Profesa Anna Tibaijuka: Kumaliza tatizo la machinga kuwe na adhabu iwekwe kwa wanaonunua ovyo barabarani

Ita cost
Sio effective
Too messy
Na itavutia rushwa

Ukimkamata mtu ananunua kwa machinga halafu ana kitambulisho chochote itakuwaje?!

Na hiyo faini italipwaje. Kwa polisi/mgambo aliyekukamata au kituoni?
 
Kuna maswali najiuliza mbona kama wanasiasa wa tanzania baraz Wana uwezo mkubwa sana katka comedy kuliko hata politics Kuna haja yakua halalisha kua politics in tz is directly proportional to comedy

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Mbunge wa zamani wa jimbo la Muleba Prof Anna Tubaijuka amesema tatizo la machinga halitaisha kwa kutoa amri na kuwafukuza mbali bunge linatakiwa kukaa na kutunga sheria yenye adhabu kwa wateja wanaopenda kununua bidhaa hovyo mabarabarani.

Prof Tibaijuka amesema wamachinga hufuata wateja na kama hamna wateja hutamuona machinga kwenye hilo eneo hivyo serikali lazima ijikite kubadilisha utamaduni wa wanunuzi wawe wananunua kwenye masoko maalumu yalitengwa na siyo kununua hovyo hovyo mabarabarani.

Huyu Bibi anazeeka vibaya sana
 
Chamsingi ni serikali kuwa na sera nzuri za kuwainua kiuchumi machinga,unafikiri nani anapenda apange nyanya barabarani anyeshewe na mvua aungue na jua.na ukiangalia idadi ya machinga imeongezeka sana miaka sita hii ni kwasababu ya ugumu wa maisha,umachinga ndio option ya mwisho kwa jobless yeyote
 
Haihitaji hayo yote TRA wakikaza kukamata wasio na risiti lazima machinga wataondoka
Upuuzi mwingine huu. Hayo maduka rasmi tu Kariakoomengi hayatoi risiti yenye thamani halisi.
 
Mbunge wa zamani wa jimbo la Muleba Prof Anna Tubaijuka amesema tatizo la machinga halitaisha kwa kutoa amri na kuwafukuza mbali bunge linatakiwa kukaa na kutunga sheria yenye adhabu kwa wateja wanaopenda kununua bidhaa hovyo mabarabarani.

Prof Tibaijuka amesema wamachinga hufuata wateja na kama hamna wateja hutamuona machinga kwenye hilo eneo hivyo serikali lazima ijikite kubadilisha utamaduni wa wanunuzi wawe wananunua kwenye masoko maalumu yalitengwa na siyo kununua hovyo hovyo mabarabarani.

Kadri unavyozidi kupanua ndiyo kadri unavyozidi kutamani. Mama amesoma hadi nayo masomo yakamsoma.
 
Hii milori iliyojazana kariakoo na vijiofisi vya usafirishaji vipo barabarani kariakoo vimezuia barabara ni kero kilioko wamachinga, ila nasikia ni magari ya wakubwa wa hao ndio biashara zao hawawezi kuondolewaila kwa wamachinga tumeonewa
Malori ni kero kariakoo kuliko machinga
Wameonea watu tu
 
Back
Top Bottom