Profesa shivji huiamini rangi yako na kabila lako huko bara? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Profesa shivji huiamini rangi yako na kabila lako huko bara?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by jamhuri ya zanzibar, Aug 12, 2012.

 1. jamhuri ya zanzibar

  jamhuri ya zanzibar Senior Member

  #1
  Aug 12, 2012
  Joined: Jul 17, 2012
  Messages: 114
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Sikubaliani asilan na maneno ya Profesa Issa Shivji kuwa iwapo Muungano utavunjika Wazanzibari ndio watakaoathirika sana. Kwanza suala la Wazanzibari kuwa wako wengi wanafanya biashara Bara na kwamba ukivunjika Muungano watafukuzwa hivi ni vitisho vya watembea barabarani kuliko falsafa ya kiprofesa. Ukiangalia kwa kipimo cha ‘asilimia’ na sio idadi, basi wenye asili ya Tanganyika walioko Zanzibar ni wengi zaidi kuliko wenye asili ya Zanzibar walioko Tanganyika.

  Biashara leo duniani imeunganishwa na mfumo wa utandawazi kuliko siasa na ndio maana Wakongo, Warwanda, Wazambia, Wangazija, Wachina nk. wako wengi Tanganyika na wala hakuna Muungano kati ya nchi watokazo na Tanganyika. Watu wanapofanya biashara hujinufaisha wao wenyewe pamoja na kunufaisha uchumi wa nchi wanayofanya biashara na ndio maana nchi zetu bila kuogopa kutawaliwa tena zinazialika nchi zote duania kuja kufanya biashara.

  Kama itatokea Muungano uvunjike na Wazanzibari wafukuzwe Bara huu ni umbogo wa kisiasa ambao naamini Bara hawawezi kuufanya kutokana na hadhi waliojiwekea duniani kwa kuheshimu haki za binadamu na amani. Ndio maana nchi hili ilikubali hata kuwapa hifadhi wakimbizi wa nchi nyengine na leo wanatafutiwa uraia pamoja na kwamba nchi zao hazina tena kadhia zilizowakimbiza.

  Hapa hapana tena nafasi wa kuwaelimisha Wazanzibari kuhusu historia ya Muungano na faida zake kwani wasiojuwa historia ya Muungano kama mimi basi wana uzoefu wa kutosha wa faida na hasara za Muungano kwani ndio wanaishi ndani ya Muungano wenyewe. Leo kwa mfano ushuru wa forodha ulisawazishwa kwa matakwa ya Tanganyika na Wafadhili na ikaundwa Mamlaka ya Mapato ya Tanzana (TRA) na Ofisi ya Zanzibar inaongozwa na Msaidizi Kamishna na wafanyakazi wote wanaajiriwa na Muungano na wanalipwa mshahara na Muungano na wanapangiwa kazi na Muungano.

  Sheria ya forodha ya nchini na kimataifa inasema mzigo ukiingizwa katika bandari yoyote ya nchi utachukuliwa umeingia nchini. Kama Tanzania ni nchi moja kwa Profesa ulivyotusomesha, inakuwaje leo mizigo ikilipiwa ushuru Zanzibar na ikipelekwa Bara inazuiwa na kutakiwa kulipiwa ushuru upya kama haujaingia nchini?

  Hivi sasa kuna magari zaidi ya 400 kutoka Zanzibar iyamezuiwa Bara na maofisa tu Serikali! Huu ni ushahidi kuwa mazingiza ya nchi zetu hayaruhusu kuwa na mfumo wa uendeshaji wa pomoja lakini yanaruhusu kuwa na mfumo mashirikiano tu kihaki.

  Kusema kuwa kuwe na Rais mmoja na Waziri Mkuu mmoja na kutoka pande mbili ndio kuimeza Zanzibar kinyemela na sikutarajia Profesa alietokea Zanzibar angependekeza uhusuda huu wa wazi. Profesa aliebobea kwa sheria na historia atakumbuka kuwa Mwenye Kigoda aliwahi kuwaita Kenya Nyanga’u.

  Hii ndio sehemu ya historia wasioijuwa wengi wetu na anayo nafasi nzuri ya kuwasomesha Watanzania. Leo tuko tayari kuzichapa na Malawi kwa Ziwa tu lakini hatuoni umuhimu wa Bahari na ardhi ya Zanzibar. Kama wanaotaka kuvunjika kwa Muungano wana tamaa za kibinafsi, na wale wanaotaka Zanzibar itoweke basi wanatamaa kubwa zaidi kwani wanataka kuhakikisha kuwa Zanzibar inamaliza historia yake, utamaduni wake na dini zake.

  Hii ndio tamaa mbaya zaidi duniani kuliko ya suala la kibiashara alilolielezea Profesa Shivji. Mimi si miongoni mwa wanaotaka kuvunjika Muungano na hakuna mwanasiasa aliyewahi kutoa maoni kuuvunja Muungano hadi sasa, lakini tunachotaka ni Muungano utakaowapa uhuru wananchi wa pande mbili kujiamulia mambo yao ya kiuchumi na kijamii na yale yanayowatia khofu watu duniani yaani ya kuchafuka AMANI yapakie katika Muungano kwani sote tunataka tuishi kiusalama.

  Naamini Profesa kwa kushauri Serikali moja ndio hasa anafanya kazi iliyoachwa na Nyerere na pengine ndio maana akakabidhiwa KIGODA. Profesa anashangaza kuonekana kwamba pamoja na elimu yake kubwa hakukomboka kimawazo. Bado ni mtumwa wa mawazo ya Nyerere. Wasiwasi wangu ni kwamba anadhani kwa sababu ya rangi na kabila yake, usomi wake utapata heshima kwa njia pekee ya kuwa mtumwa wa mawazo ya Nyerere. Shivji anafahamu fika kuwa wazanzibari adui yetu namba moja ni Nyerere. Hata katika kitabu chake cha “Pan Africanism or Pragmatism? Lessons from Tanganyika and Zanzibar Union” Professa Shivji amemnukuu Nyerere wazi wazi akionyesha nia yake mbaya sana kwa Zanzibar mapema kabla hata ya muungano wenyewe kwa kusema “ningekuwa na uwezo ningevididimiza viziwa vya Zanzibar katika bahari ya hindi”. Sisi wazanzibari tunaamini kuvididimiza katika bahari ya hindi hakuweza lakini angalau kuvipoteza katika ramani ya dunia amefanikiwa. Profesa ajuwe ni Mwalimu alietufikisha katika mtafaruku huu ambao hatuko tayari tena kuuendeleza. Professa wazanzibari tunakuheshimu sana, hatupendi tukuingize katika orodha ya maadui zetu. Na kwa hili ni vyema utuombe radhi.

  Tunampongeza na kumshukuru sana mwenyekiti wa baraza la katiba la Zanzibar Profesa Abdul Sherrif na jopo zima la baraza lake kwa kuja na kitu kipya cha Muungano wa MKATABA. Huyu ndie Profesa na msomi mwenye uchungu kwa Zanzibar. Kwa sababu ni mzanzibari. Hatushangai Shivji kusaidia kutukandamiza maana Zanzibar haimuhusu. Kabla ya kuja kwa wazo la muungano wa MKATABA wazanzibari tulikuwa tumeganda katika mifumo ya muungano iliyomo katika sera za vyama vya siasa ambapo mifumo yote haikuonekana kuwa na jawabu ya kudumu ya kero za muungano huu.

  Tunamwambia tena Shivji na Zanzibar Maprofesa wapo na awzoefu kuliko yeye na wenye kuheshimika ulimwengu mzima. Tumeshaamua muungano wa MKATABA hayo ndio maamuzi ya wazanzibari, vinginevyo tutaona wakati ukiwadia. Haitakuwa Zanzibar peke yake kuingia katika muungano wa namna hii ipo mingi tu duniani. Na bila shaka ndio miungano yenye nguvu.

  Jamhuri ya watu wa Zanzibar kwanza.
   

  Attached Files:

 2. d

  dandabo JF-Expert Member

  #2
  Aug 12, 2012
  Joined: Feb 18, 2012
  Messages: 303
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 45
  usijifariji na wakenya na wachina walio nchini kwa amani ukadhani itakua ivyo ivyo kwa wazenji kama muungano utavunjika. Nakuhakikishia tutaishia kuwa mahasimu na si marafiki tena!
   
 3. Kabembe

  Kabembe JF-Expert Member

  #3
  Aug 12, 2012
  Joined: Feb 11, 2009
  Messages: 2,236
  Likes Received: 928
  Trophy Points: 280
  Ndugu Jamhuri ya zanzibar profesa Shivji hasingeyasema hayo yaliyokukera wala sisi wengine tusingeyajua hayo ya moyoni mwako,na maadamu huu ni wakati wa wataanzania kujadiliana na kuuamua mustakbari wa nchi zao basi hoja ya profesa Shivji ina tija kwani huu ndio wakati wake muafaka wa hoja chokonozi.
   
 4. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #4
  Aug 12, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,104
  Likes Received: 551
  Trophy Points: 280
  unajua kwamba kuna wazanzibar kibao kwenye taasisi za tanganyika? Unadhani wataachwa kama wafanyabiashara wa kichina? Vunjeni muungano muone, tutawafukuza wazi wazi
   
 5. Opaque

  Opaque JF-Expert Member

  #5
  Aug 12, 2012
  Joined: Oct 24, 2008
  Messages: 1,138
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Daah, likishafikia suala la kufukuzwa Bara basi wazanzibari mnakuwa mmekamatwa pabaya, mnatoa lugha ya kuisifia Tanganyika kuwa ni nchi yenye upendo na kadhalika. Mbona lisipozungumziwa hilo mnatutukana? Hakuna asiye raia anayeruhusiwa kufanya biashara bila kulipia vibali vya wageni, na wala hakuna asiye raia anayeruhusiwa kumiliki ardhi ndani ya nchi nyingine. Jiandaeni kisaikolojia kwa yatakayofuata, hakuna kutoa lugha ya kuisifia Tanganyika hapa!
   
 6. peri

  peri JF-Expert Member

  #6
  Aug 12, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,588
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  hakuna mzanzibari atakae fukuzwa bara hata mmoja, kama nikufukuza inabidi tuanze na wachina na wakenya manake hawa hatuna muuongano nao wala hatujawahi kuwa nao.
   
 7. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #7
  Aug 12, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,588
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Swala la rangi limeingiaje hapa???
   
 8. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #8
  Aug 12, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,946
  Likes Received: 1,271
  Trophy Points: 280
  Muungano ukivunjika wooote wanaomiliki ardhi watatuachia! Usianze kutusifia kijinga. Na mmejijaza kama miviazi huku bara. Si muanze na kina Hamad Rashid, Mabumba n.k. ili watoke bungeni na kurudi kwenye 'kawilaya' kenu
   
 9. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #9
  Aug 12, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,946
  Likes Received: 1,271
  Trophy Points: 280
  acha ujinga wewe

  jidanganye
   
 10. Tuyuku

  Tuyuku JF-Expert Member

  #10
  Aug 12, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 3,149
  Likes Received: 1,405
  Trophy Points: 280
  Wazanzibar shauri yenu. Msije sema hatukuwakanya!
   
 11. jamhuri ya zanzibar

  jamhuri ya zanzibar Senior Member

  #11
  Aug 12, 2012
  Joined: Jul 17, 2012
  Messages: 114
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mimi naamini hafukuzwi mzanzibari Tanganyika na hata akifukuzwa ni kutia maji katika pakacha maana huku Zanzibar pia watanganyika wamejaaaaaaaa kibaooooooooooo, lkn sisi hatutawafukuza maana wengi wamekuja kutafuta vibarua tokea muungano haujafikiriwa. Tutaishi nao tu. Hao watakaofukuzwa bara ndio waliomstari wa mbele kudai Zanzibar yao. Maana nchi yao itakuwa na fursa za kutosha na nguvu za kiuchumi jambo ambalo litawaondoshea sababu ya kuwekeza ugenini. Mimi naamini sio tu wako Tnganyika kwa sababu ya muungano unaruhusu lkn pia muungano umeiba nguvu za kiuchumi za Zanzibar na kuzipeleka Tanganyika kwa maana hii wamefuata fursa zilizotoroshwa.
   
 12. simplemind

  simplemind JF-Expert Member

  #12
  Aug 12, 2012
  Joined: Apr 10, 2009
  Messages: 11,800
  Likes Received: 2,571
  Trophy Points: 280
  kama unatupenda
  tununulie zeze
  tukilipiga Zanzibari
  hadi maziwa makuu
  wanacheza.
   
 13. king kan

  king kan JF-Expert Member

  #13
  Aug 12, 2012
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 1,264
  Likes Received: 715
  Trophy Points: 280
  Tatizo la Wazanzibar ni wanafiki kupita maelezo. Hamuelewi kila akitokea profesa au mtu mashuhuri akaja mnafuata mawazo yake bila kwanza kufikiri. Tulipowakomboa kutoka kwa sultani na Waarabu wapo waliopendekeza tuwe serikali moja ikiwamo hao waanzilishi wa Baraza la Mapinduzi, Mwl. Nyerere akakataa(alihofu tungewameza) hapo wote wakamsifu mwalimu angalau wakawa wafuasi wake kwa muda. Baadae baharia akaanza vitimbi anataka kutoka ndoani akapata wafuasi, alipopotezwa
  akaibuka Jumbe na kura ya maoni mkamuunga mkono, alivyoitwa na chama mkamsulubu. Bwana Mwinyi alipopewa urais bara mbembwe zenu zikatulia, muungano ukawa poa kwa muda, walivyoibuka G55 na Mwinyi wenu pamoja nanyi mkawa hamuelewi. Salmin akaja na issue yake ya oac na mengine, ccm walipompunch chini J. k. N vilaza wote wakamkimbia. Maalim na Jussa walipowamobile mlikuwa tayari kuuana, kamanda Maalim alipowafanya Pemba wamezwe na unguja hakuna aliyekumbuka msimamo wao wa zamani. Sasa wamewasahau akina maalimu na sera yao ya serikali tatu na urais wa zamu sio wa vigezo wamekuja akina Ahmed Rajab wametoa lecture ya muungano wa mkataba Wazanzibar wamewafuata, najua atatokea kilaza atawataka mjitenge na muungano mtakubali. Du kweli nyie kama tiala hufuata direction ya muongozaji. Nyie kweli wanafiki.
   
 14. S

  SPANERBOY UDZUNGWA JF-Expert Member

  #14
  Aug 12, 2012
  Joined: Jun 20, 2012
  Messages: 623
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Kama na wewe ni mzenji unatakiwa ujue ni lazima tuwafukuze
   
 15. mwakajila

  mwakajila Senior Member

  #15
  Aug 12, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 188
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kwenye ushuru wa forodha hapo kuna issue kidogo kinachotokea ni officers wanaconfirm ushuru uliolipwa ni sahihi kama umelipa kodi ndogo basi unatakiwa ulipe the difference hiyo ni kuweka usawa wa malipo ya kodi kwa gari zinazotoka zanzibar na zinazopitia bandari ya dar..
   
 16. y

  yaya JF-Expert Member

  #16
  Aug 12, 2012
  Joined: Jun 29, 2011
  Messages: 694
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu, umeongea au niseme umeandika kama vile mtu ambaye hata shule hajawahi kukanyaga, ambako angeweza hata kujua kwamba kuna kitu kinachoitwa sheria ya uhamiaji, wachilia mbali sheria za uwekezaji.

  Hivi unadhani huo muungano wa Tanganyika na Zanzibar ukifa hao wa-Zenji walioko Tz-bara wataendelea kufaidi wanachokifaidi sasa?
  Kwa taarifa yako wataanza kuomba vibali vya ukaazi na uwekezaji kwa wale wenye biashara kubwa. Na kama unavyojua katika maombi siku zote huwa kuna ndiyo na hapana tu na si zidi ya hayo majibu mawili.

  Jaribu kupima hayo maneno machache niliyokwambia ndipo utakapojua kwamba Profesa Shivji ni mwalimu wa chuo kikuu aliyebobea au ni wa chekechea?

  Msijidanganye kwa kujipa moyo kwamba every thing's gonna be ok.
   
 17. B

  Bangoo JF-Expert Member

  #17
  Aug 12, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 5,594
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Tuko tayari kwenda vitani kutetea sehemu ya Tanganyika (zanzibar)
   
Loading...