Prof Tibaijuka lazima ajiuzulu


zanzibar ni kimeo,kama noingekuwa raisi kesho naifanya kuwa wilaya za tanga na dsm,kila kukicha chokochoko hawa jamaa wanzani sisi tunawategemea kwa lipi? Ama kweli hawa jamaa wan roho za waarabu,tunawang'a ng'ania wa nini?
 
kosa ni kubwa sana Zanzibar(mkoa) kuipa hazi ya nchi matokeo yake ndizo hizi chokochoko, yani watu million moja na robo wanatusumbua hivyo, nasikia kichefuchefu kuona Jussa anaendekezwa sana , watu kama hawa ni kuwakata kilimilimi

CCM ndio wanajua ku-deal na hawa wenzao. Seif Sharif Hamad ndio alikuwa anaongoza kwa kidomodomo, siku hizi tangu apewe ruksa kunywa chai Ikulu unamsikia tena? Huyo Jusi Mwitu akipewa kacheo kidogo tu, mambo yoote atayasahau. Ni njaa tu inamsumbua
 
Kilichoombwa ni bahari kuu ya kimataifa sio eneo la Zanzibar JUSSA FIKILI KABLA YA KUSEMA

waelezee hao majuha wasojua kutambua, hapo umepiga ikulu kwenyewe! kilichoombwa hawakijui na wanacholalamika sijui kimetokea wapi!? poor barubaru &co.
 
waelezee hao majuha wasojua kutambua, hapo umepiga ikulu kwenyewe! kilichoombwa hawakijui na wanacholalamika sijui kimetokea wapi!? poor barubaru &co.

Itakuuma sana.

Lakin tunashangaa Je imekuwa nongwa kwa BLW kupitia Jusa kuhoji kuhusu mchakato mzima wa kupeleka hayo maombi?

Ebo kuna siri gani behind maombi hayo?

Lazima kieleweke hapo. Jusa kaza buti na komaeni hapo mpaka kieleweke.



 


Kumbuka vile vile Znz ni nchi kamili yenye mamlaka kamili na hilo limebainishwa katika katiba ya Znz.


Hivi Zanzibar inatambuliwa UN kama nchi? Hivi UN waweza pokea ombi toka kwa mwanachama ambaye si nchi akiishtaki nchi? Zanzibar kwenda kupinga UN wataenda kama nani hadi UN wawasikilize? Hivi CUF wanajua wanachoongea? Hivi UN wanafikiri ni Jimbo la Wawi ambako mwana CUF yeyote aweza enda na kusema lolote.CUF hata wakienda UN nobody will listen to them after all CUF is not a UN member.
 

Naam Waziri wa zanzibar alishiriki lakini hii haina maana kuwa hakuna makosa yaliyofanyika.


Ningependa kukumbusha kuwa suwala la Dowans lilimugharimu Waziri Mkuu sio waziri wa kawaida kama Shamuhuna.
Halafu juu ya uelewa wako unataka tukufahamu vipi? Hii zanzibar haipo na wewe unamtambua Shamuhuna na Serikali ya Mapinduzi, jee hawa wao( SMZ) na Shamuhuna ni kama nani?
Utashi mwengine unaweza kukuondoshea heshima uliyojijengea. Kama Wananchi hawakubaliani na uamuzi wa Kiongozi kwanini uhisi kuwa si jambo la kawaida wakati wewe kama Mwanakijiji umekuwa mstari wa mbele kuwakosoa viongozi na Serikali iliyochaguliwa na wananchi?
 
Kilichoombwa ni bahari kuu ya kimataifa sio eneo la Zanzibar JUSSA FIKILI KABLA YA KUSEMA

Je unaijua bahari kuu weye?
Utawezaje kuizungumzia bahari kuu kwa Tanganyika bila kuihusisha Zanzibar?
Je ongezeka hilo Znz itafaidikaje nalo? kama watafanikiwa ombi lao huko UN, Znz itaongezewa au kupunguziwa eneo lake la bahari kwa kiasi gani?

Kwanini Braza la wawakilishi alikuhusishwa katika mchakato mzima?
kuna siri gani hapo wakti kitu hichi hakimo katika mkataba wa muungano wa Tanganyika na Znz?:eyebrows:nafikiri

hayo ni masuala yanayotakiwa kuulizwa katika kadhia nzima na kufanya Tibaijuka na Shamuhuna lazima wajiuzuru.

 


Fatilia vikao vya Baraza la Wawakilishi kwani jawabu ya mnafiki ni ndogo tu. Umpende au usimpende hiyo ndio Habari ya Wawakilishi wa Zanzibar sio Jussa.
 

Unahangaika bure ndugu yangu kuwafahamisha na kuwapa maana wakati hawajuwi neno lenyewe muungano. Kwao wao Tanzania ni Tanganyika na Tanganyika ni Tanzania wala hawjuwi kuwa kuna kitu Zanzibar.

Kwao wao matusi na kejeli ndio wanachokijuwa na utakuwa mwenzao kama utakuwa unaweza kufanya kama wao tu.
 


Kumbuka kuwa hata Tanganyika haiwezi kufikisha jambo lolote Un kwa sababu haitambuliki kisharia. Na unaposema Tanzania maana yake ni Tanganyika na Zanzibar.

Tunachohoji vipi Tibaijuka waziri wa Ardhi wa Tanganyika apeleke maombi UN kwa niaba ya Tanzania pasi na kuhusisha Znz huusan watunga sharia wa nchi hizo mbili huru zilizoungana kimkataba?

CUF na BLW wameliona hilo japo Chadema wanalipinga kiaina. Kwani hilo sio tatizo kwenu kwani nia yenu ni kuidhulumu Znz na kukuza tanganyika. Znz wameliona hilo na mpaka kieleweke.

lazima mjue Zanzibar ni nchi kamili yenye mamlaka kamili kwa mujibu wa sharia za Znz. Na Muungano wanalijua hilo.


 
Naona kama unajichanganya mwenyewe. Unaposema Tanzania iliwakilishwa ....... na Zanzibar haikuwakilishwa ......, Una maana gani? Unataka kutuambia Zanzibar si sehemu ya Tanzania?
 

Mwanakijiji hii nchi yako ya "Tanzania" ni nchi ya ajabu sana! Ni nchi isiyofuata wala isiyojali kuvunjwa katiba yake au sivyo?



Iwapo Zanzibar ina Katiba yake ambayo inapingana na yako ya "Tanzania" na Hiyo "Tanzania" (unayojidai kuwa ndiyo pekee iliopo katika hili suwala la Muungano) inakaa kimya na kukubali uhaini basi pole Bwana Mwanakijiji huna nchi bali ni kichekesho na hata hilo ombi ndio maana likawa kichekesho, kuchukuwa Watanganyika wote kuwakilisha maombi kwa niaba ya Wazanzibari(kama unavyotaka tuamini) nawe ukashabikia basi nawe unaungana na huo mkumbo wa kichekeshochekesho cha"Tanzania"
 

Ahsantum.

Ni vizuri tuwape Darsa wajue kuwa Tanzania si Tanganyika pekee bali na Zanzibar ipo pia.



 


Naanza kutilia mashaka kamfumo ka elimu kwa upande fulani. Nisingeshangaa mtu aliepata madrasa kama mnavyotuita agekuwa hana uwezo wa kufahamu.
Hivyo wewe hujuwi mfumo wa Muungano au ndio mnaoiba mitihani? Eti upupu! hivyo huoni aibu kuaibisha elimu mbele ya Madrasa?
 
Nimelipenda hilo neno. Rarely huwa linatumika kuelezea hisia kali mtu alizonazo. Ila kwa kumwambia Prof ajiuzuru ni kumuonea. She did not go there as Prof Tibaijuka trust me

Tatizo ni mfumo uleule wa "Wacha tufanye, watapiga kelele lakini hakuna litakalofanywa"
Huyo Tibaijuka alipokwenda alikuwa anajuwa kuwa anachofanya ni dhuluma lakini ndio mfumo na ndio maana Kiwete alitia saini muswada na baadae ndio anakaribisha Wapinzani anajuwa ni povu la soda nae ameshatimiza matakwa yake.
 



Pita tu na kapu lako la ujinga!!!!
 


lazima mjue Zanzibar ni nchi kamili yenye mamlaka kamili kwa mujibu wa sharia za Znz. Na Muungano wanalijua hilo.


Ni sawa ulivyosema kuwa Zanzibar ni nchi kamili kwa sharia za Zanzibar sio za UN.Ni kweli hata muungano tunalijua.Ukienda UN unatakiwa uende na faili la sheria za UN huendi na faili la sharia za Zanzibar faili la sharia za Zanzibar mwisho wake ni bandari ya Zanzibar.
 

Hivyo Karume alihudhuria mara ngapi?
 
Muungano upi huo unaongelea? Muungano wa Tangayika na Zanzibar? Kama ndiyo hivyo basi Prof Tibaijuka ni Waziri wa Ardhi na Makazi wa Tanganyika na Zanzibar (i.e. Muungano)

Acha masaburi bana!

They think alike!! Kwani si huo Muungano unaolalamikiwa au vipi? Utatowaje mifano ya kitu kinacholalamikiwa?
Usipofahamu nani ni Tibaijuka na nani Shamuhuna huwezi kuupigia debe "Utanzania" unaoutaka wewe. Angalau pangefananishwa magufuli na Tibaijuka basi ungekuwa na hoja!
 

Na vile vile Tibaijuka alitakiwa aende na faili la Tanganyika sio Tanzania. Kwani Tanzania ni muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Je unalijua hilo?

Kwani madaraka ya Tibaijuka mwisho msasani wala hayafiki Znz. Kwa kuwa amejivika kilemba cha Tanzania ndipo tunapomuhoji alipewa na nani madaraka ya kuiwakilisha kwenye jambo lisilo la muungano? Je aliowawakilisha wanalijua hilo?

Kwa vyovyote lazima kiungwana ajiuzuru.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…