Kakke
JF-Expert Member
- Dec 4, 2010
- 1,883
- 1,482
Jumuiya ya Kimataifa imekataa kumtambua Profesa Lipumba kama Mwenyekiti wa Taifa wa The Civic United Front (CUF-Chama Cha Wananchi) kutokana na kuheshimu maamuzi halali yaliyofanywa na wajumbe wa mktano mkuu wa Taifa wa CUF walioridhia na kuthibitisha kujiuzulu kwa Lipumba katika nafasi ya uenyekiti kwa hiari yake mwaka juzi tarehe 5/8/2015. Msimamo huo umetolewa na kiongozi wa vyama vya kiriberali Ulaya Mr. Verhofstadt G. aliyekuwa akiwasilisha muswada wa mapendekezo ya namna ya kuzisaidia nchi za Afrika kupambana na umasikini, na kuziongezea uwezo katika sekta za Afya na elimu. Katika tamko lake hilo Kiongozi huyo amesema “we don’t recognized professor Ibrahim as a Chairman of The Civic United Front Party in Tanzania due to his own will and motion to resign from the post since August, 2015 while his party was in the critical time on preparation for General Election ………However The party National Convention approved his resignation according to CUF Constitution…..” ilisema sehemu ya maelezo yake aliyowasilisha na kusisitiza lazima suala la Zanzibar lipatiwe ufumbuzi wa haraka kama ilivyowekwa ratiba ya utekelezaji. Pia amezungumzia juu ya sheria ya makosa ya mtandao ambayo inaondoa haki na uhuru wa kikatiba kwa wananchi kutoa maoni yao na kuwasiliana baina yao katika kufuatilia utendaji na uwajibikaji wa serikali yao. Mr. Verhofstadt ameelezea kusikitishwa kwake na njama anazofanya Professor Ibrahim Lipumba kuzorotesha jitihada za kulipatia ufumbuzi wa haraka suala la Zanzibar kwa kusababisha ukosefu wa utulivu katika siasa za ndani za Chama cha CUF. Ameeleza kuwa lazima viongozi wa Afrika wajifunze kusimamia maamuzi wanayotoa na kujiheshimu. Jaribio la kutaka kufanya mabadiliko ya uongozi wa ndani ya Chama kwa kutaka kumuondoa Mr. Ismail Jusa –Mkurugenzi wa Mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa hali akijua kuwa Mr. Jusa amekuwa ni kiunganishi muhimu baina ya CUF na Jumuiya mbalimbali za Kimataifa lakini pia ni msaidizi wa karibu wa Katibu Mkuu, Maalim Seif ni jambo lisilokubalika na wapenda demokrasia. Taarifa hizo zimefahamika baada ya aliyedaiwa mteule wa Lipumba wa mambo ya nje kuandika barua ya kujitambulisha kwa Jumuiya ya Kimataifa na kuomba msaada wa fedha kiasi cha Euro 59196.61 ambazo ni sawa na Tshs 140 milioni zilizodaiwa kwa ajili ya kuendeshea mafunzo. Maombi hayo yamekataliwa na kuelezwa kuwa hawatambuliwi.
www.liberal-international.org/news/africa..... February 27, 2017
www.liberal-international.org/news/africa..... February 27, 2017