage utaifunga kwa kukosa matunda yaliyo tayari.

Nilikuwaga na wazo la kuwa na kama cafe ila ideal na matunda tu pamoja na juice. Hili wazo mpaka leo ninalo bado kulitekeleza tu.
 
Wazo zuri mmpe mwana CCM wataifanya agenda na:sera za Kila mkoa na wilaya itenge maeneo kwa ajili ya kulima bustani za matunda kwa watanzania wote hili akipat meko atalifanyiaa kazi.
we kweli goroka.... hahahhaha kma jina lako.
 
Sijui kama kibongo bongo kuna mtu ameshawahi kuwaza hii.

Leo nimekaa nimefikiri sana nikapata wazo na kuja na hii project niliyoipa jina la Fruit Garden (bustani ya matunda),sema tu pesa sina ningejaribu kuifanya.

Project ni ngumu inaitaji pesa na muda, ili kuitekeleza na kuwa vile mawazo na fikra zangu zinataka iwe.

Project yenyewe ni kutengeneza Bustani ambayo ndani yake itakuwa imesheheni miti mbali mbali ya Matunda,ambayo watu watatembelea na kujipatia matunda fresh yakichumwa na kuliwa papo kwa papo.

Ni hivi lipatikane eneo karibu na mji, kama hekari moja na zaidi. Eneo lipigwe fensi fupi, na juu ya fens ziwekwe chuma flani za kuchomelea ambayo itaruhusu wapita njia kuiona bustani ndani kwa urahisi,

Eneo litengenezwe vizuri na ndani ya bustani yatengenezwe mazingira flani kwa kupanda miti ya kutosha ya matunda pekee , kama vile maembe, mananasi, machungwa, maparachichi, maapple,matikiti, zabibu, na miti mingine mingi ya matunda, kwa ustadi na kwa mpangilio wa kuvutia.

Then kupitia miti ya matunda ile mirefu, au ndani ya bustani zitengezwe gardeni nzuri zenye viti stadi vitakayowezesha watu wanaoingia kupumzika na kupata sehemu za kulia matunda wanayoitaji.

Kwa kifupi: Project iwe ni ya kuzalisha matunda na kuyauza yakiwa fresh kwa wateja wanaokuja kutembelea bustani hiyo na kupumzika.

Matokeo ya project hii ni kubwa haraka haraka tu kwanza kupitia fensi inayozunguka bustani kuwekwe gate ambalo watu watapita hapo kwa gate pass (kiasi flani cha pesa) ya kuwezesha kutembelea bustani hiyo, na kwa wanaotaka kupumzika.

Ndani ya bustani yenyewe kuwe na wahudumu ambao ni Nadhifu wa kuwahudumia wateja pindi wanapoitaji kuandaliwa matunda ya kula. Kila tunda likiwa na bei yake, matunda yawe ni fresh tu ni lile litakalo chumwa kuandaliwa na mwisho kuliwa, N.k

Mwisho kabisa kutakuwa na sehemu ya uoteshaji wa miti ya matunda kwa ajiri ya kuuza kwa wateja wanaotembelea bustani hiyo. N.k

Project hii ni gharama kwenye kuitekeleza na inachukua muda lakini faida zake ni kubwa sana kama itafanyika mikoa ya Arusha au Dar es Salam kwa sababu ya wingi wa watu waliopo pamoja na watalii wengi wanaofika kutembeaa katika mikoa hiyo.

NB: Nimendika shortly tu kwa sababu ya muda lakini nafikiri kiasi nitakuwa nimeeleweka.
Unataka kiasi gani kutekeleza hii project
 
Nikitaja kiasi kiasi cha pesa nitakuongopea kwa sababu bado sijafanya physical study ya mradi ili nijue gharama yake,

ila kwa haraka haraka ni pesa nyingi kidogo inaitajika,
Kwa sababu eneo litaitaji miundombinu ya kusaport kila Aina ya matunda yapandwayo, maafisa kilimo, wafanyakazi na N.K
 
Hiyo inaitwa botanical garden .kwa mara ya kwanza zero atoa idea isiyohusu kuchakatana
 
Ishu ni hali ya hewa,mfano avocados sidhani kama zinastawi vyema Dar. Kingine kwa heka moja kweli itatosha uweke miembe, migomba, mistafeli, michungwa n.k. halafu kingine itafika stage utaifunga kwa kukosa matunda yaliyo tayari.

Nilikuwaga na wazo la kuwa na kama cafe ila ideal na matunda tu pamoja na juice. Hili wazo mpaka leo ninalo bado kulitekeleza tu.
Hili ni wazo, eneo linaweza likawa zaidi,
Kuhusu matunda sasa hivi tupo kwenye kilimo cha kisasa, mbegu za kisasa zenye uwezo wa kuzaa almost mwaka mzima na matunda yakawepo
 
Usisahau kuweka vyumba viwili vitatu vya kupumzikia unaweza jikuta unaopoa mzigo hapo garden ukaenda kuuchakata fasta,itakulipa short time 5000
 
Hili ni wazo, eneo linaweza likawa zaidi,
Kuhusu matunda sasa hivi tupo kwenye kilimo cha kisasa, mbegu za kisasa zenye uwezo wa kuzaa almost mwaka mzima na matunda yakawepo
Kuna drawbacks nyingi sana project ya aina hiyo.
1. Matunda hustawi kwa kutegemea eneo husika. Huwezi kuchanganya matunda ya kila aiana na yakastawi na kuzaa yote.
2. Matunda huzaa kwa msimu. Hata ukiweza kupata eg matunda aina tano yanayostawi eneo moja lakini uzaaji na uvunaji wake hauwezi kuwa wa wakati mmoja.
Yote tisa, lakini bado sioni mantiki ya watu kwenda kuona umuhimu wa kwenda sehemu ya bustani kula matunda wakati wanaweza kwenda sehemu iliyotengenezwa special na kuchagua kula matunda ya aina mbali mbali kutoka sehemu mbali mbali.
 
Back
Top Bottom