MALCOM LUMUMBA
JF-Expert Member
- Jul 26, 2012
- 21,033
- 64,840
Wasalaaam ndugu zangu,
Wale wakubwa shikamoo, wadogo marahaba.
Leo nimeamini ule usemi unaosema UGUMU WA MAISHA NI KIPIMO CHA AKILI.
Katika vyote cheza na woooote siyo mtoto wa kike.
Bwana kifupi leo Young Malcom nilipewa kazi ya kusimamia mitihani ya darasa la economics.
Ile kufika ndani ya darasa kumbe ni kubwa balaaa. Yani nafasi kati ya kiti na kiti unaweza kupita na bodaboda kwa spidi kali.
Maticha wakasema hawa wanafunzi ni mabingwa wa chabo leo tumewakomoa kabisa.
Kuna lizee moja liprofessa limejisifia sana limetunga mtihani mgumu na limewaweza wanafunzi kwa kuwapanga kwenye HALL kubwa vile.
Nikaitwa nikapewa somo kwamba ukikamata mtu anapiga chabo au kaingia na kipapai usimwache. Maaana wanafunzi wengi wamenipita umri na watanichukulia poa kama babu yao vile.
Wamenijaza gesi kama nusu saa hivi na mimi nikavimba kama pulizo hivi; nkasema astakhafulilahi leo sichekei mtu navaa uso wa kenge.
Ile nimeanza kugawa makaratasi kabla hawajaingia nkahakikisha pepa zimefunikwa mtu hasomi kitu. Nkawaruhusu waanze kuingia nikawapanga randomly tu.
Sasa bwana kuna mademu kama sita hivi wakaingia wamevaa mabaibui, huoni hata mkono ni uso tu. Nkasema hawa hata siwagusi kabisa isije ikaleta matatizo hapa, basi wakakaa vizuri bila bughundi.
Mtihani umeanza nimecheka sana watu wametoa mimacho wanatia huruma kweli na kunicheki mimi full uso kenge wala sionei mtu huruma.
Kuna maza moja ni in service halafu mnene kama pipa, ametoa jasho viganjani karatasi imelowa imekuwa kama OX-BOW LAKE.
Akijaribu kugeuka mimi nasogea nyuma yake kabisa.
Kuna jamaa jingine hilo ndiyo nikalikatamata infraglante delicto linabadilishana karatasi. Yani nikalitoa nje, limenitishia kweli kwamba ntakuharibia maisha bwana mdogo. Nikiliangalia kweli lile jamaa linaweza hata kuni Molest hili khaa. Domo jeusi na mimacho myekundu daaah.
Nikapiga moyo konde nikakazaa uso balaa nikatishia kuambatanisha pepa nipeleke kwa Dean of faculty. Nkachukua stapler machine nikaanza unganisha. Ghafla jamaa likaaza kulia mdogo wangu nihurumie kaka yako,oohooo nikajue kumbe lile biti lilikuwa zima moto tu.
Jamaa amelia sana,
Mimi nina watoto na familia na huu ndiyo mwaka wa mwisho.
Basi nkakaza sura; kimoyo moyo nkasema mabo si hayo mimi ndiyo David nimeua Goliati. Nkamwambia asubiri nje pale.
Ile kurudi klas,
Akaja examination officer kuleta vitambulisho fulani. Ile kuita majina dada moja akanyosha kumbe ni kati ya wale wenye baibui, jina lenyewe la Kikristo. Nkawaza sana, sasa wanafunzi walicheka mle darasani alivyonyoosha mkono. Nkajiuliza kunani hapa, bwana wee kumbe yule dada huwa havai Hijab wala nini.
Mle ndani ya baibui kaweka earphones na simu karekodi mavitu kibao kumbe anaminya kitufe tu anasikiliza nondo, yeye full kuandika tu.
Ile nimegundua nimesoma mchezo daah kumbe hata wanachat aisee.
Leo nikahakikisha ule msemo usicheze na Mtoto wa kike waweza kufa.
Hata kabla sijawakamata wkakusanya pepa wamemaliza mapema,
Ubaya kuna moja wao kanifuata kaniambia mwalimu Huwezi kuelewa ingredients zangu, utaishia kuelewa za keki tu.
Ilibidi mwishowe kuona hali ni mbaya nikibana sana kutakuwa na sifuri nyingi ikabidi nitoke tu nje ya darasa kuwaacha waigiliziane.
Na lile jamaa nikariruhusu lirudi dakika za 40 za mwisho,
Ujanja wote wa Arusha uliisha, likawa lipole balaa.
Ila funga kazi ni wale wadada sijapata kuona mimi tangu nazaliwa.
Mitihani ijayo natafuta mwalimu wa kike Muislamu anisaidie kuwakagua khaaaaaaaa.
Mhhhh sijapata ona.