Profesa Jay ft Juma Nature-Zali La Mentali(Lyrics)

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
20,744
25,445
VERSE 1
(Aaaaaaaaaaaah)
Naamka asubuhi ni kuchwiri tena mapema
Nautoa mkeka sakafuni kisha naukunja vyema
Nawaza nitakula nini mentali kisha naguna
Naanza kujikongoja kichwa chini mikono nyuma
Naelekea kilingeni nilikopaki mkokoteni
Nasaga na rumba kimshazali nyie acheni
Nawapa 'Hi' machizi wananipa 'Peace' tunafurahi
Tunapiga stori nyingi walahi bila maslahi
Mara napata zali napeleka Tanga Uswahili
Wananipa buku mbili danga chee nazisunda chini
Wakati natoka huku kijasho chembamba kikinitoka
Nikaona toto la nguvu nikajikuta nimeropoka
"Dada habari samahani naomba niulize swali"
Akajibu "Maskini koma tafadhali hii ngoma ya gari!"
"Ehee unajua dada...", "We vipi hebu nipishe!"
"Dada mbona mkali?", "Wee kinyago kweli yaishe!"
Nikasema Inshallah hiyo yote kwa sababu ya fukara
Nisije nikakubaka nitupwe selo nikawe kafara
Nikaachana naye sehemu za nyuma akizitingsha
Nilikula kwa macho hali yangu haikuridhisha
Nageuza mkokoteni nakuelekea maskani
Nikawapa stori machizi wakanicheka ikawa utani
Siku moja nililemaa maskani sikuwa na tenda
Na nilikuwa nikitafakari ni vipi siku itakwenda
Kumbe kuna gari ilikuja na kupaki karibu yangu
Sikuweza kuisikia labda sababu ya njaa yangu
Nilishtushwa ghafla na mlio mkali wa honi
Nilipatwa na mshtuko na hofu kubwa moyoni
Kuangalia pembeni ilikuwa imepaki Toyota Surf
Kulikuwa na sura ngeni ya malaika akaomba dafu
Nilisita kunyanyuka kwa sababu nilikuwa mchafu
Na alitoa elfu kumi na alikuwa akitaka dafu
Nilipokea hela alichotaka nilimletea akakipokea
Tabasamu zito akanitolea nilimpa chanji
"Ohh no keep change, una mawazo mengi itakufariji weekend"
Alikunywa maji ya dafu akalitupa na kunikonyeza
Niliganda kama nyamafu nikahisi alinibeza
Alinipa busu la huba shavuni akanichombeza
"I love You!" akawasha gari akateleza

CHORUS - Juma Nature
Zali la mentalii limetokea wakati mimi nina njaa
Nikapendwa na demu mkali
Na kuwaacha watu wote wakinishangaa katika mitaaa

VERSE 2
Zilipita siku mbili nikiwaza kilichotokea
Nikawaza yule ni mtu au jini amenitokea
Potelea mbali uchawi hauendi kwa mentali
Narudi nanyonya napuliza mentali nakuwa shwari
Nabeba rumbesa nakatiza Samora Avenue
Mara kwa ghafla mbele yangu inapaki Toyota Mark II
Ohh napata ghadhabu mara nyingi sipendi dharau
Naifuata gari kuanza kupaka mara nahema juu juu "Aaa" ni yule mrembo"
"Maskini pole sana mzigo mbona mzito kweli utafika nao salama"
Natabasamu "Oh nimeshazoea mama na namshukuru Mwenyezi Mungu kwani hii ni kama karama!"
Anakuwa mnyonge anakata kucha anantazama anaaza kulia anatoa leso anainama
Namwambia "Bibie ni mara ya pili tunaonana
na sidhani kama ni mbaya iwapo tutafahamiana"
"Naitwa Vicky, nina miaka 22, ni mtoto wa kipekee kwenye familia ya kitajiri"
'Oh naitwa Jay ukiniita fukara haukosei
Na naishi kwa nguvu za macho siku zenyewe hazisogei
Alishuka toka garini na kusema "Jay nakupenda!"
Akaruka kwangu mdomoni na kuanza kupata denda
Nilichomoka kwake na kuanza kurudi nyuma
"Tafadhali mpenzi Jay jamani nionee huruma
Acha kubeba mizigo panda ndani kwenye mchuna
Twende Mbezi Beach kwangu upepo unapovuma"
Sikiliza Vicky napenda tuwe marafiki
Lakini hadhi yako hutakiwi kuwa na mtu wa dhiki
Hata wazazi wako naaamini hawataafiki
Tajiri na tajiri maskini sithaminiki
Tafuta kibopa mwenzio ili usishushe hadhi yako
Mimi sistahili hata kuwa kijakazi wako
"Tafadhali Jay usitamke maneno hayo
Naomba unielewe haya machache niyasemayo
Hadi huu wakati mimi nimekupenda kwa dhati
Ukikubali niwe wako nitajiita mwenye bahati"
"Nimeelewa Vicky naomba niwahishe mzigo
Tajiri ni mkorofi anan'subiri migomigo
Na kila nikichelewa mwenzako napata kipigo
Nasaga na rumba jua na mvua kwa mpigo!"
Tuliongea mengi akanipa hela za matumizi
Sikuwahi hata kuziona nilikuwa kama chizi
Niliacha kubeba mizigo penzi letu likaota mizizi
Watu wa uswahili wakasema natumia kizizi.

CHORUS - Juma Nature
Zali la mentali limetokea wakati mimi n'njaa

VERSE 3
Baada ya miezi mitano Vicky alipata ujauzito
Tulifurahi sana mambo yakawa mpwito mpwito
Swala la kwenda kwa wazazi wake halikuwa zito
Walifurahi sana kuniona tukafanya tambiko
Walisema Jay maisha ya Vicky yapo chini yako
Tumefurahi mmpendana kumlea ni jukumu lako
Ilipangwa mikakati kamambe ya kufunga ndoa
Watu hawakuamini kama mimi Vicky nitamuoa
Ilifika siku ya siku mentali Jay ndani ya jumba
Na Vicky ndani ya shela hakuna uchawi wala ndumba
Tulishikana mikono ni nderemo na vifijo
Tukafunga pingu za maisha kanisani bila ya fujo
Furaha isiyo kifani lilifanyika bonge la party
Watoto wa Uswahili walibeba wali kwenye mashati (du)!
Zawadi zilizagaa zilikuwa nyingi tena kemkem
Baba mkwe alitupa Benzi, kiwanda nyumba na BM
Acha zawadi nyingi kutoka kila sehemu
Nilikumbuka nikacheka nilivyoteswa na wale mademu
Mambo swadakta nipo na Vicky ndio my wife
Kidume nang'aa wanajigonga shenzi type (shenzi type)
Nilipokuwa arosto mlinikwepa kama ukoma
Mambo juu ya mstari kunisalimu mnaona noma
Sasa hivi napeta na baridi kali full kipupwe
Mlio nicheka wanataka ardhi ipasuke
Naelekea kilingeni kuwapa dili machizi wangu
Tena mara kwa mara siwezi kuwacha asili yangu
Vicky ni Jay, Jay ni Vicky mustarehe kutoka ndani ya dhiki
Sasa kila siku sherehe ahaaaa!

Mkuu hii ngoma ni Kali sana na haitokuja kuchuja hata Siku moja ila kuna jambo moja na-dought kila nikiwa nazungumzia kuhusu hii ngoma na washikaji.
Iko hv sasa, hii ngoma inasikika sauti ya mda ambaye ana bashasha na kuweza kuflow vizuri na biti..
Iila had I Leo sijamfahamu huyu Dada.. Naomba unitafutie jina lake na hata picha yake
 
Ngoma iliyotufariji sana sisi wasukuma mikokoteni, sema ndo sijui Vicky alikuwa mmoja tu!
 
Back
Top Bottom