Profesa Malima: Kwanini nimejitoa CCM

Sep 19, 2019
43
383
KUTOKA MAKTABA KUU

Feb: 15, 2022.

Na Sheikh Ponda Issa Ponda

HOTUBA YA RAIS SAMIA NA PROFESA MALIMA

“Kuna makundi wanayoyafanya ndani ya serikali wanayajua. Makundi hayo yanageuka na kusema Serikali ya awamu ya sita ufisadi umerudi, mambo yako ovyo, kumbe wao ndio wako ovyo. Mambo hayo (ya ufisadi) hayakufanyika ndani ya awamu ya sita bali yamefanyika huko nyuma, lakini gari bovu linaangushiwa awamu ya sita. Sitakubali”.

Hayo ni sehemu ya hotuba ya Rais Samia Suluhu Hassan ya tarehe 5 Desemba 2021, akitupa lawama ndani ya serikali ya CCM.

Tabia hiyo ya kusukumiziana gari bovu imejengwa na kudumu katika chama na serikali hiyo kwa muda mrefu. Hotuba ifuatayo ya Profesa Kigoma Ali Malima ya tarehe 16 Julai 1995, katika mkutano wa hadhara Tabora baada ya kujitoa CCM na serikalini na kujiunga Upinzani, imebeba malalamiko kama hayo:

“Ndugu wananchi, miaka 38, iliyopita niliamua kuingia katika chama cha TANU ili kupigania uhuru wa nchi yetu. Wakati huo nilikuwa kijana mwenye umrii wa miaka 20, nikisoma shule ya wavulana ya Tabora. Niiliamua hivyo baada ya kuona hamna maana ya kuendelea na masomo wakati wanchi wandhalilishwa na Wakoloni.

Kwakuwa jambo hilo lilinikereketa mno, ndiyo nikaamua nijiunge na chama kile miaka 38, iliyopita. Niliacha shule nikajiunga na watanganyika wenzangu kudai uhuru nikazunguuka nchi hii kwa mapana na marefu.

Uamuzi huo niliufanya nikiwa hapa Tabora na ulikuwa uamuzi wa kihistoria kiasi kwamba rafiki zangu waliniambia kwanini usiendelee na masomo tukamaliza kwanza? Nikawajibu nyie endeleeni tutakutana baadae. Na tulikutana kweli. Mimi nikaenda kupigania uhuru (wao wakaendelea na masomo).

La msingi ninalotaka kusema hapa leo hii, ni kwamba hivi karibuni niliamua kujitoa CCM na kujiunga na chama kipya cha NRA. Nawaombeni na nyinyi ndugu zangu mliopo hapa tufanye hivyo, tujiunge na chama hiki wote kwa pamoja.

Uamuzi huo utatuwezesha kutenda na kusimamia utekelezaji wa haki na usawa kwa wote kwa dhati. Utawala wa CCM, unazungumza usawa halafu unajenga matabaka ya wenye nchi na wanaodhalilishwa. Huo ni usawa wa hadaa.

Nilipofanya uamuzi huu mgumu, wazushi walisema eti nitakuja huku (Tabora) kutangaza rasmi, kujitoa CCM, lakini nitafanya hivyo kwenye swala ya ijumaa Msikitini. Eti ninakuja kutangaza kugombea urais wa taifa letu Msikitini. Mimi nimekaa kwenye siasa miaka 38, ni kweli sijui kwamba jambo hilo halifanywi Msikitini?

Na watu hao wenye madaraka wakafanya kila njia kunizuia nisifike Tabora mapema ati, ili nisiwahi swala ya ijumaa (nikatangaza uamuzi huo wakati wa swala). Yaani wamefikia kiasi hicho. Uvumi ukaenezwa na kasheshe ikatokea Msikitini. Askari wakajazwa Msikitini baada ya uzushi huo kwamba, Profesa Malima anakuja kutangaza kujitoa CCM Msikitini.

Yote hayo ni kutaka kuonyesha kwamba mimi “ni mdini”, sijui Muislam mwenye siasa kali na majina mengine wanayoyatumia dhidi yangu. Wakati fulani, gazeti moja likazusha nimejenga Msikiti katika wizara. Sasa nimetoka katika mawizara hayo wakatazame kama kuna Msikiti nilioujenga huko. Lakini hakuna hata kiongozi mmoja wa CCM wala wa serikali aliyesimama kunitetea (akasema huo ni uzushi), au kuliambia gazeti hilo likapige picha huo Msikiti watu wauone.

Bali walikua wanasema, mwacheni akione. Sasa mimi niwaelewe vipi? Mbona viongozi wengine wakipatwa na matatizo wanawatetea? Gazeti na heshima yake linasema uongo.

Nilipofika Wizarani hapakuwa na choo cha ndani. Waziri anakaa ofisi ambayo, choo kipo kama kule kwenye mwembe ule! Ukishikwa na tumbo watu wote wanajua mzee leo kakwama. Mimi naujua ustaarabu, nilichofanya nilipofika pale nikamwita Mhandisi ashughulikie hilo kikajengwa choo.

Eti huo ndio Msikiti na watu wenye akili zao wakaamini jambo hilo. Nimewapeleka watu hao Mahakamani ingawa kesi ya nyani ukipeleka kwa ngedere ni kazi bure. Sasa ni mwaka wa nne kesi haijasikilizwa. Naona bilashaka wanatafuta Jaji asiyenifahamu. (Hotuba hii muhimu iataendelea kesho).
 
Back
Top Bottom