Professa Tibaijuka ashtushwa na kasi ya ukuaji wa deni la taifa

Professa Tibaijuka ashtushwa na kasi ya ukuaji wa deni la taifa

Just Pray

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,142
Reaction score
4,779
" Je deni la Taifa ni himilivu kweli? Kuna vigezo viwili vya kuangalia. 1. Kwanza ni mtazamo wa mapato ya serikali yanayotumika kulipia Deni. Hapa tumelemewa kwani hadi Juni 2024, Tanzania ilitumia asilimia 44.3 ya mapato yake ya ndani kwa ajili ya kulipia deni la umma ikivuka kabisa kiwango cha juu kilichopendekezwa na IMF na Benki ya Dunia ambacho ni asilimia 18 kwa nchi zenye uwezo wa kati wa kubeba deni na hivyo kuathiri uwezo na uwekezaji wa serikali katika huduma muhimu kama elimu, afya na miundombinu.

Barabara nyingi ziko hali mbaya na Makandarasi wengi hawajalipwa na baadhi wamefirisika. Vijana waliojiajiri kama makandarasi hawawezi kuimarika ikiwa hawalipwi katika muda kwa huduma wanazotoa.

2. Kigezo cha pili ni Uwiano wa deni kwa Pato la Taifa (GDP).
Kufikia Juni 30, 2024, deni la taifa lilifikia Shilingi Trilioni 97.35, ongezeko la asilimia 18.36 kutoka mwaka uliopita. Na katika bajeti mpya limefikia Trilioni 107.

Hata hivyo, uwiano wa deni kwa Pato la Taifa (GDP) ulikuwa asilimia 30.8 – chini ya kiwango cha hatari cha asilimia 55 kinachotumiwa na IMF kwa nchi zenye uwezo wa kati wa kubeba deni.

Hii ina maana kuwa, kwa sasa, ukubwa wa deni ukilinganishwa na uchumi bado uko katika viwango vinavyokubalika na wakopeshaji hasa kwa maslahi yao.

Tathmini ya Hatari na Uendelevu wa Deni

Kwa mujibu wa uchambuzi wa pamoja wa IMF na Benki ya Dunia, Tanzania bado iko katika hatari ya kati ya kushindwa kulipa deni la nje (moderate risk of debt distress).

Ingawa uwiano wa deni kwa GDP uko chini, ongezeko kubwa la sehemu ya mapato ya serikali linalotumika kulipia deni linaashiria ongezeko la mzigo wa deni kwa muda mfupi.

Kiujumla ni kweli Tanzania bado ina nafasi ya kudhibiti deni lake kwa mujibu wa viwango vya kimataifa, hasa ikizingatiwa uwiano wa deni kwa GDP.

Uwazi, nidhamu ya bajeti, na ufuatiliaji wa matumizi ya fedha ni muhimu ili kuhakikisha uendelevu wa deni na kulinda huduma za msingi kwa wananchi na kuepuka kuwabebesha mzigo wa kodi na tozo za viwango vya juu ."Ameandika Prof. Anna Tibaijuka, Mtaalamu wa uchumi, Mwanasiasa, Mbunge na Waziri wa zamani wa Tanzania.
 
Tukisema sisi mnasema ni kawaida ok kasema professor
 
Kila siku tunadanganywa mashirika yanatoa magawio ya mabilioni, mapato ya makusanyo ya TRA yameongezeka kwa matrilioni, miradi yote tunatumia pesa za ndani.

Budget yetu 70% ni pesa za donor country.

Deni linaongezekaje, au tunakopa kufanya nini?
 
Adui wa mwanamke ni mwanamke, siku hizi kanawashwa kweli haka kenye macho kama senene
 
Mwigulu Nchemba anaogopa kudai kodi kisa ana nia ya kugombea urais hapo baadae
 
Back
Top Bottom