Profesa Makame Mbarawa amemteua Bwana Masanja Kungu Kadogosa kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu (TRL)

R.B

JF-Expert Member
May 10, 2012
6,296
2,575
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amemteua Bwana Masanja Kungu Kadogosa kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRL), ambako anakwenda kuchukua nafasi ya Mhandisi Elias Mshana ambaye anastaafu hivi karibuni.

Kabla ya Uteuzi huo Bwana Masanja Kadogosa alikuwa Mkurugenzi Idara ya Mikopo Benki ya Rasilimali Tanzania (TIB). Uteuzi huo unaanza mara moja.

Imetolewa na;

Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.

02 Februari, 2016
 
Ni muhimu uteuzi ufanyike kwa kuzingatia ujuzi na weledi na siyo dini, kabila, ukanda au kujuana. Hapa ni kazi tu!!
 
Cha msingi awe mbunifu afufue shirika hili muhimu! Akiweza kuwekeza kwenye reli bila mizengwe treni za abiria na mizigo kwenda Mpanda, Singida, Arusha na Kilombero zitakuwepo.

Reli ya standard gauge baadae! Hii ya zamani ifufuke kwanza wananchi wapate unafuu wa kusafiri na kusafirisha mizigo yao. Na hapo hapo barabara zetu zitadumu.
 
Afadhali wasukuma tumekumbukwa, tunawaacha wakwere na Ngoma zao, wachaga walie tu so mnajifanya mmesoma sasa mtaisoma namba
 
Hebu acheni hiyo dhana ya kujadili kama kuna muelekeo wa ukabila acheni sio dalili nzuri na wala uteuzi hauangalii dini wala kabila wewe unaejiita Gulwa acha kabisa upumbavu huo
 
HIVI Kwa Mujibu Wa KATIBA Ya JMT Ya 1977, Mwenye MAMLAKA Ya KUTEUA Wakurugenzi, MAWAZIRI, Ma DC Na Ma RC, RAS, N.k Si RAIS Wa JMT Na Yeye Ndiye Mwenye MAMLAKA Ya Kutengua Uteuzi Wake Pia!!!

SASA Sijui Kisheria MAWAZIRI Wana MAMLAKA Ya KUTEUA Au KUTENGUA Uteuzi Wa Hao Watumishi Au Viongozi!!! MAANA Nasikia Saana Hivi Sasa MAWAZIRI Wakisema Wamefanya Hivyo!!!

NAKUMBUKA Mh. PINDA Alishindwa Kumchukulia HATUA Katibu Mkuu Wizara Ya NISHATI Na MADINI Wa Wkt Ule, AMBAYE Alikumbwa Na Kashfa Ya KUKUSANYA Pesa, Kwa Ajili Ya "KUWAHONGA WABUNGE "Ili Wapitishe Bajeti Ya Wizara Husika!! Kwa Kusema BUNGENI, Laiti Ningekuwa Na MAMLAKA Ya Kumfukuza Kazi, Basi Ningefanya Hivyo Mara Mmoja!!! ILA MAMLAKA Ya Kutengua UTEUZI Wake Na Kumfuta KAZI Ni Ya MAMLAKA Ya UTEUZI (RAIS) Mwenyewe!! HIVYO Namsubiria Atoke Afrika Kusini Nimpatie Taarifa Hizi!!!!! SASA Hawa Inakuwaje!!!!??
 
Back
Top Bottom