- Atahutubia mikutano ya wasomi duniani
- Vijiji 1,500 nchini kuwa na umeme Aprili 30
Mkutano huo ujulikanao kama World Economic Forum unafanyika jijini Davos nchini humo.
Aidha kutoka nchini Uswisi, Profesa Muhongo ataelekea nchini Marekani alikoalikwa na Sserikali ya nchi hiyo kwenye mkutano mkubwa unaojadili masuala ya nishati ambapo yeye atakuwa mmoja wa watoa mada.
Akitoka nchini Marekani, Profesa Muhongo ataelekea nchini Italia ambako pia amealikwa kama mmoja wa wataalamu duniani.
Wakati mataifa makubwa yakipigana vikumbo kuwasilisha mialiko kwa Profesa Sospeter kwa kuthamini na kuheshimu utalaamu wake, wanasiasa na wafanyabiashara hapa nchini wameendelea kupuuza utaalamu huo na kuwalaghai watanzania.