Profesa Mwandosya na Dr. Mwakyembe hawapikiki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Profesa Mwandosya na Dr. Mwakyembe hawapikiki

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ntambaswala, Jul 25, 2011.

 1. N

  Ntambaswala JF-Expert Member

  #1
  Jul 25, 2011
  Joined: Dec 7, 2008
  Messages: 255
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Kuelekea uchaguzi kwa 2015, habari za kuaminika kutoka vyanzo visivyopenda kujulikana zinadai kuwa hawa jamaa sasa hivi hawaivi chungu kimoja. Ingawa mwaka 2005 walikuwa pamoja, inaaminika kuwa sasa kila mtu yuko kivyake hasa kwa vile Dr. Mwakyembe naye ni malighafi ya urais

  Pia inaaminika sasa hivi JK anaelewana vizuri na Profesa Mwandosya kwani aliyekuwa hasa anawatenganisha kabla( ukiacha ugomvi wao wa zamani) ni Edward Lowasa ambaye inasemekana anaelekea kumalizwa nguvu zake ndani ya CCM na serikali.

  Kitendo cha Profesa kuwa karibu na JK kinaonyesha kuwa angalau sasa Profesa anaweza kuwa na sapoti fulani toka kwa JK kama ataamua kugombea. Kitendo hicho hakijawafurahisha Sitta na Dr. Mwakyembe ambao wanaona mmoja kati yao ndio anafaa kuwa mgombea urais 2015.

  Pia kitendo cha Mpendazoe kuwaumbua Dr Mwakyembe, Sitta na Nape kuwa ni miongoni mwa waanzilishi wa CCJ kimewapunguzia sana umaarufu ndani ya chama, huku Profesa akiwa hajapata msukosuko wowote wa kisiasa.

  Hata hivyo tofauti na Profesa, Dr. Mwakyembe anauzika kwa urahisi na hata chama cha wazee wa kuandamana wanamkubali sana Dr. Mwakyembe tofauti na Profesa ambaye hakubaliki kabisa hata na CUF au NCCR Mageuzi.


  .
   
 2. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #2
  Jul 25, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Hivi bado tunamhitaji Mwandosya kwa ajili ya urais? Hivi vibabu sasa vipumzike bwana. Matokeo ya kuchagua hawa wazee ndiyo kama haya ya akina JK, akili ilishachoka kufikiria, anashindwa kufanya mambo ya maana yenye faida kwa taifa. Aende zake huko tunataka fresh blood sasa.
   
 3. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #3
  Jul 25, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Hakuna anayefaa kuwa raisi hapo

  Mwandosya ni Mgonjwa jamani lol.....Mwakyembe inatakiwa ajivue gamba hatutaki raisi fisadi, huyu ana ile scandal ya posho mara 3. Wapishe mwingine atakaye kuwa na uchungu na nchi.
   
 4. N

  Ntambaswala JF-Expert Member

  #4
  Jul 25, 2011
  Joined: Dec 7, 2008
  Messages: 255
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Mwalimu Nyerere aliwahi kumwambia kiongozi mmoja mwandamizi wa CCM kuwa- wewe hujawahi kufanya jambo zuri wala jambo baya kwahiyo hufai kuwa kiongozi ...............................

  Kumbe ili uwe kiongozi lazima uwe unaweza kufanya jambo baya au zuri..............kufanya maamuzi mazuri au mabaya

  Dr. Mwakyembe alisimamia tume ya Richmondi ingawa naye ni muoga maana angeamua kukomaa na kujitoa CCM akaenda upinzani angekuwa yuko juu sana hivi sasa. Kitendo cha kukubali uwaziri mdogo kimemshusha chati sawa na swahiba wake Sitta

  Profesa nasikia aliwahi kuacha kazi kuepusha kuharibu weledi wake ila naona anakosa ile sauti ya utawala ambayo inaweza kuwaaminisha wananchi kuwa akiingia Ikulu atavunja mikataba yote ya madini, Loliondo n.k
   
 5. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #5
  Jul 25, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Nani kajaribu kuwapika?
   
 6. UmkhontoweSizwe

  UmkhontoweSizwe JF-Expert Member

  #6
  Jul 25, 2011
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 2,971
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Nani mwenye uchungu na nchi ndani ya CCM ??
   
 7. N

  Ntambaswala JF-Expert Member

  #7
  Jul 25, 2011
  Joined: Dec 7, 2008
  Messages: 255
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Arafat,
  Swali zuri sana, nasikia wazee wa huko kwao waliwaita kuwauliza nani kati yao anajiandaa kugombea urais. Lengo ilikuwa ni kwa wazee kuwa na focus na mtu mmoja na kuelekeza rasilimali adimu kwa mtu mmoja. Nasikia hakuna muafaka uliopatikana maana kila mtu anataka kuwa mgombea
   
 8. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #8
  Jul 25, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,566
  Likes Received: 18,529
  Trophy Points: 280
  Ntambaswala,
  Kwa maoni yangu, hizi ni siasa za Mbeya tuu, hakuna ubaya kuwa na 'wishfull thinking' hata kama ni empty hopes. Hebu mfikirie JK na umaarufu aliokuwa nao 2005 na jinsi alivyoshinda kwa kishindo kwa over 80%, halafu fikiria kilichompata JK kwenye uchaguzi wa 2010 na ujio wa Dr. Slaa kwenye mbio hizo, JK licha ya kuwa ni sitting president, akigombea kiti alichokikalia with all the support ya presidential institution, halafu CCM ndio chama tawala, ukijumlisha mbinu zote walizotumia, safi na chafu, plus support ya Tume pendeleo ya uchaguzi kuwasaidia, bado ushindi wa JK ulipururuka mpaka 40%!, hivyo mgombea wa CCM wa 2015, lazima awe ni mtu atakayeweza kumkabili Dr. Slaa, kitu ambacho si Prof. Mwandosya, wala Dr. Mwakiembe ana fit, unless otherwise kama CCM kupitia state machinery yake, watafanikiwa kum contain Dr. Slaa before 2015!.

  Nashauri wale washabiki wa siasa za Mbeya, kwenye urais, bora msahau, the sooner the better, ili msijeishia kujihuzunikia bure.

  Nakumbushia kwa msisitizo, kuna makabila fulani, uraisi ni BIG NO!
   
 9. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #9
  Jul 25, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Mkuu watakuwepo wachache! ila huko duuu niwakutafuta sana
   
 10. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #10
  Jul 25, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  No comment mpaka nipate zile za kiinteligencia maana ni kama umeamua kuangalia upepo uanaelekea wapi ndo ukatunga iyo
  CU bidae
   
 11. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #11
  Jul 25, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Tungekuwa bar ningesema mpatieni huyu jamaa crate kwa bill yangu.

  Uraisi 2015 ni shughuli pevu Tanzania tegemea sarakasi za aina zote
   
 12. Maarko

  Maarko JF-Expert Member

  #12
  Jul 25, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,030
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  CCM wanaweza wakaendelea kuongoza dola kama watampendekeza Sitta kugombea urais 2015,ila wakiteua mwingine yeyote CDM njia nyeupe pee.
   
 13. Mwamikili

  Mwamikili JF-Expert Member

  #13
  Jul 25, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 416
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  kaka hayo ni majungu tu badili mada iwe nani anafaa kuwa rais kati ya mwakyembe na mwandosya sio hawapikiki chungu kimoja, EL is the president of 2015 or membe kama hutaki jinyonge
   
 14. N

  Ntambaswala JF-Expert Member

  #14
  Jul 25, 2011
  Joined: Dec 7, 2008
  Messages: 255
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35

  Pasco,
  Umepigilia msumari hasa, uliyosema ni kweli kabisa. Na mimi naona kweli hizo ni wishful thinking kwa watu wa Mbeya kutaka kutoa rais. Ila mke wangu hajapendezwa kabisa na post yako maana anaamini kaka yake (shemeji yangu) -Dr Mwakyembe ndo atakuwa mgombea wa urais 2015, iwe kupitia magwanda au magamba
   
 15. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #15
  Jul 25, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,673
  Trophy Points: 280
  Imefikia mahali leo tunajadili uraisi wa 2015 wakati tuna changamoto nyingi namna hii?Shame on us!
   
 16. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #16
  Jul 25, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,673
  Trophy Points: 280
  Nani amekudanganya?
   
 17. Watu

  Watu JF-Expert Member

  #17
  Jul 25, 2011
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 3,054
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Mwandosya afya mgogoro, mwombe kwanza arudi kabla hujamwombea awepo 2015
   
 18. The Dreamer

  The Dreamer JF-Expert Member

  #18
  Jul 25, 2011
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tehe tehe tehe!!! Wapikwe wamekuwa ndizi bana? Najua unajua so you just made me laugh!
   
 19. The Dreamer

  The Dreamer JF-Expert Member

  #19
  Jul 25, 2011
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hakuna hata jina moja ulilotaja laweza kupitishwa. Nasikia Naodha au mwanamama wa UN anaweza kuwa mgombea wa chama cha magamba
   
 20. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #20
  Jul 25, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,695
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  You've spoken well ndugu, hii nchi imekuwa na watu ambao ni obsessed na uongozi. Hata mwaka haujaisha tangu uchaguzi uliopita, sisi tunawaza rais ajae.
   
Loading...