Bwana Erick hongera sana naona kazi ya TanV ipo vizuri.
Hebu niambie kutengeneza website km hiyo unacharge sh ngapi??
Je web inaweza kuwa na contents nyingi zaidi ya hapo?
Je kwa kumiliki website yangu naweza kupata mapato kwa watu kuitembelea??Je waweza kutoa mfano hapa wa kile mtu anachoweza kuingiza kwa idadi gani ya watumiaji wanaoitembelea.
Naomba kuwasilisha.
Sent using Jamii Forums mobile app
1. Hapo mwanzo nlikuwa nikicharge baada ya kazi kuisha ndiyo napiga mahesabu... lakini sasa ivi nimeamua kuweka packages ili kuweka urahisi kwa wote.
so, iko ivi:
- Local Businesses and Small Companies: Tsh. 340,000 ( inachukua siku 3 mpaka 7)
- Blog: Tsh. 380,000 ( Inachukua siku 5 mpaka 9 )
- Organizations and Institutions: Tsh. 460,000 ( inachukua siku 5 mpaka 11 )
- Ecommerce site: Tsh. 570,000 ( inachukua siku 10 mpaka 15 )
2. Website inaweza ikawa na content nyingi utakavyo wewe, tena inapendeza zaidi.
3. Ndiyo, unaweza ukaingiza kipato kwa watu kuitembelea tu.. kuna namna mbili.
a. Unaweza ukajiunga na Adsense, ambapo Google wataruhusu watu watumie website yako kutupia matangazo yako na kisha wanakulipa automatic, na kiasi unacholipwa wanaamua Google wenyewe.
b. Unaweza ukawa kama influencer endapo website yako itakuwa inatembelewa na watu wengi, kwamba ukaruhusu watu kuja kutangaza kwenye website yako, ila gharama unazipanga wewe mwenyewe.
4. Mfano.... Ntakupa mfano kwa Adsense makadirio yao, ila inabidi ufahamu kwamba hawaangalii idadi ya watumiaji wanaoitembelea..
- Wanaangalia ni mara ngapi page yako ya website imeangaliwa, hata kama unatembelewa na wastani watu 200 kwa mwezi, lakini wanaifungua page za website yako, zenye matangazo, mara tano kwa siku, basi itahesabika umetembelewa mara 1000 kwa siku, au mara 30,000 kwa mwezi..... Hivyo watakulipa kwa kuangalia ni mara ngapi ukurasa wa website yako umeangaliwa.
- pia wanatazama sana na website yako inajihusisha na nini, yani.. website inayohusika na mambo ya afya malipo yake ni tofauti na website inayohusika na mambo ya michezo.
- Vile vile na wanaangalia na Taifa unalotokea, malipo kwa wamarekani sio sawa na waafrika hata kama mnapata idadi sawa kwa mwezi, kwa sababu marekani watu wanauwezekano mkubwa wa kubonyeza hayo matangazo (Higher Conversion Rate) kuliko watu wa afrika.
- Google ads, wastani wanalipa %68 kwa mwenye website, yani mtu akilipia 100 kwa google ili atangaziwe biashara yake, basi 68 inakwenda kwa mwenye website, ambapo tangazo liliwekwa.
- kwa kawaida Adsense hulipa $0.10 mpaka $0.30 kila mara ukurasa wa website yako wenye matangazo utakapoangaliwa hata kama mtu huyo huyo akaufungua ukurasa huo mara tano. Lakini wastani ni $0.18 , kwahiyo kama ukurasa wako utatazamwa mara 30,000 kwa mwezi inamaana utalipwa, $5,400.