TANZIA Profesa Augustine Massawe, Daktari bingwa wa Magonjwa ya Watoto afariki dunia

Lala salama baba. Tunakushukuru sana wa huduma Mungu aliyokuwa amekujalia

Uliitumia vyema karama Mungu aliyoiweka ndani yako

Mwendo umemaliza

---
Daktari Bingwa wa Watoto Dr Augustine Massawe wa Furaha Medical amefariki Dunia leo Jijini Dar es Salaam. Taarifa kutoka kwa familia ni kwamba Dkt. Massawe amefariki asubuhi hii katika hospitali ya Muhimbili alipokuwa amelazwa kwa siku kadhaa kwa matibabu.

Huu ugonjwa ni kama umeelekezwa kwa ma profesa walah!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lala salama baba. Tunakushukuru sana wa huduma Mungu aliyokuwa amekujalia

Uliitumia vyema karama Mungu aliyoiweka ndani yako

Mwendo umemaliza 💔💔💔

---
Daktari Bingwa wa Watoto Dr Augustine Massawe wa Furaha Medical amefariki Dunia leo Jijini Dar es Salaam. Taarifa kutoka kwa familia ni kwamba Dkt. Massawe amefariki asubuhi hii katika hospitali ya Muhimbili alipokuwa amelazwa kwa siku kadhaa kwa matibabu.

Apumzike kwa amani Profesa Massawe.

Mtaani kwetu ndani ya mita 100 leo kuna misiba 2.

Siku za 3, 4 na hata 8 kwa siku ndani ya Wiki zilizopita, tumeishuhudia.

Mungu na akutie nguvu.
 
Lala salama baba. Tunakushukuru sana wa huduma Mungu aliyokuwa amekujalia

Uliitumia vyema karama Mungu aliyoiweka ndani yako

Mwendo umemaliza 💔💔💔

---
Daktari Bingwa wa Watoto Dr Augustine Massawe wa Furaha Medical amefariki Dunia leo Jijini Dar es Salaam. Taarifa kutoka kwa familia ni kwamba Dkt. Massawe amefariki asubuhi hii katika hospitali ya Muhimbili alipokuwa amelazwa kwa siku kadhaa kwa matibabu.

RIEP baba Furaha...Umetibu watoto wetu ambao nao wameshakuwa ma dr. Sasa...Sleep well baba yetu
Mwaka huu Mungu atatie nguvu
Tunapoteza resource ya nchi sijui itakuaje huko mbele
 
Dah! Inasikitisha sana. Mwezi uliopita nilipeleka watoto kule hospitali yake moya Bunju nafikiri. Nikasema afadhali amepata eneo kubwa na ameboresha miundo mbinu. Kumbe yeye anapanga yake na Mungu anamipango yake. So sad!
Linapokuja swala la usawa kifo kinatuweka sawa. Mungu aturehemu na huu upepo.
 
Mungu huwa hatii nguvu wajinga.Kazi yake Mungu ilikuwa ni kutupa akili na alishamaliza kazi hiyo.

Kwamba na hao wa Ulaya na maeneo mengine wanaoendelea kufa hawana akili?

Unaweza kutoa jawabu la wenye akili wanachofanya waepuke kifo? Hali ni mbaya CDC na FDA wako kwenye mijadala mizito kuhusu Booster kwa waliokwishachanjwa dozi zote, hebu tupe mbadala mkuu.
 
Kwa huu mwendo unavyoenda, kila siku vipanga wanavyoondoka, muda si mrefu tutabakiwa na vilaza wa chadomo tu huku mitaani.
Kuwa kipanga yenyewe ni stress tosha, unauchosha mwili.....kama ilivyoandikwa 'akili nyingi huuchosha' mwili. Vilaza wengi ndo maana unakuta wamenenepeana maana akili haifanyi kazi yoyote ya maana zaidi ya ujinga ujinga......
 
2005 nilipata huduma toka kwa huyu mzee pale morocco. Binti yangu aliyezaliwa tu akiwa na siku kama 6. Alikuwa akilia sana muda wote. Akipewa nyonyo ananyonya baada ya muda kidogo analia tena.
Nikampeleka pale. Sitakaa nidharau taaluma ya mtu. Hata akiwa mkuluma.
Mzee masawe akamwambia wife akamue maziwa ajazi kikombe kilikuwa pale. Kukamua kumbe mama maziwa hana na mtoto analia sababu hashibi. Nikaanza kuingia super market kununua mazuwa ya kopo. Kwa sasa ni mkubwa na yupo form two pale St marie Eugen.

Pumzika kwa amani mzee wangu Masawe.
 
Rest in peace Doctor

Mara ya mwisho mwanangu kapata jipu matata sana kichwani, kila mtu anasema hilo la kutumbua tu.

Nikafunga safari mpaka Bunju, mzee kacheki kanipa antibiotics moja tu. Siku tatu jipu kwisha kabisa.

Tupendane jamani, you never know the last time unaongea na mtu
 
Jinsi vifo vya watu maarufu vilivyotawala mitandaoni mwezi huu,ni zaidi ya mwezi wowote ule toka huyu mgeni aingie last year.

Ilikuwa kwa maDon sasa ipo kwa "wanazuoni" pia.
 
Back
Top Bottom