Profiling Europe’s jihadists

Erijo

JF-Expert Member
Dec 28, 2015
453
379
20160409_woc890.png


Tambua nchi za ulaya zinazochangia kuongezeka kwa wapiganaji wa kudi la kigaidi la Islamic State.

Kumekuwa na ongezeko kubwa la wageni wengi kwenda kujiunga na kikundi cha kigaidi cha IS kilichopo Syria na Iraq, wengi wa wapiganaji wa wanaojiunga na IS kutoka ulaya, imelifanya bara hilo kupata changamoto kubwa za kiusalama.

Kwa mujibu wa taasisi ya kimataifa ya kupambana na vitendo vya kigaidi (International Centre for Counter-Terrorism) imeeleza kuwa idadi ya raia kutoka katika nchi za ulaya wanaojiunga na kikundi hicho cha kigaidi imeongezeka mara dufu, aidha taasisi hiyo imesema idadi hiyo imeongezeka mara mbili zaidi kwa kipindi cha miezi 18 na kufikia wapigaji 4,000 wanajiunga na IS kutoka barani ulaya.

Mbili ya tatu ya wapiganaji wanaojiunga watoka Belgium, Britain, France na Germany. Taasisi hiyo imeitaja Ufaransa kuwa inaongoza kwa kuchangia idadi kubwa ya wapiganaji wa jihadi wa kundi la IS huko Syria na Iraq.

Taarifa hii imekuja baada ya kushuhudia hatua kali zilizochukuliwa na nchi za ulaya hususani baada ya matukio ya kigaidi kukumba bara hilo, hii imezusha taaruki na kutishia usalama wa mataifa ya ulaya, wakati wakijianda kwenda Syria na Iraq kuteketeza magaidi wa IS, huku nyumbani kwao kuna kundi kubwa la vijana wanakwenda kujiunga na kundi hilo.

source: http://www.economist.com/blogs/grap...src=scn/li/te/bl/ed/profilingeuropesjihadists
 
Back
Top Bottom