Project funding sources | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Project funding sources

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Mzuzu, Sep 22, 2009.

 1. Mzuzu

  Mzuzu JF-Expert Member

  #1
  Sep 22, 2009
  Joined: Jul 11, 2007
  Messages: 487
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  Heshima mbele wana JF,

  Nimekuwa nahangaikia kupata habari au msaada wa mawazo kutoka sehemu mbalimbali nafikiri na hapa jamvini lazima kuna msaada mkubwa wa mchango naweza kupata kwani naamini hapa ni kitovu cha taaluma na ujuzi wa mambo.

  Kwa muda mrefu sana nimekuwa nikifikiria na kutafuta njia mablimbali za kuweza kufanya sisi kama vijana wa kitanzania katika mambo ya kiuchumi (nikimaanisha kuwa na biashara kubwa) tunazoweza kuanzisha vijana na kutufanya kuondokana na mawazo ya kuajiriwa hasa kwa vijana wenye elimu ya chuo kikuu. Lakini ninasikitika sana kuona watanzania wengi tunagombea nafasi za kuajiriwa tu na serikali yetu haina msaada wowote wa kuwezesha kuleta mafanikio. Serikali yetu inatafafsiri ujasiriamali ni kumwezesha mtu kupata rizki, mi naamini bila viwanda vidogo vya kati huo ujasiriamali hautakuwa na manufaa yoyote, wazalishaji wanatakiwa wajue soko na processing ikifanyika thamani ya mazao yao inaongezeka kwenye masoko ya kimataifa.

  Kwa mtazamo wangu nimekuwa nikiamini watu wenye elimu ya chuo kikuu wanatakiwa kuwa na mtazamo wa kuanzisha ajira kwani wao wamepevuka upeo tofauti na waliokosa elimu hiyo.

  Kwa wanaJF wanaojua jinsi ya kupata resources jamani ninaomba msaada wa mawazo.

  Nimefanya feasibility study kwa miaka kadhaa sasa na hatimaye nimeaandaa business plan ya kufanya processing ya cassava (mihogo) kutengeneza starch. Mali ghafi hakuna asiyejua inapatikana nchi kwetu popote pale unahitaji kuwahakikishia wakulima soko tu na watakufanyia mambo ya kutosha. Hii itainua uchumi wa wakulima wadogo sana na hasa kwenye maeneo ambayo kilimo cha pamba kimeanguka na mikoa kame kama ya kati isiyo na zao la biashara kwani popote inastawi

  Soko lipo juu sana na lengo ku export tayari kuna watu wanahitaji sana kuimport kutoka Tanzania nimejaribu kutangaza na kupata response nzuri sana. Kuna soko kubwa sana nchini (yote inaagizwa toka nje esp SA) kuna soko kubwa sana pale TBL na viwanda vingine vinavyotengeneza madawa, nguo, bia, tambi, biscuits, noodles, almost viwanda vyote vinavyotengeneza vyakula (canned na bottled) vinahitaji starch.

  Tatizo kubwa nililonalo ni kwamba natafuta source ya funds kuanzisha kamradi haka ambacho profit margin yake ipo juu sana. Nipo tayari kwa mazungumzo specific ya jinsi ya kufanya ili mradi niweze kutimiza hii ndoto. Mradi huu unaweza kuwa expanded katika muda wa miaka 2 au 3 ukawa na plant nyingine ya kuzalisha ethanol kwa kutumia waste materials baada ya kuprocess cassava na tayari nimeanza kudraft plan yake. Nimejaribu kupita Tanzania investment bank na kuongea nao wakawa na interest ya kusaidia ila nikawa sina colateral wala mdhamini mwenye assets nzuri (mimi mtoto wa mkulima tu hata elimu yangu ni ya kuungaunga tu) ninaweza kuraise kidogo tu. Nimepita na NBC ikawa vilevile tu na mradi unakubalika na tatizo siaminiki tu kwa vile sina historia ya kushika pesa kubwa.

  Ninaweza kusimamia hii kazi na ikawa juu kiasi cha kuridhisha na kushindana na biashara kubwa tu hata kuanzisha zingine safi zaidi.

  Haya wadau naomba reference kwenye source au tujiunege na kuona nini cha kufanya. Nipo kwa wazi nasikiliza mawazo yenu na ushauri! unaweza kuchangia au kuniPM vyovyote utakavyoona

  Ahsanteni sana
   
 2. K

  Koba JF-Expert Member

  #2
  Sep 22, 2009
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 495
  Trophy Points: 180
  safi sana hata nchi zilizoendelea zimejengwa a watu kama nyie...jitahidi utafanikiwa tuu maana penye nia pana njia,mimi sina uwezo kwa sasa!
   
 3. O

  Ogah JF-Expert Member

  #3
  Sep 22, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Hebu mPM Mkuu Malila........atakupa malezo mazuri (experience ya vitu kama hivyo), kwani ni mjasiriamali mkubwa sana tu...........ngojanimtafute aje hapa amwage shule.......

  Ni mradi mzuri, je unaweza kuweka hapa hiyo business plan yako.....au waweza kuniPM ili kujua twaweza kujoin vipi nguvu..........
   
 4. Mzuzu

  Mzuzu JF-Expert Member

  #4
  Sep 22, 2009
  Joined: Jul 11, 2007
  Messages: 487
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  Ni page 40 hivi. Naendelea kuzishape zaidi... NtakuPM
   
 5. Triplets

  Triplets JF-Expert Member

  #5
  Sep 22, 2009
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 1,103
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  I'm proud of you countrymate,
   
 6. Chipukizi

  Chipukizi JF-Expert Member

  #6
  Sep 22, 2009
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 1,972
  Likes Received: 430
  Trophy Points: 180
  Salam,
  Ata mimi nipo katika kuanzisha mradi huohuo,na kuna wachina wanajenga viwanda vya cassava starch production dunia nzima na sasa wanajenga kimoja cha 150 tonnes per day Eddo state Nigeria.

  Wamenitumia full proposal ambayo ina bei na ata matumizi ya kiwanda kwa mwaka na mapato yake.

  kuna uncle wangu amenipa mabenki ambayo yapo tayari kufund icho kiwanda nimetembelea Mkuranga kule kuna umoja wa walima miogo (mohogo Saccos) hawa na Uongozi wa Wilaya(serikali) wapo tayari kuwa wabia.so tayari kumbe kuna groud ya kuifanya project ipatiwe funds.

  Mkuu wa wilaya ya Kisarawe pia amekubali kusaidia na kutoa land ya kiwanda soko la unga wa muhogo ata apa Tanzania lipo kubwa tu, jua ya kuwa tomato paste,chill,cone za baresa na sausege azitengenezwi bila muhogo.

  Let us meet and team up, tufanye pamoja mimi source ya funds ninazo.

  But at this time nna other 4 projects nazifanya so hii ya kasava ningependa kuifanya na mtu
  please let us meet
   
 7. Z

  Zamazamani JF-Expert Member

  #7
  Sep 22, 2009
  Joined: Jun 13, 2008
  Messages: 1,624
  Likes Received: 339
  Trophy Points: 180
  Jamani....hata mimi ni mjasiriamali katika fani ya kilimo....kwa sasa nina projevcts mbili za mpunga na vitunguu....proposals zake zimetulia na ni bankable....lakini tatizo kama kawaida ni security...hivyo kama kuna mdau tunaweza kuunganisha nguvu..hasa ktk suala la kutafuta fund sources na mengineyo......anakaribishwa.....nitashukuru
  zamani
   
 8. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #8
  Sep 23, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Proposal yako ni ya aina gani ya vituguu. Kuna vituguu vyeupe ndivyo vina bei nzuri soko la nje na hapa nchini pia. Vituguu hivi vinapendwa kwa sababu wakati wa kukata havitoi majimaji machungu yanayoumiza macho. Vinalimwa sana mikoa ya baridi ya Arusha na Kilimanjaro sielewi kwa maeneo ya joto kama vinastawi vizuri
   
 9. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #9
  Sep 23, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Mkuu
  watu wa Oxfarm wanatoa funds kwa projects kama yako. wameshafadhili na kuendeleza miradi kadhaa afrika hivyo usisite kuwatafuta.

  mimi nina knowledge ya fairtrade ambapo kama ukitaka tuition na contacts usiogope kuwasiliana.
   
 10. Mzuzu

  Mzuzu JF-Expert Member

  #10
  Sep 25, 2009
  Joined: Jul 11, 2007
  Messages: 487
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  Cheki mail yako kwa draft mkuu!
   
 11. Mzuzu

  Mzuzu JF-Expert Member

  #11
  Sep 25, 2009
  Joined: Jul 11, 2007
  Messages: 487
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  cheki pm mkuu!
   
 12. E

  Edo JF-Expert Member

  #12
  Sep 25, 2009
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 728
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Benki kuu ina huduma ya Export Guarantee Scheme na kuna orodha ya mabenki ambayo yanashiriki kwenye mpango huu. Nadhani miradi yote ambayo wadau mmeitaja hapa mwaweza kupata hiyo guarantee.
   
 13. Mzuzu

  Mzuzu JF-Expert Member

  #13
  Sep 25, 2009
  Joined: Jul 11, 2007
  Messages: 487
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  Mkuu Edo hiyo nafikiri ni ya kisiasa zaidi. Niliongea na maafisa wa NBC wakasema hiyo wenzio wanatumia kupatia maslahi yao kati ya miradi waliyopitasha haifiki hata 10% ilipewa guarantee. Akienda Mzindakaya atapata wengine mmh nq maamuzi yanaweza kuchukua hata miaka 2 hayajatolewa tena unaweza kupewa guarantee ya 40% tu. So unakuwa na wakat mgumu zaidi mkuu
   
 14. safariwafungo

  safariwafungo Senior Member

  #14
  Oct 1, 2009
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 136
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  I have been impressed by the idea of strenghten entrepreneurial tendency especially for graduates, as an intellectual i have also a project in the position to be funded. iko powa hiyo idea yako. Mimi ni entrepreneurial chemist nipo tayari kukusaidia so that we can move our country forward na kwa wale wengine wote wenye idea kama hizo please let contact with me via safariwafungo@yahoo.com
   
 15. Mzuzu

  Mzuzu JF-Expert Member

  #15
  Oct 18, 2009
  Joined: Jul 11, 2007
  Messages: 487
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  WanaJF mwenye mchango zaidi naomba asaidie kupanua mawazo yangu na wenzangu wanaojaribu kujiinua na hatimaye kuinua uchumi wetu jamani!

  Nashukuru kwa wote ambao tayari wamechangia na wengine tumewasiliana zaidi na kushauriana.
   
 16. B

  Bobby JF-Expert Member

  #16
  Oct 18, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,683
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  Mzuzu mimi pia ni mjasiriamali waweza kunipm and c how we can move forward together.I'm more than available for your idea which sounds fine nadhani.
   
 17. Shaycas

  Shaycas JF-Expert Member

  #17
  Oct 18, 2009
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 899
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  It's a good project if funded.
  Myself I have a plan to invest in social work. Proposal is ready seeking for fund.
  I prefer to start it in Dodoma,the fast growing town.
   
 18. P

  PUNJE JF-Expert Member

  #18
  Oct 18, 2009
  Joined: Jul 30, 2008
  Messages: 334
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 45
  ..................hongereni wanaJF kwa ushirikiano mnaounesha kila mara inapohitajika kufanya hivyo. Mungu awabariki
   
 19. M

  Mkandara Verified User

  #19
  Oct 19, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mzuzu,
  Mkuu wangu nashukuru sana kwa jitihada zako ambazo sii rahisi kuzipata toka kwa vijana wetu wa Kitanzania. Hakika soko la mhogo lipo ila kuweza kupata mashirika ambayo yapo tayari kumwaga mtaji inakuwa kazi ngumu kidogo isipokuwa mimi nafahamu Foundation moja ambayo hujishughulisha zaidi ya kilimo hasa nchi maskini...Ila wao wamejikita ktk kilimo cha Kahawa kwa sababu mwanzilishi wa foundation hii ana own mashirika makubwa ya kahawa ikiwa ni pamoja na shirika la uuzaji na migahawa lijulikanalo kwa jina la Tim Hotons.

  Jaribu kuwasiliana nao ila kama ingekuwa ni kahawa ningekwambia fanya kazi moja kubwa..kuwaunganisha wakulima wote wa Kahawa ktk eneno lako muunde chombo kimoja ambacho kitawakilisha mawazo ya wakulima wadogo wadogo halafu kwa kutumia jina la chombo hicho ndio wasiliana na viongozi wa Foundation hiyo..
  Hata hivyo, jaribu huwezi jua, pia inawweza kuwasaidia wanabodi wengine ambao watakuwa interested. Inaitwa Hanns R. Neumann Stiftung Foundation.
   
 20. Mzuzu

  Mzuzu JF-Expert Member

  #20
  Oct 19, 2009
  Joined: Jul 11, 2007
  Messages: 487
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  Nashukuru mkuu tutawasiliana
   
Loading...