Professor muhongo na sera ya umeme vijijini.

kanaku

Member
May 13, 2013
9
45
1. Serikali haina pesa za kulipa fidia kwa wale wote watakaoathiriwa na mradi wa umeme vijijni. 2. Watakaodai fidia itabidi wasubiri mpaka pesa ipatikane, hivyo tutaendelea na wale walioafiki kutodai fidia ili kuharakisha maendeleo. (29/12/2013 – Butima, Musoma) Huu ndio msimamo wa Serikali ambao umekuwa ukinukuliwa kupitia Professor wetu huyu aliyepewa dhamana ya kusimamia Nishati na Madini kwa kupitia wimbo wa kuharakisha maendeleo vijijini. Binafsi nautazama msimamo huwa kama udicteta wa serikali dhidi ya wanyonge ambao hautofautiani sana na Operation Kimbungailiyosababisha unyanyasaji wa hali ya juu na hata mauaji. Kuvunja nyumba ya mnyonge ya "tope yenye kuezekwa kwa nyasi" kule kijijini ili kupitisha umeme hakuna tofauti kimantiki na kuvunjwa kwa nyumba ghorofa ya Professor Muhongo iliyoko Masaki Dar es salaam ili kupisha ujenzi wa Barabara, je kwa mtazao huo professor anaweza kuwa tayari kutodai fidia kama anavyowataka wanyonge? Na tena wanyonge ambao kwa namna fulani hawana mbadala wa kuwa na nyumba nyingine mahala pengine kama inavyoweza kuwa kwa Professor na wengine wengi wa kada yake. Msimamo huu sio sawa kwa namna iwayo yoyote na hivyo serikali naishauri kuzingatia yafuatayo: a) Utaratibu ufanywe" kuassess" uharibifu, ili uharibifu ukubwa kulingana na vigezo vitakavyowekwa na vyombo huru kama mahakama kupitia wataalam wa masuala haya kufidiwa. b) Fidia ni kitu cha muhimu na haki kwa waathirika, serikali lazima ikubali kuwajibika hata kama ni kwa kutoa ahadi ya maandishi ya kufidia pindi tu pesa itakapopatikana ndani ya muda ulioainishwa bayana.
c) Serikali kuacha kutoa kauli zisizo na tija kwa wanyonge ukizingatia pesa nyingi ya walala hoi inafunjwa na viongozi waliopewa dhamana serikalini, huku wanyonge wakiendelea kuwa mashuhuda wa jinsi wanyonyonywa na wale waliowasomesha kwa kodi zao na hata kuwaamini kuwa chachu ya maendeleo yao.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom