Project funding sources

Mzuzu na Malila,

Naombeni kama mna proposal zozote kuhusu machines za kuzalishia, basi mnitumie kwenye email yangu hapo chini.

Mzuzu, niandikie mmekwama wapi na mnahitaji kitu gani ili nijaribu kutafuta wawekezaji wanaoweza kuwasukuma kwenye hilo la kutengeneza starch. Nilikuwa nakufuatilia kwa siku nyingi sana kwenye makala hii hadi jana nilipokutana na jamaa anataka kujenga mashine za kutengeneza SPIRIT. Nikakumbuka kuwa ulisema kwenye mihogo, unaweza pia kutengeneza Spirit. Ndiyo maana nimekuja moja kwa moja kwako na kwa Malila, Mzee wa chungu kubwa.

Kwa sasa sisi hapa na Umoja wetu wa Watanzania Poland(TAP), tukishirikiana na Ubalozi wa Tanzania Berlin, tunajitajidi kutafuta wawekezaji watakaotaka kuwekeza peke yao au kuunga nguvu na Watanzania kwenye miradi ya aina mbalimbali. Nafikiri kwa hili tunaweza tukalifanikisha pia mkapata wadau wenye nguvu zaidi na mkaanza uzalishaji.

Tuwasiliane kwa email: Ssambali@hotmail.com au simu +48503535735 (Chairman, TAP).

Brief imekuja kwa email umeipata?
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Mzuzu,

hebu tuma tena maana sijaipata email yako au imekuja kama spam. Nipo katika kupanga timu ingawa huenda tukaja kivingine.
Kwenye mkutano wa Diasporamwezi wa nane mwqka huu hapo Dar, nilikutana na Mzee mmoja Mtanzania anayeishi Nigeria na kawa huko kwa miaka 33. Mzee huyu inasemekana ndiyo kamleta Dangote hapo Tanzania. Alisema kuwa na yeye/wao wako kwenye mchakato wa kuzalisha hiyo starch. Sijui kama mnashirikiana naye au yeye yuko kivyake.

Hongera sana kwa bidii zenu.

Brief imekuja kwa email umeipata?
 
Moja ya Project Funding Sources ni kutumia Dar Es Salaam Stock Exchange (DSE). Kuna dirisha maalum limeanzishwa DSE kwa ajili ya kusaidia wajasiria mali, linaitwa Enterprise Growth Markets (EGM) au nchi nyingine dirisha hili linaitwa Alternative Investment Market (AIM). Dirisha hili lina masharti nafuu, haliangalii track record ya mradi, linaangalia zaidi uzuri wa project (future prospects), hamna collateral (security) kwa sababu unapata equity funding.
Unaweza kubadilishana mawazo nasi kama utataka. Kampuni yetu imeisaidia SWALA OIL & GAS (T) PLC kuingia sokoni. Kampuni hii ya SWALA tuliingiza sokoni DSE mwezi wa June/July 2014 kwa kuuza hisa zake kwa Tshs 500 per share. Huu ni mwezi Oktoba 2014, hisa za SWALA zinauzwa kwa Tshs 2110 kila hisa kwa bei ya jana.
Email yangu: nsemwa@archfia.or.tz. KARIBUNI WOTE TUBADILISHANE MAWAZO
 
Majaribio ya awali yameanza na wadau mnaweza kuona clip fupi hapa kwa youtube...

FJS African Starch Development Company Ltd. - YouTube

Ilikuwa mawazo, utafiti, utendaji, sasa kiwanda na mashamba yanaonekana Bungu Rufiji. Mzuzu hongera sana.

10458852_1471734719731117_5970189810485567646_n.jpg

10505498_1469664179938171_8230024248486219652_n.jpg

10288738_1443983305839592_928936204665276920_n.jpg

Ufunguzi utafanyika lini mkuu tuje kujifunza na kununua bidhaa zako.
 
Thanks sana kiongozi. Tutakuwa operational mwezi November mwishoni na uzinduzi rasmi utakuwa mwishoni November hiyo hiyo
 
Mzuzu tani moja ya mhogo mnanunua kwa bei gani? na ni aina gani ya mhogo mnayopendekeza wakulima walime.

Kuanzia mwaka kesho kutakuwepo na uhaba mkubwa wa mihogo katika jiji la DSM, wakulima hii ndiyo fursa ya kuongeza ukubwa wa mashamba ya mihogo, kwani sasa soko la uhakika lipo.
 
Tutaanza na Tsh 100 kwa kilo na itaflactuate kuendana na bei ya starch sokoni
 
Last edited by a moderator:
Mkuu ebu tuchekiane kwenye emeail yangu (pamos@amend.org) tufanye kitu

Heshima mbele wana JF,

Nimekuwa nahangaikia kupata habari au msaada wa mawazo kutoka sehemu mbalimbali nafikiri na hapa jamvini lazima kuna msaada mkubwa wa mchango naweza kupata kwani naamini hapa ni kitovu cha taaluma na ujuzi wa mambo.

Kwa muda mrefu sana nimekuwa nikifikiria na kutafuta njia mablimbali za kuweza kufanya sisi kama vijana wa kitanzania katika mambo ya kiuchumi (nikimaanisha kuwa na biashara kubwa) tunazoweza kuanzisha vijana na kutufanya kuondokana na mawazo ya kuajiriwa hasa kwa vijana wenye elimu ya chuo kikuu. Lakini ninasikitika sana kuona watanzania wengi tunagombea nafasi za kuajiriwa tu na serikali yetu haina msaada wowote wa kuwezesha kuleta mafanikio. Serikali yetu inatafafsiri ujasiriamali ni kumwezesha mtu kupata rizki, mi naamini bila viwanda vidogo vya kati huo ujasiriamali hautakuwa na manufaa yoyote, wazalishaji wanatakiwa wajue soko na processing ikifanyika thamani ya mazao yao inaongezeka kwenye masoko ya kimataifa.

Kwa mtazamo wangu nimekuwa nikiamini watu wenye elimu ya chuo kikuu wanatakiwa kuwa na mtazamo wa kuanzisha ajira kwani wao wamepevuka upeo tofauti na waliokosa elimu hiyo.

Kwa wanaJF wanaojua jinsi ya kupata resources jamani ninaomba msaada wa mawazo.

Nimefanya feasibility study kwa miaka kadhaa sasa na hatimaye nimeaandaa business plan ya kufanya processing ya cassava (mihogo) kutengeneza starch. Mali ghafi hakuna asiyejua inapatikana nchi kwetu popote pale unahitaji kuwahakikishia wakulima soko tu na watakufanyia mambo ya kutosha. Hii itainua uchumi wa wakulima wadogo sana na hasa kwenye maeneo ambayo kilimo cha pamba kimeanguka na mikoa kame kama ya kati isiyo na zao la biashara kwani popote inastawi

Soko lipo juu sana na lengo ku export tayari kuna watu wanahitaji sana kuimport kutoka Tanzania nimejaribu kutangaza na kupata response nzuri sana. Kuna soko kubwa sana nchini (yote inaagizwa toka nje esp SA) kuna soko kubwa sana pale TBL na viwanda vingine vinavyotengeneza madawa, nguo, bia, tambi, biscuits, noodles, almost viwanda vyote vinavyotengeneza vyakula (canned na bottled) vinahitaji starch.

Tatizo kubwa nililonalo ni kwamba natafuta source ya funds kuanzisha kamradi haka ambacho profit margin yake ipo juu sana. Nipo tayari kwa mazungumzo specific ya jinsi ya kufanya ili mradi niweze kutimiza hii ndoto. Mradi huu unaweza kuwa expanded katika muda wa miaka 2 au 3 ukawa na plant nyingine ya kuzalisha ethanol kwa kutumia waste materials baada ya kuprocess cassava na tayari nimeanza kudraft plan yake. Nimejaribu kupita Tanzania investment bank na kuongea nao wakawa na interest ya kusaidia ila nikawa sina colateral wala mdhamini mwenye assets nzuri (mimi mtoto wa mkulima tu hata elimu yangu ni ya kuungaunga tu) ninaweza kuraise kidogo tu. Nimepita na NBC ikawa vilevile tu na mradi unakubalika na tatizo siaminiki tu kwa vile sina historia ya kushika pesa kubwa.

Ninaweza kusimamia hii kazi na ikawa juu kiasi cha kuridhisha na kushindana na biashara kubwa tu hata kuanzisha zingine safi zaidi.

Haya wadau naomba reference kwenye source au tujiunege na kuona nini cha kufanya. Nipo kwa wazi nasikiliza mawazo yenu na ushauri! unaweza kuchangia au kuniPM vyovyote utakavyoona

Ahsanteni sana
 
mkuu nicheki kwa 0719168700,tufanye yetu
 
Proposal yako ni ya aina gani ya vituguu. Kuna vituguu vyeupe ndivyo vina bei nzuri soko la nje na hapa nchini pia. Vituguu hivi vinapendwa kwa sababu wakati wa kukata havitoi majimaji machungu yanayoumiza macho. Vinalimwa sana mikoa ya baridi ya Arusha na Kilimanjaro sielewi kwa maeneo ya joto kama vinastawi vizuri
Hivyo vikali pia ni vizuri kwa ajiri ya kuextract compound itayoitwa Cs inTumika sana huko china kwa ajiri ya kutengenezea mabomu ya machozi yaani tear gas .Also pili pili kama pesa ipo hata Tanzania inawezekana
 
Mkuu Mzuzu , Malila et al nawashukuruni sana kwa mawazo yenu ya kujenga. Hakika machozi yana nilenga lenga kwa kuona namna vijana wa kitanzania mlivyotumia sehemu ya akili na ujuzi wenu kuokoa kizazi hiki.
Natumai siku moja mtakuja toa ushuhuda wenu hapa jukwaani namna umoja wa dhati ulivyo wasaidia kufikia nia yenu.
Natamani nimtumie kopi ya wzo lako waziri mkuu , waziri wa kilimo, waziri wa viwanda na uwekezaji ili aone kuwa Tanzania imejaaliwa vijana wenye akili timamu, maono, nia, na maalifa ya kujenga nchi.
Hongereni sana kwa mawazo ya kujenga.
 
Mkuu Mzuzu , Malila et al nawashukuruni sana kwa mawazo yenu ya kujenga. Hakika machozi yana nilenga lenga kwa kuona namna vijana wa kitanzania mlivyotumia sehemu ya aikili na ujuzi wenu kuokoa kizazi hiki.
Natumai siku moja mtakuja toa ushuhuda wenu hapa jukwaani namna umoja wa dhati ulivyo wasaidia kufikia nia yenu.
Natamani nimtumie kopi ya wzo lako waziri mkuu , waziri wa kilimo, waziri wa viwanda ana uwekezaji ili aone kuwa Tanzania imejaaliwa vijana wenye akili timamu, maono, nia, na maalifa ya kujenhga nchi.
Hongereni sana kwa mawazo ya kujenga.

Asante Mkuu,

Naomba nimrudishie Mungu shukrani hizi kwa kuwa tumefanya hicho kidogo kwa uweza wake, naam namwomba Mungu atupe nguvu na uhai na afya ili tufikie malengo na hatimaye tuwe tumechangia maendeleo ya nchi yetu kwa kiasi fulani.

Be blessed mkuu.
 
Back
Top Bottom