Professor Frank Chiteji amefariki dunia. Tumetoka mbali pamoja.
Nilifahamiana naye kwa miaka mingi sana tangu mwishoni mwa miaka ya sabini alipokuwa mwanafunzi Michigan State University pamoja na Issa Kaboko Musoke, mwandishi wa habari Daily News na baadaye professor UDSM.
Chiteji na Musoke walikuwa roommates walipokuwa wanafunzi Michigan State nilipokwenda kuwatembelea miaka ile, na baadaye kumtembelea Haidari Amani (later also a professor, UDSM) ambaye pia alikuwa mwanafunzi pale.
Chiteji alianza kufanya kazi pale muda mfupi baada ya FRELIMO kuanzishwa Dar 1962. Mwaka 1963, alikuwa katika jitihada ya kujaribu kupata scholarship kwenda kusoma USA. Mwanzoni, aliwaambia Ubalozi wa Amerika kwamba hataki kwenda kusoma USSR ingawa baadaye alikwenda kule.