Rockcity native
JF-Expert Member
- Dec 31, 2012
- 2,174
- 1,460
Habari za weekend wana JF,
Nina swali moja kwa Prof Safari, hivi mbona simwoni katika majukwaa ya M4C au katika harakati yoyote ile ya CHADEMA? Mara ya mwisho kumsikia ilikua katika hekaheka ya uchaguzi mdogo wa Igunga aliposimamia kidete suala la DC kuvuliwa hijabu hapo kidogo alisikika akitetea chama. Lakini toka mda huo sijamwona kwenye harakati yoyote.
Au kuja kwake CHADEMA ilikua nguvu ya soda kumkomoa Lipumba?
MAJIBU toka CHADEMA:

Mkuu,
Prof. Safari yupo, na mbali ya kuwa mwanachama mwandamizi, ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, mmoja wa wanasheria waandamizi wa CHADEMA ambao wamekuwa wakifanya kazi usiku na mchana kupambana na hila chafu za CCM kuvuruga nchi na kuumiza wananchi kwa kutumia mhimili wa mahakama na baadhi ya watumishi wasiokuwa waaminifu wanaoamua kutumikia maslahi ya CCM badala ya maadili yao kwa kutafsiri sheria na kutenda haki.
Ameshiriki katika kutoa ushauri na kushiriki moja kwa moja katika kesi nyingi ambazo ama chama kimefungua au kimefunguliwa kwa viongozi wake kushtakiwa.
Ni mtu anayetumika na amekubali kutoa uwezo na uzoefu wake katika masuala ya kisheria, kisiasa, kijamii na pia kitaaluma, kila anapohitajika kufanya hivyo, kwa ajili ya Watanzania. Anashiriki vikao ambavyo ndivyo vinaamua hiyo M4C. Maana yake yeye na wenzake katika CC, anayo nafasi ya kutoa mchango wa operesheni kufanyika au kutofanyika!
Ni mmoja kati ya wanasheria watakaotambuliwa na chama kama umma utakavyojulishwa karibuni.
Tunasonga mbele kwenda kuwatumikia Watanzania katika nyanja zote, ikiwemo huu utumishi bora na uliotukuka wa akina Prof. Safari na wenzake wengi tu na hapa naweza kuwataja kwa uchache sana sana (maana wako wengi kuanzia ngazi ya taifa mpaka vitongojini na mitaani), Mabere Nyaucho Marando, Method Kimomogolo, Mbogoro, Tundu Lissu, Amani Mwaipaja na watu wengine wenye dhamana mbalimbali ndani na nje ya chama.
Rockcity, nikuulize swali poti wangu, nani aliyesababisha leo hii Peter Kafumu, si mbunge wa Igunga, hata kabla hajatimiza mwaka mmoja bungeni?
Makene