Profesa Kitila Mkumbo karibu CCM lakini usituvuruge

Kiboko.

JF-Expert Member
Jul 31, 2013
2,891
1,211
Pilipili usiyokula Profesa Kitila inakuwashaje? Baada ya kuteuliwa na Rais wetu Dkt. John Magufuli kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji ukiwa bado mwanachama wa vyama vya upinzani haikuwa shida maana Rais aliamini katika uwezo wako na akiamini maendeleo hayana vyama na hilo lilidhihirika na siyo wewe tu ni wengi tu walioteuliwa kutoka upinzani na kupewa uongozi. Ulifanya vyema na baadae ukahamia kwenye chama cha Mapinduzi ambacho ni chama mama na kilichojengwa kwa misingi mizuri yenye ujamaa na demokrasia ya kutosha.

Tunaamini wewe ni mwanasiasa na ni kitu unachokipenda maana baada ya kuteuliwa ulianza harakati za kugombea ubunge jimbo la Iramba Magharibi pasipo kujali kama hilo eneo linaongozwa na chama cha Mapinduzi.

Uliendelea na harakati za kutaka huo ubunge nadhani hii siyo siri Tanzania nzima inajua kuwa ulipambana kwa nguvu zote kuhakikisha unamtoa aliyepo lakini ghafla ulipotea na kuhamia Ubungo dakika za majeruhi na kuibuka mshindi kwenye kura za maoni kupitia CCM kwa nafasi ya ubunge najua sasa hivi unasubiria kwa hamu uteuliwe ili upeperushe Bendera.

Masikitiko na dukuduku letu sisi wanaCCM ni kwa nini unatumia nguvu nyingi kuwasapoti wapinzani? Au ulikuja CCM kwa kazi maalumu ya kuhakikisha unaivunja CCM? Kama una hiyo ndoto pole sana maana hautaweza hao unaowashawishi wataambulia kuangukia pua ,CCM ya sasa ni imara kuliko jana inayoongozwa na Mwenyekiti bingwa ambaye kakijenga chama kuanzia ngazi ya chini mpaka ngazi ya juu. Hadi sasa tunapoelekea kwenye uchaguzi wanachama wa CCm na wale wasiyo na vyama wataenda kumpigia kura za kutosha kuendelea kuwatumia wananchi.

Huu mpango wako unaoufanya kuwahamasisha madiwani wahamie upinzani ambao kura hazikutosha kwenye udiwani jimboni Iramba Magharibi maana yako ni nini? Iramba huwa hakuna upinzani ila sasa tunaona unaimarisha upinzani kwa kuwapatia watu. Tayari madiwani walioangukia pua sasa hivi wameanza kubisha hodi kwenye vyama vya upinzani kama Kinota JB, Semen Nansolwa, Frank Shila, Henry Nkandi na vikao vilifanyika cha kwanza kilifanyikia kijiji cha Mgela, cha pili Ulemo na cha tatu Ndago.

Tukikuita mpinzani unaona tunakubagua ndani ya chama lakini umetoa maelekezo kwenye kijiji ulichozaliwa cha Mgela kwamba wachague upinzani. Na hii imeishaonekana dhahiri shahiri yule mgombea udiwani kwenye kata yako ya Mtoa tayari kashahamia chama cha ACT Wazalendo. Hata Jeska Kishoa mgombea ubunge kupitia Chadema jimbo la Iramba alivyofika leo kijiji cha Mgela alijinadi kuwa wewe ni rafiki yake hivyo wananchi wasiichague CCM. Acha kuwa popo kuwachanganya watu kama wewe ni mnyama au ndege. Kama umeamua kuwa CCM basi ungana na CCm kukijenga chama kuliko kuwa Ndumilakuwili.

Wako Kiboko.
21a91957-bd80-4e6e-bb70-0d5bfe7ebddb.jpg

9634b2c7-6ca4-4c22-a1ed-effd3215e378.jpg
 
Kitila mkumbo ni jembe

Unapoteza muda na majungu yako humu

Wewe ni nani? Unawezaje kuishi dunia ya wanaojulikana wakati umejificha?
 
Ccm sio chama imara, bali kina kiburi kwa sasa maana mwenyekiti wake anajivunia madaraka ya urais, na yuko juu ya sheria. Hivyo anaweza kuagiza chochote ili kuibeba ccm.
 
Huyu jamaa nilimuona pandikizi
la CCM baada ya kumzuga Zitto eti wapindue uongozi wa chama!!

Zitto akaingia mkenge yakatokea yaliyotokea....ila sema tu Zitto kwa siku hizi za karibuni ame gain uaminifu toka kwa wananchi...amesimama tena na yupo vizuri.

But Lissu kwa sasa anaaminiwa 100% yaani pasi na shaka kwamba ni upinzani wa kweli..hii ndiyo turufu kubwa anayopata mwanasiasa yoyote yule...msimamo wa kisiasa!!.

Hawa waitishe mikutano ya dini weee...Lissu hashuki ndiyo kwanza wanampaisha!!

Kwa wana CCM; Huyu kaeni naye kwa akili sana!! atawavuruga.
 
Mtoa mada acha UJINGA!!! NA we katafute pa kugombea Unamchongea kitila mkumbo ili asiaminike achukiwe ili upate nn. Mbona hatupendani kiasi hiki watu waSingida? Lipi jema kwenu. Alikuja mkamshauri amwachie Mwigulu kakubali. Niko ULEMO unachosema siyo KWELI na hapa Ni nyumbani toka Jana nimekwenda ndago shelui hayo ya kwako una roho mbaya Sana
 
Back
Top Bottom