Programu zinazokuongezea salio katika simu yako

Chrix_Tz

JF-Expert Member
Apr 15, 2015
880
1,098
Habari ya ijumaa.. Si vibaya tukazidi kupeana elimu kidogo huku tukiendelea kufurahia vema siku muhim leo ya duniani kote ya (BLACK FRIDAY).
Ningependa kukueleza jambo moja kuhusu matangazo ya biashara. Matangazo ya biashara kwa kiasi kikubwa ndiyo yanafanya internet izidi kupanuka. Wadau wengi wanaojihusisha na mitandao hutegemea hasa matangazo ili kujipatia kipato.

Baada ya kufahamu hayo basi naomba Chrix_Tz nikupe SIRI ya kuongeza salio bure katika simu yako kama unatumia smartphone. Kupitia Google Play Store, unakutana na programu nyingi zilizotengenezwa kwa shughuli maalumu kadha wa kadha. Hivyo ili uweze kupata salio bure unachohitaji kufanya ni

Download App hizo bure kutoka Google Play Store.Kisha tumia muda wako kutizama matangazo yao tu, haya huweza kuwa katika mfumo wa picha, sauti au video. Ukikata matangazo haya haupati hasara yoyote wao wanaridhika tu kujua kwamba ujumbe wao umekufikia.

Programu zinazokuongezea salio katika simu yako ni kama zifuatazo:


1. EUREKA

App hii hulipa kila mwisho wa mwezi katika mfumo wa salio la simu. Lakini pia kama ukinunua kifurushi utapewa discount kubwa.

2. SMARTPHONEMATE

Hii hailipi kutokana na matangazo. App hii imetengezwa na wataalamu wa upekuzi ambao nia yao ni kufahamu jinsi watu ulimwenguni wanavyotumia smartphone. Unachotakiwa kufanya kila siku angalau bonyeza batoni yoyote ile ilhali umeconnect internet basi nawe kila mwisho wa mwezi unalipwa salio kwa kusaidia kufanikisha zoezi hili.
3. LADOOO

Hii inakulipa ndani ya dakika tu endapo utadownload baadhi ya App nyingine ambazo wao wangependa uzi download, na ukishadownload zifungue hadi angalau zipite sekunde 10. Baada ya hapo unaweza kukata na kudownload nyingine kama watakavyokuelekeza. Ni njia bora zaidi kwani kama una kifurushi una download tu kisha una uninstall app hizo walizokuhitaji u download.

4. PAISA SWIPE

Hii huingia katika upande wa kulock screen au ku unlock. Badala ya kutumia pattern, au ku slide mshale, utapata kuona picha za matangazo mbalimbali wakati wa ku unlock. Hakikisha kabla ya ku unlock uwe umeconnectiwa mtandaoni.


Kama hauna smartphone au hata kama unayo, unaweza kuongeza salio kweli kabisa kwa kutembelea tovuti zifuatazo ambazo huwalipa watu katika mifumo mbalimbali ikiwemo salio.


WWW.ULTOO.COM

Hii inasapoti malipo kwa mitandao karibu yote. Unaweza kujipatia salio baada ya kujiunga na tovuti hii na ukawakaribisha (INVITE) marafiki zako wengine. Lakini zaidi kupitia njia ya kucheza na kutatua chemsha bongo kadhaa.

WWW.160BY2.COM

Hapa unaweza kujipatia salio kwa kuwaalika wenzako katika mtandao huu kwa kutuma SMS za bure. Pia kwa kutimiza baadhi ya majukumu mengine.


WWW.ANDYPLAY.COM

Tovuti hii takupatia magemu kama chemshabongo ambazo endapo utazikamilisha utaweza kujipatia salio..
unnamed.jpeg
 
Back
Top Bottom