Nitahakikisha kuwa kila mwananchi anakuwa na uwezo au kuwezeshwa kupata milo mitatu kwa siku. Hatua za makusudi zitachukuliwa kuhakikisha kuwa kinamama wajawazito na watoto wachanga wanapata lishe bora itakayowasaidia watoto kujengeka vizuri katika viungo vya mwili, kinga ya mwili na ubongo, ili waweze kushiriki kikamilifu katika kujielimisha na kujiendeleza
Niposafarini naelekea Mwanza nasikia kesho terehe 5 Otober 2020 atakuwa viwanja vya Ngokoz/Dampo Mwanza.
nikipata nafasi ntaenda kusikiliza madini ya Lipumba mtaalam wa kunadi sera zinazotekelezwa na serikali adhimi ya CCM chama changu.
Huyu tangu atumiwe na CCM na kukabidhiwa ofisi na hatimye kuhamishia ofisini kitanda, vyeti na mabegi kisa tu anamuogopa maalimu Seifu. Sina Imani naye tena.